Mwakyembe: Lowassa ndiye Richmond...Aliamua Kujiuzulu Uwaziri ili Kukwepa Aibu Kama Ingejulikana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MJUMBE wa timu ya kampeni ya CCM, Dk Harrison Mwakyembe, amesema sakata la kashfa ya Richmond, haliwezi kuachwa kuzungumzwa na wanaCCM kwa kuwa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa ameanza kusingizia watu wengine kuhusika na kashfa hiyo, jambo ambalo alisema haliwezi kuachwa lipotee bila kujibiwa.

Aliyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Ubungo jana, mkutano uliokwenda sambamba na kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Dk Didas Massaburi.

“Unaposema kuna wakubwa juu waliamuru Mkataba wa Richmond usivunjwe maana yake unamsema Rais wa nchi.

"Katika suala lile hakuna rais wala nani, mhusika mkuu ni Lowassa na alifanya hivyo kwa uroho tu wa kutaka kujipatia fedha na upo ushahidi wa maboksi mawili.

“Tulimpa masharti mawili; Kwanza ajipime kutokana na ushahidi uliopatikana wa yeye kushiriki. Pili ilikuwa ni kwa Bunge kuthibitisha ushiriki wake endapo angegoma.

"Alichofanya ni kuamua kujiuzulu ili kukwepa aibu. Sasa katika hili rais anatokea wapi au anaposema alionewa ni katika lipi?” Alihoji.

Akizungumzia kutofuatana na Dk Magufuli katika mikutano yake kuzungumzia kashfa ya Richmond na kuachia makada wengine kuzungumzia suala hilo, Dk Mwakyembe alisema ni kutokana na wajumbe 32 wa Kamati ya Kampeni kuwa na majukumu katika maeneo mbalimbali nchini.

“Wale wajumbe 32 tumegawanyika katika maeneo mbalimbali, na kila mtu anaonana na wananchi kwa njia na staili tofauti lakini lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa CCM inaibuka na ushindi wa kishindo. Hata kama wajumbe wote 32 tukifuatana na Dk Magufuli hatuwezi kuzungumza wote kutokana na muda,” alisema.

Akimnadi Dk Masaburi, Dk Mwakyembe ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Kyela na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alisema mgombea huyo wa ubunge katika Jimbo la Ubungo kupitia CCM ni aina ya wachapakazi ambao wanahitajika katika uongozi ujao wa Dk Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo.

“Jimbo la Ubungo ni jimbo la kimkakati kutokana na umuhimu wake. Kwanza ni Jimbo la viwanda, pili ni lango la Jiji na hivyo ni sura ya Dar es Salaam, lakini tatu ni Jimbo la Elimu ya Juu kutokana na kuwepo kwa Chuo Kikuu na Chuo cha Usafirishaji. Dk Masaburi ni aina ya mbunge anayehitajika kuliongoza ili kulifanya Taifa kulitendea haki,” alisema.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

23 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu nae hajitambui, Lowassa kasema hakuna alichofanya Rais hajui, ajibu Rais sio wewe, Wewe mwenyewe ulisema hautoi ukweli wote ili Serikali isianguke, tutajie, alibaki nani? serikali ikasimama?

    ReplyDelete
  2. hiii Richmond hii ni old news, kwanini hamzungumzii ESCROW?

    ReplyDelete
  3. Mgonjwa huyu
    Ana kisasi na Lowassa
    Ubungo ya kubenea wala msipoteze muda

    ReplyDelete
  4. Niliamini kuwa mtu akisema flani mgonjwa au atatatizo anajitambua.Nimetafakari upya uzima wa kiakili wa baazi ya viongozi wa CCM.Moja anayeweza kusema mtu mgonjwa ni Doctor peke yake.Vinginevyo wewe unayesema mgonjwa ndio unaumwa.
    Pili Doctor Mwakyembe unashindwa kusoma alama za nyakati,tangu campain zimeanza hubirini Richmond and ugonjwa Lowassa anachanja Mbuga.Mabadiliko lazima.
    Tujibu maswahi haya.
    1. Tuonesha document zinazoonesha Rich mond yaluwasa.
    2.Tuzibitishie kwanini hadi leo umeme unakatikakatika.
    3.Kama rich mond niya lowassa kwanini mnailipa hadi leo.
    4.Ule mkataba Nani mwingine alisini mbali ya luwassa.
    5.Nani alikutana na Viongozi wa Richmond Marekani kabla ya mkataba kusainiwa.

