Mtikila Amerusha Kombora Kwa Mgombea Urais Edward Lowasa..Nimekuwekea Hapa Hilo Kombora

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KATIKA UCHAGUZI MKUU HUU TUSIRUHUSU MAFISADI WALICHEZEE TAIFA

Edward Lowasa ni balaa kwa Taifa!

Democratic Party (DP) inatarajia kufikisha Mahakamani chama cha
CCM pamoja na wanachama wake sita, Edward Lowasa na wengine,
kwa mujibu wa Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, kwa kosa

kubwa sana la kuvunja Katiba na Sheria za Nchi kwa kuanza kampeni
ya Uchaguzi kabla ya wakati unaopasa kwa mujibu wa Sheria.



1 Tunao ushahidi mzito unaothibitisha kwamba Edward Lowasa na
wenzake walianza kampeni ya urais ndani ya chama chao kabla ya
wakati, na kwamba chama chao kiliwapa adhabu ya kutofanya siasa

kwa miezi 12. Lakini safari hii Lowasa ameanza kampeni ya urais
Arusha kwa mkutano mkubwa sana wa hadhara wa kampeni haramu
na kumwaga rushwa ya kutisha!



2 Kama ni wadhamini alipaswa kuwapata katika ofisi za chama chake,
katika mikoa nane (8) tu Tanganyika na mikoa miwili tu Unguja na
Pemba, wadhamini 45 tu katika kila mkoa. Lakini Edward Lowasa
amefanya mikutano nchi nzima, ya kuwaahidi maelfu ya wananchi
katika kila mkutano wa hadhara, mambo atakayofanya kama wakimpa
kura zao awe Rais! Hii ndiyo kampeni halisi, ambayo ni ukiukaji wa
Katiba na Sheria za Nchi! Uchaguzi Mkuu unaendeshwa na Sheria, hivyo
ni lazima Sheria ichukue mkondo wake dhidi yake kwa kuivunja.

3 Edward Lowasa amevunja Katiba ya Nchi na Sheria ya kiwango cha
fedha kinachoruhusiwa kutumika katika shughuli halali za Uchaguzi,
kiasi kwamba CCM na Taasisi zote za uchunguzi wa kifedha nchini,
upelelezi wa Jinai na Usalama wa Taifa ni mlazima wanayo kazi muhimu
sana ya kupata ukweli kuhusu haya mabilioni ya fedha yanayomwagwa
nchini na fisadi Edward Lowasa, ameyapata wapi na kwa namna gani,
kumehusika ‘’Money laundering’ au la, kama mapato ya mapesa hayo
yote ni halali, na kama mapato hayo yote yalilipiwa kodi inayopasa kwa
ajili ya Taifa.
Ni marufuku kabisa tena ni makufuru Edward Lowasa kuruhusiwa
kugombea urais, kwa sababu amevunja Katiba ya Nchi na Sheria na
Kanuni za Uchaguzi. Sifa mojawapo ya kustahili kugombea uongozi wa
nchi yoyote ni maadili mema na uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na
taratibu za Utawala wa Sheria

4 Edward Lowasa, kwa kujimilikisha maeneo nchi nzima kwa kutumia
kifisadi Uwaziri wake wa Ardhi, ameliweka Taifa katika hatari kubwa ya
mmwagiko wa damu baina ya wakulima na wafugaji, baada ya kueneza
nchi nzima makundi ya ng’ombe wake, na kusababisha mapigano
makali ya mara kwa mara kila mahali nchini kati ya wafugaji wake na
wakulima. Kwa sababu ya uovu huu hata katika kampeni yake haramu
Lowasa ameshindwa kusema lolote juu ya kilimo, ingawa ndio uti wa
mgongo wa uchumi wa nchi yetu na ndiyo shughuli inayotunza uhai wa
asilimia 95 ya wananchi!
Kwa kuwaingilia wakulima katika ardhi yao, kuwaua ovyo, kuwaonea
kiasi cha kufisha matumaini yao katika kilimo, kumeifanya kauli mbiu
ya “Kilimo kwanza” kuwa porojo tu ya kisanii!

5 Edward Lowasa ni mwiko kabisa kupewa kugombea urais, kwa
sababu siyo tu aliutumia kifisadi Uwaziri wa Ardhi akajitajirisha na
kujipatia maeneo makubwa ya ardhi nchini kote, bali alitumia kifisadi
zaidi uwaziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, katika uagizaji wa
mashangingi ya Wabunge, mawaziri, wakuu wa Mikoa na Wilaya.

