Mwigizaji Jack Wolper Ashutumiwa Kumpiga Mizinga Mume Mtarajiwa na Wastara Juma

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwigizaji Wastara Juma, akiwa na mume wake mtarajiwa Mark Edi.
Gazeti la Risasi Limetoa Shutuma Kubwa kwa Mrembo na Muingizaji Jack Wolper ya kuwa huwa anampiga mizinga Mume mtarajiwa wa Wastara...

Chanzo hicho cha hii Habari Kimehabarisha kama ifuatavyo:


AIBU! Staa wa sinema  za Kibongo, Jacqueline Wolper amedaiwa kuwa na tabia ya kumpiga mizinga (kuomba fedha) mume mtarajiwa wa mwigizaji Wastara Juma, Mark Edi.

Chanzo makini kilicho karibu na Mark ambaye ni mfanyabiashara mwenye maduka ya nguo jijini Dar, kimepenyeza habari kuwa, kabla ya kuanzisha uhusiano na Wastara, Mark alikuwa na uhusiano na Wolper lakini alimshindwa kutokana na tabia hiyo ya kupiga mizinga.

“Yaani Wolper ni balaa, anampiga sana mizingamizinga jamaa, mara anataka elfu 25, mara 30 yaani ni balaa tupu hadi ikafika steji Mark akaamua kumpiga chini na kutulia na Wastara,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kugaiwa ‘ubuyu’ huo sambamba na ushahidi wa SMS zilizoonesha Wolper akimuomba Mark fedha, mwanahabari wetu alimtafuta Mark ili kuweza kujua kama madai hayo yana ukweli ambapo alipopatikana alikiri na kudai amemchoka mwigizaji huyo.

“Daah! Umezipataje hizo habari? Ni kweli Wolper alikuwa mtu wangu lakini kwa sasa sina habari naye, ni mtu muongomuongo, mizinga kila wakati hadi nikaona bora niachane naye nitulie na Wastara,” alisema Mark ambaye kwa sasa wanapika na kupakua na Wastara.

Jitihada za kumpata Wolper ili aweze kufunguka kwa upande wake hazikuzaa matunda kwani simu yake iliita bila kupokelewa, jitihada zinaendelea.

Je una Maoni Gani Kuhusu Hii Habari?
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad