Gwajima Afunguka......Asema Aliagiza Bastola yake ili Ajihami Baada ya Taarifa Kuzagaa Mitandaoni kuwa Amefariki Dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hii  ni  Picha  iliyosambazwa  katika  mitandao  ya  kijamii  ikidai  kuwa  Gwajima  kafariki  dunia  na  yuko  Mochwari.Taarifa  hizi  zilimpa  hofu  Gwajima  na  kumfanya  Aagize  Bastola  yake  kwa  ajili  ya  kujihami.
**********

Utata umeibuka kuhusu bastola waliyodaiwa kukamatwa nayo wafuasi wa Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima baada ya kiongozi huyo kusema anaimiliki kihalali kinyume na maelezo ya polisi.
  
Gwajima aliyetolewa kwenye chumba cha uangalizi maalumu cha Hospitali ya TMJ jana, amelitaka Jeshi la Polisi kurudisha bastola hiyo, akisema ni mali yake na aliiagiza ipelekwe hospitalini kwa sababu ya kujilinda.
 
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo alipolazwa baada ya kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu akiwa katika mahojiano na polisi, Gwajima alisema anashangaa kukamatwa kwa wachungaji wake waliokuwapo kwa ajili ya kumlinda.
 
Hata hivyo, katika kwa upande mwingine, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema bunduki hiyo haina umiliki halali wa Gwajima wala wa wachungaji 15 waliokamatwa lakini baadaye jioni baada ya maelezo ya Gwajima, alitoa taarifa akisema bastola hiyo ni mali halali ya askofu huyo. Pia alisema kuhusu risasi 17 za bunduki aina ya Shortgun, Gwajima anamiliki bunduki ya aina hiyo lakini akasema uchunguzi kuhusu watu hao 15 unaendelea.

Kauli ya Gwajima
Akizungumza kwa shida akiwa amejishika tumbo, Gwajima alisemaalipopata taarifa za uvumi kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia, aliagiza wachungaji waende hospitalini kwa ajili ya kumlinda, lakini wakaishia mikononi mwa polisi wakidaiwa kutaka kumtorosha.
 
Alisema alihofia kuwapo kwa watu wabaya ambao wangeweza kumdhuru halafu wakasingizia kitendo hicho kufanywa na polisi kwa kuwa alipata tatizo akiwa mikononi mwao.
 
“Usiku wasiwasi ulizidi, huku kila mmoja akiwa hafahamu kwa nini ujumbe wa namna ile unasambazwa kwenye mitandao, msambazaji ni nani, ana nia gani, nikaamua kuwaagiza waniletee silaha yangu iliyokuwa kwenye begi ili likitokea lolote niweze kujilinda,” alisema Gwajima.
 
Alisema alishangaa kukamatwa wachungaji wake na kuchukua silaha iliyokuwa ndani ya begi na hadi jana hakuwa ameulizwa chochote kuhusu umiliki wa silaha hiyo.
 
“Kabla sijazungumza na waandishi kueleza ukweli wa kinachodaiwa kuwa nilitaka kutoroshwa na wachungaji wangu, nilitaka kuzungumza na ZCO (Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu), lakini hajaja, kadi ya ile silaha ninayo,” alisema Gwajima.
 
Alisema madai kuwa alitaka kutoroka ilihali polisi alikwenda mwenyewe akitokea Arusha baada ya kusoma katika vyombo vya habari kuwa anatafutwa.
 
Alifafanua kuwa hata alipofika polisi kwa ajili ya mahojiano hakuwa na shaka hata kidogo, lakini alishangaa kuona anaishiwa nguvu kila baada ya muda na alipoona kichwa kinamuuma, akawaomba wampeleke hospitali ili mambo mengine yafuate baadaye, kitu ambacho hakikufanyika kwa wakati.
 
Wasiwasi kwa polisi
Alisema alijaribu kuomba apelekwe hospitali mara kadhaa, lakini hakuna aliyekubaliana naye hadi alipopoteza fahamu na kupelekwa hospitali ya Polisi Kurasini.
 
“Hivi hata kama ni chombo cha usalama, nimepata matatizo nipo mikononi mwao, halafu nikubali kutibiwa katika hospitali yao, sikulitaka hilo na hata waliposema nikatibiwe Muhimbili pia sikutaka, ndiyo maana nilikuja hapa, sisemi moja kwa moja kama Polisi wanahusika lakini kuna vitu vinanitia shaka,” alisema Gwajima.
 
Alieleza kuwa anatilia shaka Jeshi la Polisi kutokana na kuwapo vitu vingi vinavyoashiria wana kitu kingine wanatafuta, kwani jana tulikuwa na hofu ya kuvamiwa, waliokuja kutuvamia ni wao, sikugombana na Pengo, nilikuwa namkemea kama kiongozi mwenzangu wa kiroho wao, wameligeuza ni kesi.
 
“Sijawahi kulitilia shaka Jeshi la Polisi lakini katika hili napata wasiwasi mwingi, sina ugomvi na Kardinali Pengo, nampenda, hajanilaumu, wala kunishtaki, nilikuwa namkemea katika masuala yetu ya mabaraza ya dini na siyo vinginevyo,” alisema Gwajima.
 
Gwajima pia alionyesha wasiwasi wake kwa kile kilichokuwa kinang’ang’aniwa na polisi kwenda kupekua nyumbani kwake kuwa hakikuwa kitu kizuri.
 
Kova alipinga
Wakati Gwajima akisema hayo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema bastola waliyokutwa nayo wafuasi wa Gwajima haimilikiwi kihalali.
 
“Tumegundua kuwa katika wale watu waliokuwa pale akiwamo Gwajima mwenyewe, (bastola) haikuwa  katika umiliki wao halali, kwa hiyo hapa kuna kesi ya kupatikana na silaha bila kibali.”
 
Akizungumzia tuhuma kwamba polisi walimpekua mke wa Gwajima, Kova alisema hakuna polisi waliofika nyumbani kwake kufanya upekuzi wowote na kama wakitaka kufanya hivyo watafuata taratibu maalumu za upekuzi.
 
Akijibu swali kuhusu mahali Gwajima alipotakiwa kutoroshewa, Kova alisema uchunguzi huo bado unaendelea na utakapomalizika wahusika watafikishwa mahakamani.
 
Pia alipoulizwa kama Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amemsamehe Gwajima, kwani polisi imng’ang’anie, Kova alisema;“amesema anamsamehe lakini haingilii mambo ya sheria.”
 
Kuhusu sababu za Gwajima kuzimia wakati akihojiwa, Kova alisema anayepaswa kuulizwa kwa nini alianguka wakati akihojiwa na polisi ni Gwajima mwenyewe.
 
“Siri za mahojiano huwa hazitolewi kabla ya ushahidi mahakamani, sababu ya kupata shock (mshtuko) atajua mwenyewe, kwa kuwa ukifanyiwa jambo ukafurahi au ukachukia wewe ndiyo unajua ilikuwaje, chochote kitakachotokea ukicheka, ukinuna, ukizimia, wewe ndiyo tukuulize ilikuwaje mpaka ukazimia kwa sababu hisia unazipata wewe,”alisema Kova.

Makonda amtembelea
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye alikuwa amemwandikia Gwajima barua akimwita ofisi kwake, jana mchana alimtembelea hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali kiongozi huyo lakini akasisitiza kuwa nia yake bado ipo palepale.
 
“Nilimtaka leo aripoti ofisini kwangu lakini kwa bahati mbaya anaugua na amelazwa. Nitakwenda kumuona ili nijue hali yake ikoje,” alisema Makonda kabla ya kufunga safari kwenda hospitali alikolazwa.
 
Alisema pia atataka kiongozi huyo wa kiroho amweleze anavyoelewa maana ya uhuru wa kuabudu unaoelezwa katika Katiba, usajili wa taasisi yake na katiba ya taasisi hiyo. 
  
“Mimi ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni. Niliagiza polisi wamkamate na baadaye wakimaliza kumhoji aje kwangu pia atahojiwa na jopo la watu 20,” alisema Makonda.
  
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyie na wazee wa kisasi,mnaendesha sheria kibabe.,hiyo kazi si ya milele na mda si mrefu utakuwa uraiani km sio kaburini.,yanini kuwa waongo na wanafiki????then mkistaafishwa mnarudi uraiani???tunawasubiri kwa hamu mwisho wenu kesho ya baadae wote mnaosingizia kwa chuki....,

    ReplyDelete
  2. wote tutaangaika na dunia mwisho Akuna roho ya mwanadamu wala kiumbe chochote kitabaki dunia hii Akuna mtu anaefanya agano na mungu la kuishi duniani walukuepo watu nchi hii walipita wenye heshima kubwa wote wako kwenye makazi ya milee ya mwanadamu yani aridhini ngoja tuone wenye sharia ya duniani hapa kama watashinda unamtendea binadamu mwenzio mwenye damu na nyama na wote mpo sawa nanyi mtatendewa hivyo hivyo mungu tusamehe mamlaka za dunia ndivyo zilivyo

    ReplyDelete
  3. Hao wanao watumia jueni kwamba wanapita katika hii dunia wali;ikwepo watu nasifa walio nyanyasa watu wenye haki zao lakini wako wapi wamepita na hawapo imebaki historia kweli pesa inafanya mtu na haki yake anyanyaswe kuna watu wapo wanakula pesa za wananchi bila huruma lakin mmewafanya nini kwa nini mkubali kutumiwa vibaya na kumzalilisha mtu mnashindwa kuongea ukweli mnasingizia Mungu anaona achenikutumiwa nawatu wenye pesa mnaharibu nchi yetu haki huinua taifa laikini rushwa ni aibu kwa taifa acheni kunyanyasa watu mtahukumiwa hii dunia inapita hautaondoka na hao wanaokutumia peke yakao ndani ya kaburi na utasimama kutoa hesabu pekeyako Tanzania tunakwenda wapi kuweni na hofu ya Mungu Ogopeni kuongea uongo mtakufa vibaya tena kifo cha aibu Muogopeni Mungu gwajima mungu akutie nguvu nakuombea afya yako iimerike vita yetu si katika damu na nyama bali katika roho mungu bado yupo utashinda hilo ndo jaribu lako jua utashinda kwa msaada wa Mungu na ijili itasonga mbele lazima shetani aibishwe na ataabika pamoja na maajenti wake

    ReplyDelete
  4. Hivi mnaandika nini? Gwajima sijaona utetezi wake. Alilazwa yeah so hakuona hao police kama ndo walinda watu? Na je why afikirie kitu kibaya kama hicho kuhusu police? Inamana huyu huwa hajiamini kabisaa. And why ahitaji bastola takujilinda kama yeye ni mchungaji kweli so huyo Mungu unamuabudu kila siku hawezi kukulinda Gwajima? Why unataka kujichukulia mambo kivyako vyako huwaheshimu police? Ulitaka ujihami vipi kuhusu Nguo na hati yakusafiria? Hao wachungaji wenzio hawana ibada mi nafikiria pasaka hii wangeshinda makanisani kukuombea upone? Malipo ni hapahapa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hiv nyie ongeeni mkitumia akili watu wenye nia mbay utawaona kuna uhusiano gani wakosa alilofanya nakuanza kumhoji malizake amezipataje hapo kuna uhusiano kweli auna nyie mnaandika kwa vile mnaandika tu kwa sababu mnataka monekane mmekomenti kama alianza kuwambia anajisikia vibaya wampeleke hospitali hawakutaka mpaka walipo ona ameziai sasa utasema kwenye vyombo vya usdalama kuna usalama kweli palipo naukweli sema kweli na nanafisi yako ikushuhudie wao ndio wamekua watu wa kwanza kuwaumiza wataznzania hapo kuna kitu nyuma yake nivitu vya kushangaza sana mtu kaitwa kwaajili ya kutoa lugha chafu lakini anaendakuhojiwa vitu vingine malizake zinahusiana nini aliekwambia watumishi wa Mungu ni masikini ni nani watumishi wa Mungu ndo wanatakiwa wawe matajiri kuna watu nimatajiri mbona hamwafatilii tuulize hizo mali wamezitoa wapi kuweni na utu kama mmeagizwa na nyie mshindwe vyombo vya usalama imekua kama unaenda kuadhibiwa wewe unaongea nini eti polic pana usalama kosea siku moja uone kama pasasalama ilikua zamani sio saivi watu wamependa pesa kuliko utu wa mtu rushwa ndo inaanzia kwenye usalama wewe unaongea nini acheni uongo acha kutetea kitu ambacho kinaumiza....

      Delete
  5. Hivi hizo suti mbili na passport nazo ni kwa ajili ya kujilinda au hospitali wanahitahi passport?

    ReplyDelete
  6. Mi nashangaa sana watu wanaona Gwajima anaonewa mbona hali kama hiyo ikitokea kwa masheikh hatuoni mkilalamika na kunung'unika eti ooh dunia ya kupita tu ila wakifanyiwa masheikh mnaona sawa tu,watanzania tuache unafiki sheria ni msumeno acheni ifuate mkondo wake tena mi naona wamemkosea sana ilitakiwa akong'otwe na hata meno japo mawili wangeyakwanyua bila ganzi.

    ReplyDelete
  7. Hata kucha moja hawajamtoa mnalalamika!

    ReplyDelete
  8. Sheria ifuate mkondo wake.kama kavunja sheria basi imhukumu na si vingine.kwani gwajima ndio nani?halfu kumiliki siraha zote hizo nawe ni kiongozi wa dini unachohofia ni nini?mungu si ndio mlinzi wako mkuu na kila siku mnapiga kelele makanisani.acheni unafiki nyinyi wachungaji.

    ReplyDelete

Top Post Ad