    Msitudanganye hata awe vipi tunachihitaji ni mabadiliko.Nahisi umeishiwa sera.Umebaki peke yako unaihubiri richmond.

    ReplyDelete
  5. MWAKYEMBE UNA DHAMBI KUBWA NYINGI,LAKINI HAPA TUSEMEE CHACHE [NOTABLE] NI WEWE UIYEMWONDOA DR SLAA HAPA NCHINI KWAKE TANZANIA,KAKIMBIA.CHANZO, KIUHALIFU ULIMRUBUNI ZEE LA WATU 'UKAMPATIA PESA CHAFU ZA CCM,AKAYAKANA MAGEUZI NA MABADIRIKO NA SASA ANAJUTIA USALITI WAKE ULIOSABABISHWA NA WEWE.WATU HAWAKUJUI VIZURI.NI MTUNZI MAHIRI WA UONGO,UZANDIKI,UCHOCHEZI,UNAFIKI,MAJUNGU KAMA JIKE SHANGINGI.KWA UJUMLA KWA HILO UPO DARAJA A. PILI KUHUSU RICHMOND USIPINDISHE UKWELI,RICHMOND NI YA FAMILI YA KIKWETE NA ILE MITAMBO YAO ILIPOKWAMA SOUTH AFRICA KWA UHABA WA PESA ZA KUISAFIRISHA KUJA DAR-ES-SALAAM KIKWETE YEYE MWENYEWE ALIIAGIZA HAZINA BILA KUPITIA AFISA YEYOTE WA IKULU IWALIPE RICHMOND[PARTIAL SETTLEMENT] ILI WALIPIE MELI NA GHARAMA NYINGINEZO, WEWE MNAFIKI KWENYE BODI YA WAKURUGENZI WA RICHMOND WAPO RIDHWAN KIKWETE,MUSTAPHA KIKWETE,BATTULI MRISHO NA WENGINE WATANO NAKUULIZA WEE MNAFIKI MKUBWA MWAKYEMBE: HAWA NI AKINA NANI ? JEE UNAWAJUA?KAA KIMYA,TENA KIMYA KABISA MWAKYEMBE ,TUTAWAVUENI NGUO ZOTE,ZOTE KABISA,TUTAWAFUMUA.HII NI LALA SALAMA.

    ReplyDelete
  6. Dr. Mwakyembe naye atuambie makontena feki ya train yalipatinaje? hiyo familia kila mtu panya hamuaminiki October 25 out ili mjifunze. we are everywhere educating our fellow ordinary wananchi why should they vote NO to ccm.

    ReplyDelete
  7. It's too late!! Inakuwaje mnazungumza leo? kwanini hakushtakiwa?... Ukawa mbele kwa mbele tu

    ReplyDelete
  8. PATAMU HAPO!TUNASUBIRI UPANDE WA PILI,NA KAMA ITAKUWA KIMYA MAANA YAKE NI KWELI.Bado natafakari CCM au CHADEMA(maana hapa tukisema UKAWA ni uongo).Bado siku 26.

    ReplyDelete
  9. Mbona siku zote hizo hamukusema. Au ndio maji ya shingo

    ReplyDelete
  10. Hee leo hii tena lowassa kawa fisadi mbona hamukumuajibisha kipindi kile

    ReplyDelete
  11. RICHMOND NI YA KIKWETE NA FAMILIA YAKE, TUSUBIRI OCTOBER 25

    ReplyDelete
  12. hata mseme yoote tumeshawastukia tunataka tujue na ESCOW nani alichukua pesa kila siku richmond tu.WANAFKI WAKUBWA NYINYI NA NDIO MAAANA MUNGU AMEWALANI NA MWISHO WENU UMEFIKA HATA UMWANGE DAMU ZISIZO NA HATIA,LOWASA ANAZIDI KUCHAJI MBUGA,

    ReplyDelete
  13. ESCROW ACCOUNT.RUGEMALIRA BINAFSI ALIMUOMBA KIKWETE AINGILIE KATI ITOLEWE AMRI BENKI KUU KUSUDI PESA ZILE ZIINGIZWE KWENYE VIP ENGINEERING A/C YA RUGEMALIRA.ALISHIRIKISHWA WAZIRI WA NISHATI PRO.MUHONGO,MWANASHERIA MKU WA SERIKALI -WEREMA,MTU-KATI WA IKULU GURUMO NA GAVANA WA BENKI KUU NDULLU.KWANZA GAVANA ALIISTUKIA DEAL ALIKATAA LIKAJA SHINIKIZO TOKA IKULU AKALEGEA.WEREMA AKAJIINGIZA KICHWA-KICHWA BAADA YA BOSI WAKE KUMSHINIKIZA AANDIKE BARUA BOT AKIONYESHA UHALALI WA TRANSACTION HIYO.PESA IKATOKA,KAIPOKEA RUGEMALIRA,SASA MGAO WA MAFUNGU.KIWANGO ALIKUA ANATOA RUGEMALIRA KWA JINSI MTU BINAFSI ALIVYOSHIRIKI.HUYU HIKI,YULE HIKI NA HUSUSANI YULE MTOA AMRI ALIYEFANIKISHA DEAL NZIMA BILLION TANO CASH.HIZI BILLION TANO ZA ESCROW RUGEMARILA ULIMPA NANI?

    ReplyDelete
  14. Kweli Mwakyembe amejivu njia kapokea dire. Kumbe mnaficha maovu ila watu wakitoka CCM ndo mnataja madhambi yao haya sema yote kama wewe mwanaume unaemuogopa Mungu. Vinginevyo njaa zenu na uchu wa madaraka vinawafanya kubwabwaja ujinga. TUMECHOKA

    ReplyDelete
  15. BILION TANO KWNYE SANDUKU KUBWA LA BLUE LENYE STRIPS NYEUPE/NJANO LILIPELEKWA KWANZA URSINO,NA KISHA BAADAYE USIKU LIKAPELEKWA MSOGA.PENYE UDHALIMU HAPAKOSI MALAIKA WA MUNGU ATAKAYEFICHUA MAOVU.WALIFIKIRI WAKIFANYA WIZI HUO ITAKUA SIRI WAKALISHANA YAMINI LAKINI NDIO HIVYO TENA,KUMEKUCHA-KWEUPEEEEEEE.

    ReplyDelete
  16. Muongo mkubwa wewe
    Ulidai ulipewa sumu yameishia wapi
    Ulikuwa na dalili zote za ngoma
    Mnakunywa dozi
    Ila magojwa ya wenzenu mmeyavalia njuga

    ReplyDelete
  17. Jamaa anakumbuka shuka wakati ndo kumekucha,,,,,,,..,..,......alikuwa wapi huyu leo ndo anafikiri atushawishi kuwa lowasa ndo Richmond?

    ReplyDelete
  18. HILI LI MZEEE HATA AIBU HALINI SIJUI UDOKTA LILIUOPATAJE?

    ReplyDelete
  19. tumeshaelewa sasa RICHMOND asilimia 100 ni ya famili ya kikwete.asante sana.kwa hilo,sasa watakaa kimya,wameshikwa na bumbuazi na uchaguzi mkuu tumebakiza siku 24.tuzitunze vizuri kadi zetu ili kwa amani,kwa utulivu tuiadhibu ccm kwenye sanduku la kupiga kura mnamo jumapili tarehe 25 octoba 2015

    ReplyDelete
  20. JAMANI MNAZIJUA SERA KUBWA MBILI ZA SISIEM?
    1. RICHIMOND
    2. UGONJWA WA LOWASA.

    FUATILIA MIKUTANO YAO YOTE HIZO NDIO SERA ZAO KUBWA ZINAZOCHUKUA MUDA KUZIELEZEA!!

    ReplyDelete
  21. MWAKYEMBE SIKU ZOTE ULIKUWA WAPI KUSEMAAAAAA??? VIBAYA HIVYO KAKA!!

    ReplyDelete
  22. Mashairi yenu na ngonjera zenu tunazifahamu na tumezichoka! Lowasa ndio Raisi wetu, huu ni mwaka wa wanyonge na walio kandamizwa kutesa. Familia za vigogo ndio zinazo miliki kila kitu nchi hii, siku zenu zinahesabika, Mungu atatuamulia nani ni nani tarehe 25. Hivi nyie hamna sera mbali ya Lowassa ? Average Mind speaks about personalities but Smart Mind speaks about Issues , if you have a colonised Mind it's hard to think outside the box. God bless Tanzania , God stand for Lowasa.

    ReplyDelete
  23. MUANGALIE VIZURI MWAKYEMBE RANGI RANGI ANA SURA KUU TANO,NYEUSI,BLUU,NJANO,KIJANI NA HUDHURUNGI KIMAKOSA ALIZALIWA KAMA BINADAMU LAKINI YUPO KWENYE KUNDI LA PUNDAMILIA NA NDIO MAANA UBONGO WAKE UMEKAA KIPORI-POLI,SHETANI MKUBWA.

    ReplyDelete

Top Post Ad