AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Kajala Masanja:
Tangu aingie kwenye bifu na Wema Sepetu, kuna kundi ambalo linajiita Team Wema limekuwa likimshambulia kwa kumtukana na kumshutumu kwa mambo ambayo mengine hayana ukweli.
Hata hivyo, Kajala anaonekana kuwa mstaarabu kidogo kwani licha ya kutukanwa mtandaoni, yeye amekuwa mkimya akijua kujibizana na watu hao ambao wala hawana majina ni sawa na kuzidi kujichafulia.
Elizabeth Michael ‘Lulu’:
Huyu naye ni mhanga wa matusi mtandaoni. Kuna kundi la watu ambao linaonekana kuwa na chuki dhidi yake, huenda kutokana na mafanikio aliyonayo akiwa kwenye umri mdogo.
Lakini sasa, licha ya matusi anayoyaoga mtandaoni, amekuwa mvumilivu wa kuyaacha yapite. Watu wake wa karibu wanaeleza kuwa, licha ya kutukana sana mwenyewe wala hajui kwamba anatukanwa kwani si mtu wa kufuatilia nani kasema nini kibaya juu yake
Wema Sepetu:
Kama ilivyo kwa Kajala, huyu naye anashambuliwa sana na Team Kajala. Hawa ni watu ambao wamejitenga kuhakikisha wanamkosesha amani staa huyu.
Amekuwa akitukanwa kwa mengi lakini kwa kuwa anajua ustaa ni kama jalala, huwa hajali na anachukulia poa.
Ni mara chache sana amekuwa akinyanyua mdomo wake kuwajibu wale ambao wamekuwa wakimsema vibaya sambamba na kumtukana.
Kwa uchache hao ndiyo mastaa ambao hivi karibuni wametia fora kwa
kutukana na kutukanwa mtandaoni.
Tahadhari
Mastaa ambao ni wepesi kutukana mtandaoni wajue kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete atasaini ile sheria ya makosa ya mtandaoni ya mwaka 2015, watajikuta wanaenda jela hivi hivi.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
Wanaf*****lwa wote na mwenye kusaini
ReplyDelete