Mpasuko Mkubwa CCM: Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa Wapinga Jina la Edwarad Lowassa Kukatwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Habari za Hivi punde kutoka makao makuu ya CCM mkoani Dodoma  ni kwamba wajumbe wa kamati kuu  watatu ambao ni  Dkt. Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa  wamepinga maamuzi ya kamati ya kumkata mmoja wa wagombea maarufu   na kumweka mgombea asiyekuwa maarufu.

Akizungumza usiku huu majira ya saa saba za usiku Dkt. Nchimbi amesema kwamba wao watatu hawajakubaliana na maamuzi ya kamati kuu iliyoketi usiku huu chini ya Mwenyekiti Dkt Jakaya Kikwete kumkata mgombea maarufu kwa manufaa ya mgombea asiye maarufu.

“Katika kikao cha leo kamati haikupoea majina yote yaliyojadiliwa na maadili, suala ambalo ni kinyume na kanuni, pili katiba ya CCM inataka mtu anayekubalika  ndiye apewe nafasi ya kwanza, lakini kikao cha leo kimeonyesha kuminya wanaokubalika  kwa manufaa ya wachache wasiokubalika” Amesema Dkt. Nchimbi.

Hivyo basi kwa sababu hiyo wao watatu ambao ni wajumbe wa kamati kuu wamewataarifu wenzao  kwamba wamejitenga na maamuzi ya kikao hicho na kutangaza kuto kuyaunga mkono.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisiasa nchini Tanzania zinaonesha kuwa mgombea anayekubalisa sana CCM ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa  Bernad Membe.

Hapo  chini  nimekuwekea  Video  ya  Emmanuel  Nchimbi  akiyapinga  maamuzi  hayo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad