Masogange, Davido ndani ya "PENZI" zito..Wanaswa Club Wakinyweshana Pombe Kwa Raha zao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Davido
PENZI ni kikohozi, kulificha huwezi ! Habari ya mjini kwa sasa ni mahaba niue ya muuza nyago kwenye nyimbo za wanamuziki wa Bongo Fleva, Agness Gerald ‘Masogange ’ na staa wa muziki nchini Nigeria ‘Naija’ , David Adedeji Adeleke ‘Davido ’ baada ya kuoneshana penzi zito hadharani .

Habari kutoka kwa chanzo ambacho ni mtu wa karibu wa Masogange aliyeko Johannesburg nchini Afrika Kusini ‘Sauz ’ kimelieleza gazeti hili kwamba, wawili hao kwa sasa ni wapenzi wa kupika na kupakua .

Chanzo hicho kililimwagia gazeti hili ‘ubuyu ’ kwamba , katika tukio la hivi karibuni , Davido ambaye ni staa wa Ngoma za Skelewu na Aye alitokea nchini kwao, Nigeria na kwenda kukutana na mwanadada huyo nchini Afrika Kusini ambako wanaponda raha kwa sasa .

“Yaani Masogange na Davido ni mahaba niue, wanaponda raha kwa kwenda mbele maana hata juzi tu walikuwa kwenye klabu moja hivi wanakunywa na kula pamoja huku wakifurahia vilivyo uumbaji wa Mungu .

“Davido ametinga hapa Sauz akitokea Nigeria kwa ajili tu ya kuja kukutana na Masogange ambaye mara nyingi anakuwa Sauz, ” kilisema chanzo hicho.

WANASWA KLABU , WANYWESHANA POMBE
Chanzo hicho kilienda mbele zaidi na kutuma video ambayo inamuonesha Davido akimnywesha pombe Masogange huku wakiwa wamelewa tilalila bila kujali kwamba walikuwa klabu ambako kuna watu wengi.

“Angalieni hiyo video kwa ushahidi zaidi, Davido alikuwa akimnywesha pombe kali Masogange na kuna wakati Masogange naye alikuwa akimnywesha Davido .

“Nilikuwa nao klabu wakifanyiana vitendo vya kimahaba kama kunyweshana pombe kwenye chupa moja bila kujali macho ya watu ,” kilidadavua chanzo hicho na kuongeza:

“Nakwambia huku ( Sauz ) Masogange na Davido wanakula bata hadi kuku wanaona wivu . Yaani ni mapenzi mazito usiwapimie . ”

DIAMOND ATAJWA
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Davido ambaye ni rafiki wa karibu na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz ’ inadaiwa ndiye aliyemuunganishia jamaa huyo kwa Masogange kwani alikuwa akimsikia na kumuona kwa muda mrefu kwenye mitandao ya kijamii na akampenda .

“Si bure , kilichomvutia Davido ni ule mzigo wa Masogange ( makalio ) maana kila siku huwa anautundika kwenye Instagram ‘so ’ akaona mtu wa kumpigia pande ni Diamond , ” kilidai chanzo hicho.

MASOGANGE ATAFUTWA
Baada ya kuzipata habari hizo na ushahidi wa video, gazeti hili lilimtafuta Masogange ambapo jitihada hizo ziligonga mwamba kutokana na mwanadada huyo kutumiwa ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp bila kujibu.

Chanzo: GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad