Christopher Mtikila, Chipaka na Malisa Waenguliwa Mbio za Urais.......NEC Yasema Hawajatimiza Masharti. Lowassa,Magufuli WAPETA!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wanasiasa wakongwe nchini, Christopher Mtikila na John Lifa- Chipaka wametupwa nje ya kinyang’anyiro cha kugombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kushindwa kutimiza vigezo vya kisheria.

Mchungaji Mtikila anawakilisha Chama cha Democratic Party (DP) na Chipaka anawakilisha Tanzania Democratic Alliance (TADEA). Vyama vyote hivyo vilianzishwa mara tu Sheria ya Usajili wa Vyama vya Siasa, Na. 11 ya 1992, ilipopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Kupitia sheria hiyo, ndiyo ilitolewa ruhusa ya kisheria ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzania. Kabla ya sheria hiyo, masuala ya siasa yalikuwa si katika mambo ya Muungano.

Pigo la kukosa kuteuliwa kugombea urais, pia lilimpata Dk. Godfrey Malisa Kahangwa aliyewakilisha Chama cha Kijamii (CCK), chama kilichoanzishwa miaka michache iliyopita, baada ya uchaguzi mkuu wa 2010.

Akitangaza matokeo ya maombi ya vyama hivyo vitatu jioni hii, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva alisema ombi la Mchungaji Mtikila limekataliwa kwa sababu ameshindwa kuwasilisha tamko la kiapo la Mahakama Kuu, ingawa yeye aliapa lakini mgombea mwenza wake ambaye hakutajwa jina, hakufika na hakuna kiapo chake.

Jaji Lubuva ambaye alifikia ngazi ya jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, amesema Dk. Kahangwa hakutimiza idadi ya watu wanaotakiwa katika udhamini na amekosa mgombea mwenza kutoka upande wa Zanzibar.

Kwa Lifa-Chipaka, ilielezwa kwamba hakutimiza vigezo kwa vile alishindwa kuwasilisha orodha ya wadhamini kutoka Zanzibar. kisheria walitakiwa watu 200 wenye kadi za kupigia kura.

Wakati Chipaka amekosa wadhamini Zanzibar, upande huohuo chama hicho kimesimamisha mgombea urais, ambaye ni Juma Ali Khatibu, Naibu Katibu Mkuu.

Mchungaji Mtikila alilalamika mara tu alipotangaziwa uamuzi na Jaji Lubuva, kwamba alicheleweshwa kwa utaratibu tu wa ofisi ya Tume kwani alifika mapema na kuripoti ofisini kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Kwemboy.

Mtikila alidai kuwa hakufika na mgombea mwenza wake kwa wakati kwa kuwa amepata tatizo la kuumiwa mkewe na kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi na kuamua kuahirisha safari.

“Tulijitahidi hata kumtumia tiketi ya ndege lakini hakuwahi hapa. Hili tatizo ni la asili ambalo mtu analifahamu linaweza kutokea wakati wowote. Lakini mimi nimewahi hapa na jaji alinikubalia kuapa na kushauri nije kukujulisha kuwa mkinipa muda kusubiri kidogo nitakamilisha na kurudia kwake niape na mgombea mwenza akiwa amewasili,” alisema Mtikila katika kilio ambacho hakikuzingatiwa na Tume.

Jaji Lubuva alisema kwa wote walioshindwa kutimiza masharti, maana yake wamekosa kuteuliwa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa kwa utaratibu ulioandaliwa, hakuna muda wa kuwasubiri kukamilisha taratibu.

Vyama vilivyofuzu kuteuliwa wagombea wao ni pamoja na Chadema, Edward Lowassa (mgombea mwenza Juma Duni Haji) wanaowakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA); ACT-Wazalendo Anna Mghwira na mgombea mwenza Hamad Mussa Yussuf na Dk. John Magufuli (na mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan) wa CCM.

Kampeni za urais zinaanza rasmi kesho.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hiyo kawaida ndivyo walivyo hao.

    ReplyDelete
  2. WEWE MTIKILA SIKU HIZI NI MSEMAJI WA CCM SAMBAMBA NA NAPE SI MPINZANI WA KWELI TENA SASA KACHUKUE KOFIA NA SARE ZA CCM UUNGANE NAO JUKWAANI ILI WAKULIPE FADHILA KWA KUKUPA KIBALI CHA KUVUNA MSITU WA SERIKALI SAO HILL.TUNAJUA UNAUZA VIBALI HIVYO KUGANGA NJAA.MTIKILA SEMA NAAM;CCM OYEE SEMA OOOYE.UTAONDOKA NAO OCTOBA 25,2015

    ReplyDelete
  3. mtikila kaunge ccm wawe na nguvu...biashara ya kuponda upinzani tumekuxhoka wakat maendeleo kwa sasa tumeyapata kutokana na nguv ya umma ya chadema

    ReplyDelete

Top Post Ad