MAFISADI Wananiogopa Hawataki Niingie IKULU...Watanzania Maskini Wenzangu Wananikubali Sana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli, amesema mafisadi hawawezi kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kuwa wanamwogopa.

Dkt. Magufuli aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara,uliofanyika katika Viwanja vya Mvumi Misheni, Jimbo la Mtera,mkoani Dodoma.

"Mafisadi hawawezi kunichagua kwa sababu wananiogopa ila wapo Watanzania wengi wanaonipenda na kunikubali wakiwemo maskini wenzangu, wanyonge ambao watanipa kura nyingi ili niweze kuwatumikia na kutetea masilahi yao," alisema.

Alimpongeza mwanasiasa mkongwe, Mzee John Malecela kwa ujasiri wake wa kuendelea kubaki CCM licha ya kushindwa katika mbio za kuwania nafasi ya urais miaka iliyopita.

"Mzee Malecela aliwahi kugombea uteuzi wa nafasi ya urais, lakini hakufanikiwa na hakufikiria wala kuthubutu kuhama chama hata siku moja, bado yupo na amekuwa msaada mkubwa," alisema.

Alisema mbali ya kuukosa urais, pia aliangushwa kwenye nafasi ya ubunge wa Jimbo la Mtera na Livingstone Lusinde lakini hakuhama chama. Alisema anawashangaa waliohama CCM baada ya kukosa nafasi.

Aliwaomba Watanzania wamchague aweze kubadilisha maisha yao na kukuza uchumi akiwataka wasikubali kudanganywa na wapinzani ambao hawana sera wala uzoefu wa kuongoza Serikali.

Akizungumzia sera ya elimu bure, alisema hakuna sababu ya kukosa madawati wakati nchi ina rasilimali kubwa ya miti; hivyo alitoa wito kwa Wakurugenzi kukaa mkao wa kufanya kazi.

Livingstone Lusinde
Naye Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM na mgombea ubunge Jimbo la Mtera, Lusinde alisema CHADEMA kimepoteza mwelekeo baada ya kuwapokea wanasiasa waliowatuhumu kwa kashfa mbalimbali ndani na nje ya Bunge.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tukuogope kwa lipi
    Una nini cha mno wewe kinda CCM
    Unatumiwa na mafisadi CCM
    CCM unaijuwa wewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mafisadi limewachoma, mnaanza kujitetea....subirini baada ya 25/10 ndio utajua kama CCM ni kinda au BABA LAO

      Delete
  2. Kwa push up wakuogope

    ReplyDelete
  3. Wanakuogopa kwa uongo wako Kwani huendani na ilani ya CCM
    Iliyojaa ufisadi na kubebana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mafisadi papa yamehamia cdm, yanapigana kufa na kupona kujinasua kwa TINGATINGA, hilo limewaganda, mahakama ya mafisadi ikianzishwa tu, inaanza nao hao wewe mfano kwa wengine

      Delete
  4. Hatumuogopi huyo aliyekuja na jina lako kamati kuu sembuse wewe
    CCM unaijuwa wewe
    Hata ujumbe wa tawi hujawa
    Unajizijuwa itikadi za CCM wewe
    1 kulindana
    2 mbio za relay kupokezana
    3 chukuwa chako mapema
    4 watoto wangu na familliya nikistaafu kakuna mashitaka
    5tanzania ndo sisi Na ndo waamuzi WA viongozi wote nyeti
    6. Kelele za mpangaji hazitunyimi usingizi Watanzania wana tabia ya kusahau baada ya muda
    7 vitenge, kanga, fulana na burudani la kina Kiba , diamond, kopa Kila kwenye shughuli yetu bure serikali yetu inalipa utaona mafuriko ya Watu Watanzania wanapenda shughuli
    8 mapolisi wote wawe chini ya amri yetu
    9 kusafiri ulaya Kama Kazi nenda na rundo la washikaji Hakuna kuulizwa ilani yetu hiyo
    10 pita airport na dollar kibao peleka majuu shopping ya wife, vimada, na nk
    11 teuwa Watu walioshiriki wenye kampeni wape ulaji
    Ukuu a wilaya mkoa nk

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mafisadi naona mapovu yanawatoka kabla, MTAISOMA NAMBA

      Delete
  5. MZEE NAE ANACHEKESHA UTAMUWEZA MKUU WA KAYA?YAANI BOSI WAKE NA WALIMTANGULIA AWAFUNGE KWELI ?ANAONGEA ASICHO KIJUA,WATAMUANZA YEYE,PESA YA KAMPENI ANAPEWA NA HAO HAO ALAFU ANATAKA ALETA MCHEZO ALIOFANYA JK AWAZUNGUKE .

    ReplyDelete
  6. SISI WANYONGE NA MASKINI MBONA TUKO WENGI,TUTAKUPA KURA BABA.
    JIANDAE KUAPISHWA ILI UONGOZE NCHI,MAANA TUNAJUA HAUTATUANGUSHA.
    BWANA AWE NAWE.

    ReplyDelete
  7. MAGUFULI,MAGUFULI UNAMSIFI MZEE MALECELA KWA KUTOHAMA CCM JINA LAKE LILIPOKATWA NA NYERERE.HIVI UNAMJUA VIZURI HUYO MALECELA.MUULIZE LUSINDE AKWAMBIE ALIVYOPAMBANA NA VISA,VITISHO,UKOO,UJIMBO YAANI WE ACHA TUU.PILI HUYO MZEE ANA HISTORIA MBAYA MNO YA KUBADILI-BADILI WANAWAKE KAMA SOKSI.HAWAKUKUNONG'ONEZA WATU WA MVUMI? TATU NI YEYE ALIYESABABISHA MPAKA LEO SERIKALI ISIHAMIE DODOMA.ALIMSHAURI VIBAYA MZEE MWINYI WAKATI YEYE ALIKUA NDIYE MWENYEJI WAKE.MALECELA AKAKIHAMISHA HATA KIWANDA CHA SOSA PEPSI KWENDA MBEYA.MWISHO MFANO: ANGEHAMA CCM ILI AHAMIE WAPI WAKATI KILA MTU ANAMWELEWA NI ROTTEN CARROT?

    ReplyDelete
  8. ni kweli unapomtaja john samweli malecela dodoma sio mjini tuu bali mkoa mzim wanamhesabu kama mzee hasara kubwa aliyewahi kuonekana katika ulingo wa siasa na maendeleo ya ujumla ya mkoa wa dodoma.acha historia ya uongozi tangu uhuru kama mkuu wa mkoa,waziri jumuia ya afrika mashariki,wizara mbali mbali,tuzungumzie miaka nane[8] akiwa ni waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais[rais akiwa mzee ally hassan mwinyi].malecela alikua na nguvu kubwa kiuongozi na mzee mwinyi alimtegemea sana kama mshauri wake mkuu.badala yake huyu bwana kwa kuendekeza kinena akaweka na kuoa kwa vipindi wanawake katika kila mkoa kila kona ya nchi alikofanya ziara za kikazi .hakujali maendeleo ya nchi na wananchi,akaiua[PRACTICALLY] mamlaka ya ustawishaji makao makuu[cda]yeye na msekwa aliyekua mwenyekiti wa bodi.miaka yooote nane hakuna barabara dodoma iliyowekwa lami hata KILOMITA MOJA NARUDIA MOJA TUU! mtu gani huyu,kiongozi gani huyu unayemsifia wewe magufuli,kwa hali hiyo ni wazi sasa kwamba HATA WEWE JOHN POMBE MAGUFULI HAUTUFAI KUWA RAIS HATA CHEMBE,,CHOLOLO KAMA HUYO MALAYA MKUU UNAYEMSIFIA JOHN SAMWELI CHIGWIYEMISI MALECELA.

    ReplyDelete
  9. OGOPA,MWOGOPE MUNGU MAGUFULI UNATUAMBIA SISI WATANZANIA KUWA WEWE NI MASIKINI MWENZETU.EWE MWENYEZI MUNGU TUEPUSHE SISI WAJA WAKO NA HASIRA ZA MAJIBU KWA HUYU BWANA AMBAYE NI FEDHULI MUONGO,TENA MUONGO MKUBWA ANAYETUDHIHAKI NA MANENO YAKE YA UONGO WA KISHETANI.MAGUFULI NI MMOJA KATI YA MATAJIRI WAKUBWA AFRIKA MASHARIKI.TUKWAMBIE WANAYOYAJUA HAYO KWA UNDANI NI WATU WAWILI KWANZA MDHAMINI WAKE MKUU WA URAIS BENJAMIN MKAPA NA PILI ANAYEMTUNZIA KADI ZAKE ZA MABENKI YA NJE NA UMILIKI WA HISA ZA MAKAMPUNI IKIWEMO KENYA AIRWAYS SI MWINGINE BALI NI RAFIKI YAKE MKUBWA RAILA OGINGA ODINGA MWANASIASA MKONGWE WA NCHI JIRANI YA KENYA.UTAJIRI WA MAGUFULI UNAKISIWA KUWA DOLA MILLION 20[KWA UCHACHE] ACHA KUFURU MAGUFULI,MUOGOPE MUUMBA WAKO.MWEHU WEE.

    ReplyDelete

Top Post Ad