6 Edward Lowasa alikemewa mnamo mwaka 1995 na Mwalimu Nyerere
anayeenziwa na CCM lama “Baba” yao, alipotaka kugombea urais, kwa
sababu alikuwa fisadi papa, wala hakuweza kujitetea kwavile utapeli
wote aliojitajirishia ulikuwa mezani. Leo baada ya mabiashara haramu
mengi na kulipora sana Taifa kukiwa ni pamoja na utapeli wa “kununua
mvua Thailand” na kuliibia Taifa mabilioni ya fedha kwa kutumia
kampuni hewa ya RICHMOND, huyu ni fisadi-nyangumi. Ni mlemavu
wa rushwa tu wa kununuliwa na mapesa machafu anayomwaga Lowasa,
anayeweza kumruhusu fisadi Edweard Lowasa agombee urais.
Sifa za mtu wa kukugombea Urais zimeelezwa bayana na Mwenyezi
Mungu katika Kumbukumbu la Torati 17:15-20, ambazo Edward
Lowasa hana hata mojawapo! Lowasa awali alikemewa na Mwalimu
Nyerere ambaye CCM wanamuenzi kama “Baba” yao, kuwa hafai kabisa
kuwania urais, kwa sababu alikuwa fisadi papa, kama alivyomtangaza
hata Reginald Mengi pale alipolazimika kujiuzulu Uwaziri Mkuu kwa ajili
ya wizi kwa kampuni hewa ya Richmond, lakini leo akiwa fisadi la
kutisha zaidi kuliko papa eti anataka urais!
Si ajabu kwamba magabacholi yalioipora vibaya sana Nchi hii kama Sigh
Setti na hata Nazir Karamagi wote wamo katika genge la Edward
Lowasa! Si ajabu hata fisadi Reginald Mengi leo kuungana na fisadi
Lowasa yakizingatiwa machafu yake yeye mwenyewe, na kuhusika kwa
Mengi na mauaji ya Chacha Wangwe, pamoja na mpango wa Chadema
wa kumwua Mchungaji Mtikila, waraka feki wa kujaribu kuupotosha
ukweli ukatangazwa kwa ITV yake.
Katika uwaziri wake katika ofisi ya Waziri Mkuu, na katika Uwaziri wake
wa Ardhi na Uwaziri Mkuu, Lowasa alifanya ufisadi ambao katika nchi
kama China zenye uchungu na maslahi ya mataifa yao angekuwa wa
kupigwa risasi hadharani, lakini katika nchi yetu anatafuta urais!

7. Edward Lowasa AFYA yake imempiga marufuku kugombea Urais!
Kwa ajili ya kila ajira duniasni kote, moja ya mashart makuu ni lazima
mwombaji awe na afya iliyo bora, ndiyo sababu ni lazima ajira ya kila
mwombaji itegemee taarifa ya kitaalamu ya madaktari, inayothibitisha
kwamba hana dosari kiafya. Sharti hili ni la lazima kwa sababu:
a. Majukumu yote atakayopewa mwajiriwa atayatekeleza kikamilifu
kwa kutumia viungo vya mwili wake, kwahiyo viungo vyake vyote
ni lazima viwe katika hali iliyo imara kwa ajili ya kazi.
b. Hata kama kwa uthibitisho wa kitaalamu wa madaktari mwajiriwa
anazo akili nzuri kichwani mwake, akiwa na hitilafu katika viungo
vingine vya mwili wake huathiri afya ya akili zake na uwezo wa
utendaji wa akili zake.
c. Kazi ya Rais ni ngumu sana, kwa sababu ni pamoja na kusimamia
shughuli zote za maendeleo ya nchi nzima, na matatizo yote
yanayowatokea wananchi wote kila walipo, na kusimamia
utekelezaji wa majukumu yote ya watendaji wote katika Taifa,
hivyo kwamba maamuzi sahihi yanatokana na afya bora yenye
kuhakikisha uwezo unaopasa wa kiakili wakati wote
d. Hitilafu katika afya hudhoofisha uwezo wa kifikira na kusababisha
maamuzi mabovu, ambayo huleta athari mbaya sana kwa Taifa. Na
udhaifu huo huathiri mpaka maadili na hata uzalendo wa huyo
kiongozi mdhaifu. Kwa mfano akipatikana Rais anayeishi kwa
matumaini, kwa hofu ya kupoteza uhai kabla hajaweka sawa
mambo yake na ya familia na jamii yake atatumikia maslahi yake
zaidi kuliko Taifa, tatizo hilo la afya likawa limelikosesha Taifa
kipaumbele, na kuliangamiza kimaendeleo!
e. Wanaowania kugombea urais ni lazima wachunguzwe kwa makini
sana afya zao, kwa sababu kukifanyika makosa akatawazwa
mwenye hitilafu za kiafya, atakwenda kuwa mzigo mzito sana kwa
Taifa, hususan ugharamiaji wa utunzaji wa uhai wake ndani na nje
ya nchi, kukosekana na umakini anaopasa kuwa nao kwa ajili ya
dhamana kubwa aliyopewa n.k.
Kutokana na AFYA yake kuwa dhaifu sana hata kwa kumwona kwa
macho tu, kabla ya uchunguzi wa kitaalamu ni kwamba Edward Lowasa
hawezi kabisa kugombea Urais. Kwani amekosa sifa muhimu sana ya
afya bora, ambayo ni ya lazima kwa mtu yeyote anayestahili kupewa
dhamana kubwa sana ya kuliongoza Taifa. Pengine hata kugombea urais
kwenyewe anatafuta kutokana na hitilafu ya kiafya, iliyosababisha
udhaifu katika kufanya maamuzi, hivyo amejikuta kwa bahati mbaya
anagombea asichokiweza kabisa.
Ni lazima wagombea wote wa Urais, wa Ubunge na hata wa Udiwani
wachunguzwe kwa makini afya zao kabla ya kupewa kugombea, na hata
kuchunguzwa tena katikati ya muhula wa utumishi wao, kama kweli
tunalithamini na kuliheshimu Taifa.
Sifa za urais ni wito au uhanga kwa ajili ya Nchi ambao ni zaidi ya
maadili ya kizalendo, maono, vipawa na AFYA BORA. Ni dhana potofu
sana kwamba sifa ya urais ni kushabikiwa na umati wa watu! Kwa
sababu wengi hufuata mapesa na husombwa hata na magari ili umati
wa kishabiki tu upatikane. Lakini kumpenda mtu huwa lazima kuwe na
sababu, wakati ushabiki ni pepo mchafu au ‘psychological deficiency’.

LOWASA NI MOJAWAPO WA WAGONJWA WA MAGONJWA SUGU WA;IOKUWA WANATIBIWA NA BABU WA LOLIONDO NA TANGIA PALE HAJAPONA NA ZAIDI SANA ANA ANZA KUTETEMEKA

Source :Mtikila Mwenyewe :0766 053081
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lowassa ana Parkson deases, haitibiki, bali inatulia tu kwa dawa, na ugonjwa kadli miaka inavyoenda nao ndio hivyo unazidi kuwa ovyo kabisa, uwezo wa kufikiri, maamuzi, kila kitu ni ovyo kinakuwa,sababu unashambulia ubongo huo ugonjwa, haya, hao waliokazana Lowassa, Lowassa, nchi iko pabaya, tuwe na maamuzi bora. Lowassa awezi okoa nchi ndio tutaendelea kuyumbishwa na mawimbi tu

    ReplyDelete
  2. hii kali!!!!!!!!!!!!!!
    mtikila una vibomu pasta

    ReplyDelete
  3. WAAMBIE HAO WATANZANIA WAAODANGANYWA NA PESA HIZO ANAZOMWAGA NA KUJIFANYA KUJIINGIZA KWENYE MISIKTI YA KIISLAAM, ETI WAMPE KURA ! WATANZANIA KAMA HATULIONI HILO DAMU IKO NJE NJE KUMWAGIKA KWA AJILI YA MTU HUYU. HILI JITU NI FISADI, NA KILA MTU ANAJUA HATA BABA WA TAIFA ALIKWISHA MKEMEA KWA MAMBO YA RUSHWA BADO TU TUMEFUMBA MACHO, HAYA TUTAKIONA CHA MTEMA KUNI

    ReplyDelete
  4. baba mkorofi huyu, ha ha haaa eti lowasa ni mlemavu wa rushwa

    ReplyDelete

Top Post Ad