Magufuli Akataa Kumia Helikopta.......Asema Atatumia Gari ili Azijue Kero za Wananchi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MGOMBEA urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema katika sehemu kubwa ya kampeni yake, atatumia zaidi usafiri wa barabara ili apate fursa ya kuzijua kwa karibu kero za wananchi katika maeneo mengi ya nchi.

Hata hivyo, alifafanua kuwa kwa maeneo mengine yenye ulazima wa kutumia usafiri mbadala, anaweza kufanya hivyo, lakini dhamira yake ni kutumia zaidi barabara. Aidha, amezitaja sifa ya waziri ajaye wa ujenzi, ambaye atarithi wizara aliyoitumikia kwa miaka 15, iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza katika mkutano wake wa kwanza tangu kuzinduliwa kwa kampeni za chama hicho katika Kijiji cha Mishamo, kilichopo Kilometa 150 kutoka mkoani Katavi, Dk Magufuli alisema amekataa kutumia helikopta katika baadhi ya sehemu atakazofanya ziara, ili kujionea mwenyewe kero ya barabara inayowakabili Watanzania.

Moja ya barabara alizoahidi kujenga ni pamoja na kutoka Tabora mpaka Mpanda, ambayo ina kilometa zaidi ya 356 na ya Mpanda mpaka Uvinza yenye urefu wa karibu kilometa 190.

Kwa mujibu wa Magufuli ambaye amejipatia sifa ya uchapakazi katika wizara hiyo, kazi ya kwanza atakayofanya atakapochaguliwa kuwa rais, ni kuteua Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa Katiba.

Amesema kutokana na kazi kubwa ya ujenzi wa barabara iliyopo mbele yake, Waziri ajaye wa Ujenzi ni lazima awe na uwezo wa kuchapa kazi kuliko yeye, na kuongeza kuwa atamsimamia yeye mwenyewe kuhakikisha anatekeleza majukumu hayo.

Akizungumza kijijini Mishamo, Magufuli pia aliwahakikishia wananchi wa maeneo hayo, ambao baadhi yao waliokuwa wakimbizi waliotoka Burundi wakati wa machafuko ya mauaji ya kimbari, lakini wakapewa uraia wa Tanzania, kwamba uongozi wake utaheshimu na utawatambua kuwa wao ni Watanzania.

Huku akizungumza lugha mbalimbali ikiwemo Kiha, Kifipa na Kirundi, Magufuli pia aliahidi kujenga shule katika kata ambazo zimegawanywa na kujikuta zikitegemea shule moja ya sekondari, kutatua kero ya maji na umeme.

Magufuli alisema waziri atakayemteua wa umeme, akishindwa kupeleka umeme Mpanda, atoke mwenyewe huku akisema atakuwa rais wa wanaChadema, wana ACT, wana CUF na wasio na chama kwa kuwa maendeleo hayana chama.

Kuhusu reli, alisema atajenga reli ya kisasa na uwezo wa kufanya hivyo anao, ikiwemo katika kuzuia mafisadi wasitumie fedha za umma kwa kuunda Mahakama ya Maalumu ya Kushughulikia Rushwa.

Takwimu za mtandao wa barabara wakati Tanganyika, sasa Tanzania Bara ikipata Uhuru mwaka 1961, uongozi wa mkoloni uliokaa tangu miaka ya 1884 na 1885 mpaka 1961, uliacha mtandao wa barabara za lami wenye urefu wa kilometa kilometa 1,360.

Lakini katika uongozi wa miaka 10 tu ya Serikali ya Awamu ya Nne, mtandao wa barabara za lami uliojengwa na kukamilika una urefu wa kilometa 5,568 katika barabara kuu na kilometa 535, kwa upande wa barabara za mijini.

Mbali na kumalizika kwa miradi hiyo ya barabara ambayo sehemu kubwa ilisimamiwa na Dk Magufuli, kilometa zingine 3,873 ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi, huku barabara zingine za umbali wa kilometa 4,965 zikiwa zimeshafanyiwa upembuzi yakinifu na kilometa nyingine 3,336 zikiendelea kufanyiwa upembuzi yakinifu.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amemsifu Magufuli kwa uchapakazi wake na kusema CCM baada ya kufanya mchakato wake, imempata Magufuli na katika hilo, hakikufanya makosa.

Alisema Magufuli ni mwanamume wa shoka na wengine wanamuita jembe na kuongeza kuwa kwa zaidi ya miaka 20 aliyomfahamu Magufuli, ana hakika akipata urais, kila mtu atafahamu ni jembe kutokana na uwezo wake.

Pinda, ni mmoja wa makada hodari wa CCM waliotia nia kuusaka urais wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho tawala, lakini hata baada ya kukwama kuteuliwa, ameendelea kuwa imara katika chama hicho.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndiyooooo,hata Mwl.Nyerere alifanya hivyohivyo,hata treni alipanda.
    KAZI TU MWANAWANE!

    ReplyDelete
  2. POLE YAKE HATA ATEMBEE KWA MKOKOTE ANAJICHOSHA BILA SABABU ZA MSINGI HAWEZI PATA NA HATA KUJA PATA,RAIS AMESHAPATIKANA SIKU NYINGI,BADO KUAPISWA TUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  3. HAKUNA TENA NAMNA NYINGINE HAPA NI KAZI TU!!! piga kazi magufuli kila laheri katika safari yako, wataelewa tu mwisho wa siku. sahizi hawatungi sera wanajadili CCM kupitiliza muda, na wao si waje wazidishe?!! MKAPA aliona mbali juzi sijui alijuaje!! bora ukose mali upate akili aisee

    ReplyDelete
  4. KAPI ANAMNADI MGOMBEA WA CCM

    ReplyDelete
  5. big up jembe letu

    ReplyDelete
  6. JAMAA HATA MVUTO HANA ANALAZIMISHA TUUUU

    ReplyDelete
  7. HATA ATEMBEE KWA MKOKOTE UNAOSUKUMWA NA PUNDA NCHI ZIMA, KAWE HAWEZI NA HATA PATA URAIS KWA SABABU RAIS AMESHAPATIKA SIKU KINACHOSUBILIAWA NI KUAPISWA TU

    ReplyDelete
  8. Wengine wanatumia ndege kama tupo marekani vile...

    ReplyDelete
  9. Hata atembee kwa miguu nchi yote ni kazi bure tu,,kama ndio eti nae anashaangaaa raslimali zinapotea kwenye mifuko ya wachache,badala umuulize,kikwete .,mkapa aka (domo chafu) na mzee wa ruksa eti anatuuliza sisi kwanini CCM imeshindwa kututoa ktk umaskini,kama nae sio msanii nini ? km kinana na nape kushambulia serikari yao as if wao ni ukawa. kweli ccm imeanza KUKATA lazima warusherushe miguu na mikono,Bye bye CCM rest in peace

    ReplyDelete
  10. Hâta ukikaa ofisini bila kutoka kero za watanzania zinajulikana. Acheni kutuhadaa. Labda mseme bajeti haitoshi. Timechoka kudanganywa. Yeye aende akanadi sera kwa byscikel ama ndege, tunachotaka ni tanzania yenye mafanikio.

    ReplyDelete
  11. Kashakilemisha agenda za watu huyu mnamuonaaa!! yaani jana EL kapanda daladala na kusikiliza kero za wananchi, na yeye eti atatembea kwa gari kujua kero za wananchi", mwe mwe mweeee!!! kweli ccm imeishiwa nyimbo!

    ReplyDelete
  12. Dmagufuli ana kipya na kuma step yote anayofanya lowassa. Kuona lowassa yuko kwenye daladala, nae huyo; kuona ukawa wanataka salam za asalaam alleikum, tumsifu Yesu kristo na yeye huyo, ninakuambia ana tamani awe ukawa

    ReplyDelete
  13. Ningekuwa PInda sidhani kama ningekuwa hapo! Boss amekuona wewe ni zezeta! Ulichukua formu, na hata hukutokeza TANO BORA. Maana anakuona hufai wewe ni moto wa mabua!!

