Mchezaji Mrisho Khalfan Ngassa Atoa Rasmi Sauzi Afrika Akiwa na Mkewe 'Nimekuja huku kuhamia rasmi sasa, tunakwenda kuangalia nyumba'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ngassa na Mkewe Radhia
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amewasili nchini Afrika Kusini leo tayari kwa maisha mapya katika klabu mpya, Free State Stars ya Bethlehem.
Mchezaji huyo wa zamani wa Kagera Sugar, Azam FC na Simba SC, Ngassa ametua Johannesburg leo asubuhi na kuunganisha safari kwa gari la dogo la Free State kwenda Bethlehem.
Ngassa ametua na mkewe, Radhia Enea Mngazija na watakwenda kukagua nyumba aliyopewa na mwajiri wake, tayari kuanza maisha mapya.

Nimekuja huku kuhamia rasmi sasa, tunakwenda kuangalia nyumba mimi na bibie (Radhia). Unajua mambo ya nyumba ni ya akina mama. Sasa yeye akisema ameipenda nyumba, nawaambia safi, tunaingia,”amesema.

Hata hivyo, Ngassa atarejea Dar es Salaam wiki ijayo kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinachokwenda kucheza na Misri mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika katikati ya mwezi.

Nadhani sitakuwa na muda mrefu, viongozi niliwaambia kabisa natakiwa kwenye kambi ya timu ya taifa. Kwa hivyo wanajua. Natarajia kurudi wiki ijayo tu kujiunga na timu ya taifa,”amesema.
Ngassa amejiunga na FS mwanzoni mwa mwezi huu kwa Mkataba wa miaka minne, kama mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake Yanga SC.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad