Mbunge Sugu Atoa Chozi Bungeni..Adai Suala la Mtoto wake na Faiza Ally ni la Kifamilia..Adai Bado Hajamchukua Mtoto Kutoka Kwa Faiza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jana Katika Bunge Huko Dodoma Mheshimiwa Mbunge Mlata Alisemama Haya:

"Tuna Mbunge mwenzetu amemnyanyasa mwanamke mwenzetu ametumia siku moja Mahakamani kumnyang’anya mtoto wa miaka miwili.. Mbunge huyu anajijua kwa sababu mwanamke huyo anaitwa Faiza.. Faiza arudishiwe mtoto wake"

Sugu leo amesimama Bungeni na kulitokea Ufafanuzi swala hilo na Mahakama kumpa haki ya kumlea mtoto kutoka kwa Mama yake Mzazi Faiza Ally..

“Mheshimiwa naibu spika, kwa vile masuala haya binafsi mimi na mzazi mwenzangu na binti yetu, yameletwa hadharani mbele ya bunge tukufu, kwa vile masuala haya ni binafsi na ya kiunyumba yamevishwa joho la haki za wanawake na watoto na tuhuma nzito kutolewa juu yangu, mimi nalazimika kwa masikitiko makubwa na moyo mmzito kabisa kuyazungumzia hadharani mbele ya bunge lako tukufu,” alisema Sugu.

“Mheshimiwa naibu spika binti yangu Sasha Desteria anaishi Dar es Salaam na mama yake tangu alivyozaliwa tarehe 26 September 2012 na katika kipindi chote hicho mimi nimempelekea mama yake takriban shilingi 500,000 kwa mwezi kwaajili ya matunzo ya binti yetu kila mwezi. Aidha tangu awe na umri wa miaka miwili mimi nimemlipia Sasha ada yake ya shule takribani milioni 3 kila mwaka ambayo ni shilingi 750,000 kwa semester. Malipo haya ni nje ya fedha za nguo, chakula, vifaa vya kuchezea watoto pamoja na kulipia gharama za television za watoto ya cartoon katika kipindi chote tangu binti yangu alipozaliwa.

10852938_800529123337629_414595070_n
Faiza na Sasha

Mheshimiwa naibu spika, mzazi mwenzangu anayedaiwa kuwa mwanamke mnyonge na mheshimiwa Mlata, ni mwanamke anayejulikana katika kumbi za starehe karibu nchi nzima kwa kutokuwa na haya mbele ya hadhara wala mbele ya jamii. Ni mwanamke katika sherehe za tuzo za Kilimanjaro Music Awards zilizofanyika jijini Dar es salaam mwezi mmoja uliopita, alivalia nguo ambazo ziliacha sehemu zake za siri hadharani ili mpita njia azione. Picha zake katika mavazi hayo zilisambaa katika mitandao ya kijamii ya kuleta fedheha kubwa kwangu binafsi na bila shaka kwa watanzania wote wanaojali maadili katika masuala ya mavazi ya hadharani.

Kabla ya hapo picha zake nyingine wakati amevalia nepi ya mtoto yaani Diapers na kisha kusambaza katika mitandao ya kijamii. Kama angetaka mheshimiwa Mlata angeweza kupata taarifa hizi kabla ya kurusha tuhuma nzito ndani ya bunge tukufu,” alisisitiza Sugu.

Pia Sugu alizungumzia jinsi alivyolipeleka suala lake mahakamani mpaka mahakama kutoa uamuzi wa kutaka Faiza amkabidhi mtoto kwa Sugu.

“Mahakama ya mwanzo Manzese iliridhika na ushahidi wangu kwamba mzazi mwenzangu hakuwa na maadili yoyote ya kuweza kumlea mtoto wetu. Mahakama hiyo iliamuru kwamba binti yetu Sasha Desteria akabidhiwe kwangu ili niweze kumlea katika mazingira ya maadili ya usawa kwa mtoto na kwa umri wake. Hivyo mheshimiwa naibu spika kile ambacho kimedaiwa na mheshimiwa Mlata cha uporaji wa mtoto kiukweli ni amri halali ya mahakama ya Manzese iliyotolewa baada ya kusikiliza pande zote kuzingatia ushahidi uliotolewa.”

Hata hivyo Sugu alisema bado hajamchukua mtoto huyo kutoka kwa Faiza, na kwamba kuna uwezekano wa kufanyika mazungumzo ya kifamilia kulimaliza suala hilo kwa amani.

Mwisho Sugu alipomaliza Kuongea Alionekana Akitokwa na Machozi Usoni Mwake...

Je una Ushauri Gani kwa Sugu ?
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. chukua mtoto wako tabia gani hizi

    ReplyDelete
  2. Suguvka chemka kwanza katumia ubunge wake kumnyanyasa faiza, pili mavazi ya mtu haijalishi kama kaenda kwenye stare na kumuacha mtoto kwenye mikono salama shida iko wapi changudoa wangapi wana lea watoto wao? Katumia cheo chake kuvibaya hukumu siku 2? Hata hakimu aliyetoa hukumubawajibishwe.

    ReplyDelete
  3. Wayamalize kifamilia na mtoto akae na mamake,
    ila Faiza aonywe na akirudia ujinga wake Mhe.Sugu achukue mtoto.

    ReplyDelete
  4. BABA BORA SANA!!!!

    ReplyDelete
  5. nawashangaa wote waliomshutumu sugu sio kosa lake kabisaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  6. Mwambieni Mange Kimbambi aache kuingilia mahusiano ya watu dada anamdomo yule sijawahi kuona kila mtu anataka kugombana nae hivi faiza ingenguwa ndugu yake angefurahia hali hii ya kukaa uchi, au sugu angekuwa kaka yake ndiyo amezaa na huyu kituko angefurahi ndiyo maana anakonda kwasababu ya mdomo kijitu chenyewe kibaya kujipodoa kila dakika miguu njiti suburi uje dar sugu akutie adabu utakula mitama hadi akili ikukae sawa umezidi umbeya dada pumguza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mange mwenyewe ndoa yake imemmshinda ila simshangai lazima amsupport changu mwenzake.

      Delete
    2. Muachane mengi ameongea ukweli mtupu, wabongo bwana kushabiki upumbabu Tu, zaa mtoto Wako uone,

      Delete
  7. We nae toa ujinga hapa kazi kumwandama mange, mange yuko sawa 100% yule mtoto akae na mamake dunia ya sasa imeharibika,unamwita mange nji we spoku za baiskeli basi kafie mbele mna roho mbaya sana nyie, yule mtoto no mdogo sana.

    ReplyDelete
  8. Hakuna kama mama, mama ni mama tu, wenye roho mbaya wanataka mtoto akae na babake, faiza kakosea ndio lakini sio haki kumchukulia mwanae duu kazi kweli kweli!!!!

    ReplyDelete
  9. Nyie wore mnaomfagilia sugu hamjazaa, km umezaa ndio utajua uchungu WA mwana,there is no where in the world mtoto Ana nyanganwa kwa mama eti mavazi, hai kina flavian matata,happiness magesa,hoyce temu Leo mi watu wanaothaminika ktk jamii kutokana na miss,flavian matata Ana fanya umodo huko us kwa kuvaa hadi bikini, who don't know that mbona serikali inamtimia km balozi, ache kubwabwaja mchungu WA mwana anaujua mama.

    ReplyDelete
  10. wewe AnonymousJune 26, 2015 at 5:22 PM ni PUMBAFU KABISA, sababu ya kumchukua mtoto siyo mavazi bali ni TABIA mbaya ya mama.ebu fikiria mwanamke anayeweka matako yake hadharani anaweza kumlea mtotot? yaani wewe ni PUMBAFU KWELI KWELI umewahi ona wapi ma-modo wana weka matako yao hadharani NG'OMBE WEWE .... samahani kama natukana ila ki ukweli ameniudhi sana huyu... kama kuweka MATAKO hadharani ni sawa basi na wewe weka ya kwako PUMBAFU wewe

    ReplyDelete
  11. We anonimous 12:44 na ww acha upumbavu Kama tatizo kuvaa mavazi ya hasara mbona hata Wema anavaa sana mavazi ya hasara na sasa anataka kuingia bungeni. Ina maana na yy asipigiwe kura kwa yale mavazi yake ya kihasara??? Wewe ndio ngómbe. .

    ReplyDelete

Top Post Ad