    ReplyDelete
  14. Hahahahahaha magofuli panda ata gari la kupelekea maiti mochwari ccm ngoooooo hamtamiliki hii nchi na hats ikatokea mkashinda utakuwa ushindi Wa mwisho hautakaa utokee na hata kupita kwenu labda kafara za watu watakao jitoa kulikomboa taiga mikononi mwenu Lowe kubwa ndipo total give up ikiwa wote tutajitoa muhanga wachonga zengwe sahau kuwa raisi baba icho cheo ungekipata endapo usingekuwa kwenye chama cha majambazi

    ReplyDelete
  15. COMMENT ZENU ZIMEENDA SHULE,ASANTENI ,TENA MAGUFURI ANAPENDA KUIGA NDIO MAANA NASEMA HUYU NI UKAWA DAMU,JUZI MMESEMA SISI MALOFA NA NYINYI MALODI LEO TENA UNAWAGEUKA MWEZAKO KWANINI?,SHIDA ZETU ANAZIJUA LOWASA NA LEO YUPO TANDALE KUWATEMBELEA MALOFA NA NDIO TUTAKAO MCHAGUA WEWE LABDA KULA ZAKO NENDA MSOGA UTAZIPATA

    ReplyDelete
  16. Wadau mnanifurahisha tukutane jangwani jamani lazima tufunge mitaa siku hiyo,sisi hatuhongwi wala hatutaki wasaniii

    ReplyDelete
  17. HUYU NAE ANALETA MZAHA KWA MALOFA, KILA SIKU ALITUAMBIA KWAMBA ANAJUA MATIZO YA WATANZANIA,SASA ANATAKA KUJUA NINI ZAIDI? USANIII TUUU,MATATIZO YETU HATA MTOTO WA CHEKECHEA ANAYAJUA,NA CCM WANAYAJUA MIAKA NENDA RUDI,TATIZO NI KUTEKELEZA,SASA NIMEANZA KUPATA WASI WASI NA HUYU MGOMBEA WA CCM , NATAFAKARI UPYA PA KUWEKA KURA YANGU

    ReplyDelete
  18. Utajiju CCM mbele kwa mbele.Magufuli eyeeeeeee.CCM JUU JUU zaidi UKAWA mtaisoma namba.October 25

    ReplyDelete
  19. CCM NYUMA KWA NYUMA KAMA KANU...WAKAANZE UPYA! INATAKIWA CCM WAKAJIPANGE UPYA, NA WAANZE CHAMA CHA MAPINDUZI YA AINA NYINGINE. KAMA CCM NDIO CHAMA CHA MAPINDUZI...NI KWELI - SHULE ZOTE ALIZOJENGA NYERERE WAZIPINDUA; BARABARA ZOTE ALIZOACHA MKOLONI WAMEZIPINDUA; VIWANDA VYOTE WALIVYOACHIWA WAMEVINDUA; NA HATA BWAWA LA MTERA WAMELIPINDUA! CCM - chama cha MAJIZI! CHAMA CHA MAJIZI SI TU PESA YA NDANI, HATA PESA TUNAYOKOPESHWA WATANZANIA WOTE - WATU WA CCM WANAIIBA PESA HIYO PIA. JE HAYO NDIO MAPINDUZI? MUNGU MREHEMU CCM

    ReplyDelete
  20. ANGALIENI WATANZANIA WENZANGU HUYU MGOMBEA WA CCM MAGUFULI ANATAMKA`WAZI KUWA CHAMA CHAKE CCM KIMEMPATIA HELICOPTER AMEIKATAA ILA KWA MAENEO BAADHI.LEO HII KIKWETE AMEWAPIGA MARUFUKU UKAWA KUTUMIA HELICOPTER POPOTE PALE.EEEH MUNGU WANGU HAYA NI MAONEZI YA WAZI WAZI NI UKATILI NI USHENZI NI UFILAUNI NI WOGA NI UHUNI NI UCHOCHEZI WA KUTAFUTA UVUNJIFU WA AMANI NI UHALIFU

    ReplyDelete

Top Post Ad