Mafuriko ya Magufuli Kuishika Dar Leo Wakati Akizindua Kampeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


John Pombe Magufuli
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinatarajiwa kuzindua kampeni zake za urais, ubunge na udiwani nchi nzima katika viwanja vya Jangwani leo, katika mkutano utakaorushwa moja kwa moja na televisheni na redio mbalimbali nchi nzima.

Katika uzinduzi huo, CCM pia inatarajiwa kuweka ilani yake ya uchaguzi hadharani, itakayonadiwa na mgombea urais wake, Dk John Magufuli na wagombea wengine wa ubunge na udiwani nchi nzima.

 Moja ya mambo ambayo CCM inatarajiwa kufafanua ni matumaini makubwa ya uwezo wa mgombea wake katika kusimamia utekelezaji wa ilani hiyo, kutokana na historia yake ya utendaji ndani ya Serikali katika nafasi mbalimbali alizokabidhiwa, ikiwemo Waziri wa Ujenzi.

Wageni mbalimbali pia wamealikwa kuhudhuria uzinduzi huo vikiwemo pia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa CCM Mkoa, Juma Simba alisema vile vile wanatarajia wageni kutoka ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam kuhudhuria mkutano huo leo.

“Tumetuma mialiko ya mkutano wa kesho (leo) sio tu kwa wana CCM wenzetu bali pia kwa vyama vingine vya siasa ikiwa ni pamoja na kwa vyama vya ‘Ukawa’,” alisema.

Simba alisema mkutano huo utakuwa mkubwa na wa aina yake ambapo viongozi mbalimbali wa chama wanatarajiwa kushiriki na kwamba mkutano huo ratiba yake itaanza asubuhi saa tatu kwa burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na wananchi kuendelea kuwasili uwanjani.

Sifa za Magufuli Mgombea huyo amekuwa akitajwa kuwa na sifa ya mchapakazi, makini, asiyependa uvivu, ambapo Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alimpachika jina “Tingatinga”.

Rais Kikwete alimpachika Magufuli jina hilo, baada ya kutangazwa kuwashinda makada wengine wawili waliokuwa wakiwania kuteuliwa kuwania urais kupitia chama hicho katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika Dodoma.

 “Kila mtu anaitwa jembe lakini huyu ni zaidi ya jembe. Ni tingatinga… Magufuli ni bulldozer. Magufuli havumilii ujinga, ni mtu ambaye anataka kuona kazi zake zinafanyika kama alivyoagiza,” alikaririwa akisema.

Kikwete aliendelea kummwagia sifa Dk Magufuli kuhusu utendaji wake akisema kuwa alipokuwa akifuatilia makandarasi kwenye miradi ya ujenzi, alidiriki kuwatimua pale alipobaini walikuwa wakifanya kazi kinyume na makubaliano.

Baadhi ya watu waliofanya naye kazi wamekaririwa wakisema iwapo atachaguliwa kuwa rais basi wavivu wajitayarishe kukimbia kwani Waziri huyo ni mchapa kazi wa hali ya juu.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba

    ReplyDelete
  2. wateleta wasanii tuu...ndio maana hii nchi inaitwa BONGO! USANII MTUPU. MARAIS WATATU na MAWAZIRI WAKUU WAWILI (Salim na Warioba) wanakaa kumnadi mgombea mmoja! Huo sio USANII? Viongozi wa serikali - wakuu wa mikoa - Sadiq, unadhubutu kuacha kazi zako za serikali, unaenda kwenye chama kama MWANACHAMA! Na wewe ni mmoja tunaekutegemea UWE referee kwenye haya mashindano ya UCHAGUZI kwa hapa DAR ES SALAAM? Kwa kweli hiki chama isipoondoka madarakani mwaka huu, basi huenda watanzania watakuwa wamelogwa na ccm!!

    ReplyDelete

Top Post Ad