Flora Mbasha Atoa Ushahidi wake Kwa Siri Kuhusu Kesi ya Ubakaji Inayomkabili Mumewe, Emmanuel Mbasha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kesi ya kudaiwa kumbaka shemeji yake inayomkabili mfanyabiashara na mwimba Injili Bongo, Emmanuel Mbasha imeendelea kuunguruma leo katika Mahakama ya Ilala jijini Dar ambapo mkewe Flora alifika na kutoa ushahidi kwa siri.

Kesi hiyo ilianza kuunguruma kwenye ofisi ya hakimu (Chamber), mishale ya saa 5 hadi saa 8 mchana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama wa Wilaya ya Ilala, Flora Mjaya ambapo shahidi namba tatu, Flora aliitwa kutoa ushahidi wake. Kesi hiyo inaendeshwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga na imeahirishwa hadi Aprili 16, mwaka huu.

Siku hiyo, shahidi namba nne ambaye ni daktari anatarajiwa kutoa ushahidi wake na mshitakiwa anaendelea kuwa nje kwa dhamana.
 
Mbasha anashtakiwa kwa makosa mawili ya ubakaji, la kwanza anadaiwa kulifanya Mei 23, mwaka jana, eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam na Mei 25, mwaka jana akidaiwa kutenda kosa hilo kwa binti huyo kwa mara nyingine eneo hilohilo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MMMM KAMA NI KWELI MBASHA POLE SANA!!!!!KAMA UMEPAKAZIWA POLE SANA PIA. FLORA MUNGU ALISEMA SAMEHENI ILI MPATE KUSAMEHEWA NA BABA ALIYE MBINGUNI. MUNGU ANASAMEHE KWAKO INAKUAJE NGUMU WAKATI UNADAI MUNGU KWANZA?????????????DHAMBI ZENU ZIJAPO KUWA NYEKUNDU KAMA DAMU NITAWASAFISHA MUWE WEUPE KAMA THELUJI!!!!KAMA KWELI UNAMPENDA MUNGU MSAMEHE MBASHA!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau ni kweli MUNGU alisema tusamehe na tusahau, nakuunga mkono. Sema najiuliza sasa mahakama na sheria, magereza na polisi waliwekewa kina nani? nani huyo asiyetakiwa kusamehewa anayepaswa kusimama mbele ya sheria? nisaidie mdau wote twende mbinguni mimi na wewe.

      Delete
    2. KWELI MDAU KAMA NI KWELI HATUNA JINSI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE ILA KAMA AMEPAKAZIWA NDIO HAPO WASEME UKWELI ILI WAWE HURU KWA MAANA KAMA MBASHA ATAFUGWA KWA KUSINZIWA FLORA HAUWEZI KUWA HURU

      Delete

Top Post Ad