Kwaheri Dr Slaa Huwaminiki Tena Mzee...Hatujui Kesho Tena Utasema Nini, Utakuwa Wapi na Nani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dr Slaa
 Sisi wote ni wanafunzi na wahanga wa Dr. Slaa kifikra na kisiasa. Dr. Slaa umetufundisha watanzania wote kuwa CCM haifai na ndio chanzo cha ufisadi, ubadhilifu, wizi, matumizi mabaya na sera mbaya zisizotekelezaka na zilizosababisha maisha ya watanzania kuwa mabaya. Ukiwa na wenzako wa chadema kwa kutumia kampeni za sangara, M4C, redio na tv, ulitufundisha kuikataa CCM na tulikuelewa vizuri, tuliamini na tukafanya hivyo kwa moyo, kwa nguvu na kwa akili zetu zote. Wewe ndiye uliyesababisha taifa lote liichukie na kuikataa CCM kwa moyo na nguvu zote, watu wameshalielewa somo lako kuhusu ubaya wa CCM kwetu. Ulitufungua akili tuliokuwa hatujui siasa za chama cha CCM. Tulifanya hivyo kwakuamini kwamba wewe ni msomi mzuri na mtumishi wa Mungu husemi uongo na utakuwa umefanya utafiti mzuri kuhusu uhusiano uliyopo kati ya maisha ya watanzania na sera, utekelezaji wa sera na utawala wa CCM. Uliamsha hamasa na ari ya watanzania katika siasa na kufikiri juu ya maisha yao. Sasa tumeelimika sana kupitia wewe na wenzako wa chadema kuhusu ubaya wa CCM kwetu na kwa taifa, watu hawataki tena kusikia habari za CCM mitaani na maofisini. Ahsante sana baba!

Sasa wafuasi wako tumeanza kushikwa na butwaa kubwa kukuona wewe tena unakipigia debe CCM kiendelee kubakia madarakani!!!!@***&.com???. Hapa kuna mawili, ama wewe unataka kutugeuza sisi kichwa chini miguu juu, au wewe ndo umegeuka mwenyewe kichwa chini miguu juu. Tunajiuliza nini kimetokea kwa mwalimu wetu Dr. Slaa hadi kufanya hivi? Kama shida ni Lowassa kuhamia chadema basi hata wewe hukupaswa kuwa na uhalali wa kukilaumu CCM kwa ufisadi, ubadhilifu na huduma mbovu kwa wananchi, badala yake ulipaswa kuwalaumu viongozi waliotokana na CCM tu peke yake wasiofanya vizuri na sio chama chote cha CCM kuwa hakifai. Vinginevyo wewe ulikuwa katibu mkuu wa chadema hivyo ungeweza kuhakikisha kuwa rais (Lowassa) anayetokana na chama cha chadema angeongoza nchi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na maadili ya chadema tu basi. Hivyo ukiwa kama katibu mkuu wa chadema hukuwa na sababu za msingi za kumuogopa Lowassa 'fisadi' kuhamia chadema au kugombea urais kupitia chadema maana chama chini ya katibu mkuu (wewe) kingemnyoosha na kumfanya kuongoza nchi kwa mujibu wa chadema. Kama hili limeshindikana kwako na kwa chadema kwanini ulitaka hili liwezekane kwa CCM? Ulikuwa unatudanganya kuhusu ubaya wa CCM? Ulipaswa kuwalaumu viongozi na watendaji wabaya wa CCM na sio chama cha CCM chote kama chama. Unapaswa kuwaomba samahani CCM hadharani kwa kukisema chama chao vibaya badala ya kumsema mwanachama/kiongozi wa CCM ambaye ni mwizi, mbadhilifu, fisadi, n.k, pili, uwaombe radhi watanzania kwa kuwapotosha kuhusu ubaya wa CCM kama chama.

Kama wewe ukishindwa kuyafanya haya yote mawili kwapamoja taifa hili litakuwa juu ya kichwa chako kwa kuliyumbisha na kutaka kulipasua vipande. CCM wanafunzi wako tunakuona kama mwalimu usiyekuwa na msimamo, uliyehongwa, mwenye ubinafsi wa kuwa rais kwa gharama yoyote, unayependa porojo, usiyependa maamuzi ya pamoja ndani ya chama, mpotoshaji, muongo, usiyejali wafuasi na familia yako, na usiyefaa kusikilizwa tena na watu wenye shida za maisha kama sisi. Hatujui kesho tena utasema nini, utakuwa wapi na nani. Kwaheri huwaminiki mzee!!!

By Kavulata-JF
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad