Mpambano wa Mengi na Manji Wapamba Moto...Manji Atangaza Kuwa Atajiuzulu yanga iwapo Aliyosema Mengi yatakuwa ni Kweli..Ataka Mdahalo wa Yeye na Mengi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema atajiuzulu wadhifa wa uenyekiti iwapo itabainika kuwa kweli yeye ni fisadi, mwizi na muongo kama ambavyo Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi amekuwa akisukuma mashambulizi dhidi yake.

Manji amezungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Yanga, jana na kueleza hayo huku akisisitiza kumtaka Mengi ajitokeze na wakutane kwa ajili ya kufanya mdahalo wa wazi ambao utadhibitisha kuhusiana na tuhuma hizo.

Alisema kuendelea kuiongoza Yanga wakati imethibitika ni fisadi na mwizi, ni utovu wa nidhamu na wanachama wa klabu hiyo watamtilia shaka.

Bilionea huyo aliyasema hayo jana Jumapili, mbele ya wanachama wa klabu hiyo kwenye mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Yanga, makutano ya Mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar.

Manji alifunguka kuwa Mengi amekuwa akimsakama kwa muda mrefu na sasa amesema amechoka.

Manji anadai kilichomchefua zaidi ni habari iliyotoka kwenye Gazeti la Nipashe kuwa kampuni yake ya Farm Equip Tanzania and Quality Garage, ijulikanayo kama QG Engineering ilishindwa kulipa kiasi cha bilioni 9.055 serikalini.

Manji amekanusha taarifa hiyo na kuomba Julai 3, mwaka huu kukutana na mmiliki wa gazeti hilo, Mengi kwenye mdahalo ‘live’ na kila upande uje na ushahidi wa kutosha kisha Watanzania wapige kura ili muongo na mkweli ajulikane kuliko kuchafuliwa jina.

“Iwapo itabainika kweli mimi ni fisadi, muongo na mwizi, niko tayari kuachi ngazi ya uenyekiti wa Yanga na sitagombea cheo chochote hapa, maana klabu itakuwa inaongozwa na mtu asiye na vigezo sitahiki vya kuwa kiongozi,” alisema Manji.

"Watu wanapaswa kujiuliza, mimi ni fisadi ninayejulikana na vyombo vya habari vya IPP tu? Wengine hawaoni hilo? Je, kwa nini IPP pekee ndiyo waone mimi ni fisadi? hapo watu wajiulize," alisema Manji.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MAKUBWA!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. huyo mengi kazoe sana ni mnafiki akiona mtu kamshinda kibiahashara na kifedha yeye umuandama

    ReplyDelete
  3. Hayo maneno yamesemwa bungeni, Nipashe wao wame'quote' tu, hata hivyo kwani hiyo story aloiandika ni Mengi? Hebu muulizeni Mani ile faini ya 'shillingi moja' aloidai Mengi kipindi kile cha kesi yao alishalipa? Hawa wote ni 'waarabu wa pemba' wanajuana, huo ugomvi wao haukuanza leo.........wala jana..... ni wa tangu 'enzi za mwalimu'........

    ReplyDelete
  4. Labda niseme kuwa bw Manji anaonewa kwa muda mrefu toka alipouziwa maeneo ya kiislam pale chang'ombe opposite na primary school imekuwa nongwa kwake. Mgogoro huo unachangiwa sana na Manji kuiongoza Yanga kwa mafanikio kuliko yeye aliyeishia njiani. Pili Manji ni mkereketwa wa Ccm na mwingine ni wazi yupo ukawa. Mzee Mengi aache tabia mbaya ya kutaka kila kitu apate yeye. Kuna msemo kuwa kabila lake linaamini kuwa fedha yote ni yao.

    ReplyDelete

Top Post Ad