Wahalifu wa Mitandao, Wasambaza Picha za Utupu na Ngono na Wasambaza Uongo Mitandaoni Kwenda Jela Miaka 10 ama Faini Mil 50

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAHALIFU wa mtandao pamoja na wasambazaji wa picha za utupu na ngono, wasambazaji wa taarifa za uwongo, za kibaguzi na matusi na watu wengine ambao wanafanya udanganyifu unaohusiana na kompyuta wametungiwa sheria kali ambayo itawafanya kwenda jela hadi miaka 10 au kulipa faini isiyopungua Sh milioni 50.

Miongoni mwa miswada ya sheria utakaowasilishwa bungeni na Serikali wiki hii mjini hapa, ni Sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 ambayo imeainisha makosa mbalimbali yanayofanywa na wananchi katika kipindi hiki ambacho matumizi ya mtandao wa kompyuta yameongezeka.

Baadhi ya makosa yaliyoainishwa kwenye sheria hiyo ni kughushi kunakohusiana na masuala ya kompyuta, udanganyifu unaohusiana na kompyuta, ponografia za watoto, picha za utupu, matusi na ngono, makosa yanayohusiana na utambuzi, uwongo, ubaguzi, matumizi ya kibaguzi, mauaji ya kimbari na unyanyasaji kupitia mtandao wa kompyuta.

Katika sheria hiyo, mtu atakayesambaza ponografia ya watoto kupitia mtandao wa kompyuta atawajibika kulipa faini isiyopungua Sh milioni 50 au mara tatu ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au kifungo kisichopungua miaka saba jela au vyote kwa pamoja.

Mkosaji pia ataamriwa kumlipa mwathirika fidia. Kwa upande wa kusambaza picha za ngono, matusi, uasherati atalipa faini isiyopungua Sh milioni 30 au kwenda jela miaka 10 au vyote.

Lakini mtu atakayesambaza picha za utupu atalipa faini isiyopungua Sh milioni 20 au kwenda jela miaka saba au kutumikia adhabu zote kwa pamoja.

Pia kweye muswada huo mtu ambaye atatoa taarifa, data au maelezo kwa njia ya picha, maandishi, alama au aina nyingine yoyote zikiwa ni za uongo akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua Sh milioni 3 au kutumikia kifungo jela kisichopungua miezi sita au vyote.

Kwa upande wa ubaguzi, sheria hiyo inakataza mtu kutumia mtandao wa kompyuta kutozalisha vitu vya kibaguzi kwa madhumuni ya kuvisambaza na iwapo atatiwa hatiani atalazimika kulipa faini ya Sh milioni tatu au kifungo cha mwaka mmoja jela.

Pia mtu akimdhihaki mtu mwingine kwa kupitia mfumo wa kompyuta kwa mwelekeo wa ubaguzi wa rangi, kabila, asili, utaifa au dini fulani akitiwa hatiani atatozwa na Mahakama faini ya Sh milioni tatu au kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote kwa pamoja.

Pia sheria hiyo inakataza mtu kuchapisha au kusababisha kuchapishwa vitu vinavyochochea au kuhalalisha matendo yanayopelekea mauaji ya kimbari na makosa dhidi ya binadamu kwa kupitia mtandao wa kompyuta.

Mtu atakayefanya hivyo atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua Sh milioni 10 au kutumikia kifungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Pia muswada huo wa sheria unakataza mtu kutoanzisha usambazaji wa taarifa zinazotumwa bila ridhaa na ukitiwa hatiani utatozwa faini ya Sh milioni 3 au mara tatu ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au kutumikia kifungo kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. safi kabisa kuna watu wanatabia chafu za kutukana kila leo nikuvunjia heshima tafadhali tahadhari uko ndani aunje ya nchi ukitukana mtu ukitia mguu tanzania tutakushuhulikia Mange ukiwa wa kwanza

    ReplyDelete

Top Post Ad