Shinikizo la Lowassa Kuhamia CHADEMA Lazidi Kupamba Moto......Mkewe Ampigia Magoti Akimsihi Asihame!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shinikizo dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, la kumtaka akihame Chama Cha Mapinduzi (CCM) linazidi kuongezeka na katika timu yake ya ndani ni watu wawili tu wanaonekana kumtaka abakie ndani ya chama hicho.

Habari za ndani ya vikao vya kujadili hatua za kuchukuliwa na Lowassa baada ya jina lake kukatwa kwenye mchakato wa kugombea urais kupitia CCM, zinasema kuwa wandani wake wanaamini kuwa hana atakachopata kama ataendelea kubaki kwenye chama hicho tawala.

"Kaka sikiliza, inavyoelekea shinikizo dhidi ya Lowassa ni kubwa sana. Watu wake wa ndani wanataka aondoke CCM. Wanaona kama amedhalilishwa mno,"kilisema chanzo chetu ndani ya vikao hivyo.

Chanzo hicho kilichoomba kutokutajwa jina kwa sasa, kilisema kuwa watu wake wa ndani wanaamini Lowassa akiendelea kubaki CCM atakuwa amewavunja moyo wale wote waliompigania, hasa vijana waliojaa matumaini ya kumuona akiongoza taifa hili.

Wandani wa Lowassa wanaamini kuwa kama akiamua kujiunga na chama chenye nguvu cha upinzani anaweza kutimiza ndoto yake ya kuwatumikia Watanzania kama rais wa awamu ya tano.

Chanzo chetu kinasema kuwa Lowassa mwenyewe amekwisha kuamua kufanya uamuzi mgumu, ila kuna msuguano juu ya namna ya kuondoka CCM.

Taarifa zaidi zinasema kuwa watu wawili katika timu ya ndani ya Lowassa ndio wanaelekea kuwa na mawazo tofauti. Hawa ni Rostam Aziz, mwanasiasa na mfanyabiashara mashuhuri nchini na mtu mwingine anayetofautiana na mkakati huu mpya wa kung'oka CCM ni mkewe, Mama Regina Lowassa.

Chanzo chetu kinasema kuwa wawili hao wanaamini mapigo ambayo Lowassa amekumbana nayo ni mengi na yanatosha, kwa maana hiyo ingefaa tu apumzike.

"Sijui ni kwa nini RA (Rostam Aziz) anakuwa skeptical (shaka). Si unakumbuka ndiye aliyesema amechoshwa na siasa uchwara... sasa sijui kwa nini anapunguza makali,"chanzo kilisema.

Hata hivyo, vyanzo vyetu vinaongeza kuwa pamoja na upinzani huo Lowassa anadaiwa kuwa amekwisha kuamua na kinachosubiriwa sasa ni muda tu wa kutamka anakokwenda.

Wakati hali ikiwa hivyo ndani ya kambi ya Lowassa, kuna taarifa za kuaminika kuwa kumekuwa na mashauriano baina ya watu wake na viongozi waandamizi wa kambi ya upinzani juu ya mwelekeo wake wa kisiasa.

Mwandani mwingine katika kambi ya Lowassa alisema kimsingi yeye (Lowassa) amekwisha kuamua, anachofanya ni kuona kwamba watu wake wa karibu hawadhuriki na uamuzi wake huo.

Chanzo hicho kilisema kuwa wenye msimamo mkali katika kambi ya Lowassa wanaamini utabiri wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani utatoka ndani ya CCM utatimia mwaka huu.

"Mnakumbuka ya Mrema (Augustino) alipoondoka CCM siasa za Tanzania zilibadilika mpaka leo? Sasa safari hii ni zaidi," alisema.

Takriban wiki mbili sasa, Lowassa amekuwa na jambo kubwa moyoni analitaka kuwaambia Watanzania.

Mara ya kwanza alikuwa afanye mkutano na waandishi wa habari Julai 13 mwaka huu mjini Dodoma majira ya asubuhi, lakini mkutano huo ukahamishiwa Dar es Salaam ambako pia ukaahirishwa kwa muda usiojulikana.

 

Tangu wakati huo kumekuwa na tetesi kuwa alikuwa atangaze kujiondoa CCM.

Lowassa ni miongoni mwa makada 38 waliojitosa kuwania kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi ya urais wa CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu. 

 

Hata hivyo, jina lake halikuwamo katika orodha ya makada watano waliopitishwa kwenye vikao vya juu vya chama hicho ambavyo mwishowe vilimteua John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais atakayekabiliana na wagombea wa upinzani katika uchaguzi mkuu huo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad