MBOWE: Ulofa na Upumbavu Wetu ni Kwa Sababu ya CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema ili umasikini unaowakabili Watanzania uweze kuondoka lazima washirikiane kuiondoa madarakani CCM.

Amesema ulofa na upumbavu wanaodaiwa kuwa nao Watanzania umesababishwa na Serikali ya CCM kwa kuwa haiwajali Watanzania.

Mbowe  alitoa kauli  hiyo jana alipohutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Laini Polisi mjini Nzega, Mkoa wa Tabora  ambapo  pia alilazimika kuwapigisha kura za mikono wananchi wa Nzega waliohudhuria mkutano huo ili kutatua mvutano wa wagombea wa ubunge katika Jimbo la Nzega Mjini lililokuwa na wagombea wawili wa Ukawa.

Wakati wa kura hizo, mgombea wa Chadema, Charles Mabura, aliibuka mshindi dhidi ya mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Meza John.

Mgombea wa Ukawa alieteuliwa kuwania Ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Charles Mabula (kulia) akipeana mkono na aliekuwa Mgombea wa nafasi hiyo kwa Jimbo la Nzega mjini, Mezza Leonard (kati) akiekubali kushindwa baada ya kupigwa kura ya wazi na wananchi wa Nzega Mjini, jana Septemba 6, 2015.Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad