Breaking News: BASATA imemfungia Shilole Mwaka Mmoja, Hakuna Kufanya Muziki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shilole Akiwa Jukwaani Huku Mali zake Zikiwa Nje Nje...
Breaking news zilizoifikia usiku wa July 30 2015 kutoka Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) ni kwamba baraza hili limemfungia Shilole kutojihusisha na kazi yoyote ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.

Barua iliyoifikia  imeandikwa kutoka BASATA imesema >>> ‘Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili‘

‘BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa maelezo yako‘ – BASATA

‘Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae ‘ – BASATA

Je ni Sawa Kwa Shishi Kufungiwa?

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. powa kabisa maana huyu kazidi

    ReplyDelete
  2. 100% kuku wa kienyeji. Angalieni interview yake na sporah. Ndio maana Nuh haishi kuchepuka. Kachoka kubemendwa. Halafu Shilole achaga kusema ulibakwa na baba mtoto wako wa kwanza. Alikuwa mumeo. Acha uongo mamaa. Maziwa yako yamechakaaaa kwa mitulinga.

    ReplyDelete

Top Post Ad