Miss Tanzania Amchokoza Zari, Yadaiwa Ana Mahusiano ya Kimapenzi na Mwanamuziki Diamond Platnumz

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa katika pozi na miss huyo.
Musa mateja
Madai mazito! Mshiriki wa Kinyang’anyiro cha Miss Tanzania 2011/12 ambaye alianza harakati za kunyakua taji hilo akitokea Mkoa wa Shinyanga na baadaye kutwaa Taji la Miss Kanda ya Ziwa, Glory Samwel anadaiwa kumchokonoa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa kile kinachodaiwa kuwa ana ukaribu wa ‘kimalovee’ na mpenzi wa Zari, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Chanzo cha ‘unyunyuzi’ huo kilitonya kwamba, mlimbwende huyo amekuwa akionekana mara kwa mara akijivinjari na Diamond jambo ambalo wadau wamelishtukia na kubaini kuwa ana mpango wa kuingilia penzi la Zari na kusambaratishia uchumba wa wawili hao.

Ijumaa Wikienda lilinyetishiwa habari hizo hivi karibuni na kuamua kuzifanyia kazi hatua kwa hatua, ambapo liliweza kujiridhisha kwa baadhi ya matukio ya picha ambazo mrembo huyo amekuwa akipiga na Diamond.

Mbali na picha pia kuna matukio ya sherehe za ‘bethidei’ ambazo Diamond alionekana akiwa karibu na mrembo huyo.

Ukiachilia mbali uchunguzi huo, mwanahabari wetu alimtafuta mrembo huyo kwa lengo la kutaka kujiridhisha juu ya madai hayo ambapo alikiri kuwa na ukaribu na Diamond huku akifafanua kwamba uhusiano wake na jamaa huyo si wa kimapenzi kama wengi wanavyomchukulia.

Hizo picha za karibu zaidi ni zile ambazo tulipiga kwenye bethidei ya meneja wa Diamond aitwaye Salaam, ambayo ilifanyika pale nyumbani kwake (Salaam) Kijitonyama (Dar) hivi karibuni.

Ni kweli watu wengi wananituhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond lakini si kweli maana ninajuana naye kawaida tu,” alisema Glory.

Kwa upande wa Diamond aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa ni kweli anamfahamu Glory ila si mpenzi wake na anachokijua ni shabiki wake kama ilivyo kwa wengine.

Alisema hata picha alizopiga naye hakuna picha za hovyo maana zilipigwa hadharani.

Glory ni shabiki wangu wa kawaida tu kama ilivyo kwa mashabiki wangu wengine, suala la kupiga naye picha halimaanishi ni demu wangu,” alisema Diamond.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Project zinaanzaga hivohivo

    ReplyDelete
  2. huyu ataondoka na filimbi sasa maana hata ngoma itamuogopa!

    ReplyDelete
  3. Daimond ni mtoto wa mjini amezoea kuwa huru kufanya anachotaka na wakati anaotaka, kuwa na Zari ni kama mtu aliyeangingia maji sasa inabidi ayaoge. Zari yupo dunia nyengine na Daimond nyengine nasasa kuwa ni lazima ili kuwa pamoja ni mmoja amfuate mwengine na sasa inaonekana Daimond ndiye anaeyakopi maisha ya Zari, sasa amekuwa kama anacheza kamari ya apande chati au aanguke kwa jinsi maisha ya zari yalivyo. Kwa sasa inaonyesha Daimond anayamiss maisha aliyokuwa nayo ya kuwa huru anampenda amtakae, anakwenda atakapo anakula chochote na popote anakotaka.Sasa tusione anahangaika kuna vitu vingi anavikosa na anavitamani lakini amekuwa kama kondoo aliyefungwa kamba shingoni, wanawake wengine hatari wanaweka mrija anyonye vizuri ikitokea siku akiona huyu hana damu tena atakuona hufai atatafuta sehemu nyengine akaupachike maana kati ya Daimond na Zari hakuna mapenzi ila ni show tu ndiyo maana Daimond anatafuta penzi kwengine.

    ReplyDelete

Top Post Ad