Mbowe ashinda Rufaa dhidi ya Hukumu kesi ya Shambulio....Mahakama Yaamuru arejeshewe Milioni 1 aliyolipa kama faini.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi leo imeifuta hukumu iliyomtia hatiani Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na kuamuru arejeshewe Sh1 milioni alizolipa kama faini.

Hukumu hiyo ilitolewa leo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Aishiel Sumari baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Tamari Mndeme kukubali rufaa hiyo.

Mbali na sababu za rufaa zilizowasilishwa mahakamani na wakili wa Mbowe, Peter Kibatala, wakili Mndeme aliiongeza sababu zingine mbili zinaonyesha mapungufu ya hukumu hiyo.

Wakili Mndeme alimweleza Jaji kuwa shitaka lenyewe na maelezo ya shitaka vilikuwa vinatofautiana hivyo kuathiri uhalali wa shitaka na uhalali wa hukumu iliyomtia hatiani Mbowe.

Mbowe alitozwa faini ya Sh1 milioni au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kumshambulia mwangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu wa 2010 katika wilaya ya Hai, Nassir Yamin.

Hukumu hiyo iliyolalamikiwa na Mbowe kuwa haikumtendea haki kwani kesi hiyo ilifunguliwa kisiasa, ilitolewa Juni 17 mwaka huu na Hakimu Mkazi wa wilaya ya Hai wakati huo, Denis Mpelembwa.

Hata hivyo, Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), na mgombea ubunge wa Jimbo la Hai alilipa faini hiyo na kuachiwa huru na Mahakama ya wilaya ya Hai.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. After many years
    Oops
    Hii tanganya toto tuone mnafanya Kazi
    Ili mchakachuwe matokeo
    Mmeula na chuya
    Mapesa ya USA na Europe hayatoki ngo mkiiba kura CCM
    Na uzuri mwaka huu tuna Watu wetu Kila kona

    ReplyDelete
  2. VIVA KAMANDA MBOWE!

    ReplyDelete
  3. mungu ni mwema. !!!! hongera sana mbowe

    ReplyDelete
  4. Haki ya mtu haipotei sema binadamu wanaichelewesha. KAKA MBOWE MBELE KWA MBELE TUPO PAMOJA SANAAAA. Mwenyezi Mungu azidi kuwapigania na kuwapa kifua cha kuyabeba haya maneno ya uchochezi na kuchafuliwa yanayotolewa na maCCM ili MPOTEZO UELEKEO, HAWATAWEZA KWA JINA LA YESU, tuko nyuma yenu na sala zetu kwa Taifa letu tuweze kufika pale tunapopataka.

    ReplyDelete
  5. MBOWE HUNA AKILI UMESHINDWA FANYA KAZI YA KUUZA MITUMBA BARABARANI

    ReplyDelete
  6. MBOWE UMEUZA CHAMA KWA MJINGA MWEZAKO SASA UNAANZA KUTAPA TAPA

    KAMA MFA MAJI ULITEGEMEA MTASHINDA ILI UIBE VIZURI NA HUYO LOWASA WOTE NI MAFASIDI WAKUBWA

    ReplyDelete

Top Post Ad