SUMAYE: Walioficha fedha nje watazirudisha; Magufuli haiingii Ikulu 2015

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Fredrick Sumaye
Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye,   amesema kama Lowassa atafanikiwa kuingia madarakani Watanzania walioficha fedha nje ya nchi watazirudisha.Sumaye alitoa kauli  hiyo jana alipohutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Laini Polisi mjini Nzega, Mkoa wa Tabora.

Kwa mujibu wa Sumaye, fedha hizo ambazo Serikali ya CCM imeshindwa kuzirudisha zitatakiwa kurudi kwa sababu ni mali ya Watanzania.

“Jana (juzi) mmemsikia Magufuli (Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli), akisema atakapoingia madarakani atarudisha mashamba ya wananchi yaliyoporwa.

“Kwanza kabisa namwambia Magufuli kwamba Ikulu haingii, lakini sisi tutakapoingia madarakani  tutahakikisha walioiba fedha za Watanzania na kuzificha huko Ulaya au Uswisi wanazirudisha,” alisema Sumaye.

Sumaye pia alizungumzia suala la rushwa nchini na kusema kama CCM wangekuwa waungwana wasingemsimamisha mtu yeyote kugombea urais kwa sababu wameshindwa kuwaletea maisha bora Watanzania.

“Magufuli anasema akiingia madarakani atakomesha rushwa sasa kama ana uwezo huo kwa nini ameshindwa kuikomesha wakati na yeye ni waziri katika Serikali iliyokithiri kwa rushwa?

“Magufuli anasema akiingia madarakani atakuza uchumi, kama kweli ana uwezo wa kukuza uchumi kwa nini ameshindwa kuukuza kupitia Serikali ya CCM ambayo yeye ni waziri?

“Magufuli hana lolote, msimchague kwa sababu ameshiriki kununua feri mbovu inayotoka Bagamoyo  kwenda Dar es Salaam,” alisema Sumaye.

Katika maelezo yake, Sumaye alizungumzia pia taarifa za viongozi wa CCM wanaodaiwa kuwatisha wananchi wasimchague Lowassa kwa kisingizio kwamba nchi itaingia katika vita kama ilivyotokea Libya na katika nchi nyingine za Afrika Kaskazini.

Sumaye alisema hakuna vita itakayotokea  wapinzani watakapoingia madarakani na kwamba vita hiyo itatokea kama Serikali ya CCM haitataka kuondoka madarakani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad