Siwema Hajamjulia Hali Mwanae Kwa Miezi 4 Sasa – Nay wa Mitego

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nay wa Mitego amedai kuwa ni miezi minne sasa mzazi mwenzie Siwema hajamjulia hali mtoto wao, Curtis.

Nay ameiambia E-News ya EATV kuwa Siwema alimpigia simu kumjulia hali mwanae alipokuwa na miezi mitatu. Curtis ana miezi saba sasa.

“Kwa upande wangu mimi na mzazi mwenzangu unajua hatujawekeana masharti yeyote lakini inabidi niwe muwazi, Siwema hajawahi hata siku moja kumjulia hali mtoto, kama walikuwa hajui hilo,” alisema.

“Unajua mimi tayari muonekano wangu naonekana mkorofi hata kama sio mkorofi kwahiyo mtu akiongea mimi namwacha maana najua mimi moyoni mwangu nikoje na yeye akiongea anajua kabisa moyo wangu ukoje. Sijawahi kupata simu yake hata siku moja tokea mtoto ana miezi mitatu hadi sasa hivi ana miezi saba hata kupiga simu kwa mama yangu au wadogo zangu ambao anawajua kumjulia hali mtoto! Kwahiyo mimi ndio kila kitu kwa mtoto wangu Curtis hata akija baadayee nitamuona ni mnafiki tu,” aliongeza.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kwahiyo unatuambia sisi ili iweje, tuje tumuone mwanao???

    ReplyDelete
  2. siulitaka kumlea mtoto pekeake na ukamtoa kwa baby mama? sasa unabwabwaja nini?

    ReplyDelete

Top Post Ad