Sentesi 11 Ngumu MBOWE alizozitoa mbele ya Waislam Jana Siku ya Idd

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Viongozi wakuu wa umoja wa katiba ya wananachi UKAWA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Mh FREMAN MBOWE pamoja na makamu mwenyekiti wa CHADEMA Profesa SAFARI na kaimu mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF ambaye pia ni mbunge wa bunge la Africa mashariki Mh TWALHA TASLIMA leo jioni wamehudhuria Baraza la kuu la idd lililoamndaliwa na Taasisi za kiislam Tanzania shughuli iliyofanyika katika hotel ya LAMADA Jijini Dar es salaam.


Katika shughuli hiyo ambayo iliambatana na dua mbalimbali pamoja na hotuba za viongozi mbalimbali pia walialikwa wagombea urais wa vyama vyote Tanzania lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kufika huku mgombea wa UKAWA akiwakilishwa na Mh FREMAN MBOWE.
Mh mbowe alipata nafasi ya kutoa Hotuba fupi ambayo iliwagusa mamia ya waislam ambao walikuwa katika shughuli hiyo na hapa nimekunukulia baadhi ya mambo ambayo mbowe aliyazungumza na kushtua wengi

1-Nashukuru sana kwa ukaribisho wa shughuli hi,mgombea wetu ndugu EDWARD LOWASA alitamani kuwa nasi jioni hii lakini kutokana na ratiba ya kampeni kubana imebidi aunganishe kwenda kwenye kampeni za kesho huko manyara--MH MBOWE  

2-Swala la mashekh ambao wapo jela bila hukumu yoyote,tulisema siku ya ufunguzi wa kampeni na tunaendelea kusema kuwa tumewaagiza wanasheria wa chama chetu kufwatilia kwa makini na kuona nini hasa kimetokea kwao kama kuna mahali kunahitajika msaada wa kisheria tupo tayari kulishuhulikia hilo kwani sisi lengo letu ni kurudisha umoja na mshikamano Tanzania. --MH MBOWE

3-Zimebaki siku takribani 30 sasa kabla ya watanzania kufanya maamuzi halisi,ni muda wa maamuzi ndugu watanzania. --MH MBOWE

4-TANESCO imefilisika na watanzania wengi hawajui hili,sasa shirika la umeme halina hata sent na wameamua kufanya mgao wa kimya kimya lakini ukweli ni kwamba huu mgao ni mkubwa sana huko tuendako kwa sababu hawana hela na wanaficha ukweli,kuna mgao mkali sana sasa wa kimya kimya na utaendelea kuwa mkali kadiri siku zinavyokwenda. --MH MBOWE

5-Kuna wizi mkubwa sana wa mafuta Tanzania na kuna baadhi ya watu wakubwa wanauratibu wizi huo,Tanzania ina akiba ya mafuta hadi mwezi wa 11 lakini serikali imetoa hati ya kuingiza mafuta nchini ambapo baadhi ya wahusika ni familia ya Rais KIKWETE. --MH MBOWE

6-Serikali yetu ya awamu ya tano sio serikali ya visasi kama inavyodhaniwa,ila ni serikali ya kuwarudisha watanzania pamoja kwa maridhiano,na maelewano,ila kuna watu itabidi washughulikiwe kwa mijibu wa sheria kutokana na kuligharimu taifa hao tutafanya hivyo. --MH MBOWE

7-Tume ya uchaguzi ya miezi miwili iliyopita sio tume ya sasa,mwenyekiti yupo ila watendaji wengi wameondolewa bila sababu za msingi. --MH MBOWE

8-Mtendaji mmoja mkuu wa tume juzi tumepata taarifa kuwa ameondolewa na kupelekwa kusikojulikana na amerudhishwa na kutakiwa kukabidhi ofisi mara moja. --MH MBOWE

9-Tume ya sasa inaongozwa na wanajeshi na usalama wa taifa,mimi mbowe ndio nasema kama kuna mtu anabisha waje wanikamate leo,hatuwezi kuvumiliana kiasi hiki ni wakati wa kuwekana wazi ili watanzania wafanye jambo wanalolitaka. --MH MBOWE

10-Nasema hivi hatutakubai hujuma hizi ambazo zinaendelea sasa tutasema hadi mwisho. --MH MBOWE

11-Mwisho kabisa nasema hivi ni wajibu wetu kutafuta kura,kupiga kura na kulinda kura hivyo ndugu zangu waislam nawaomba tushirikiane katika hili,ASANTENI KWA KUNISIKILIZA--MH MBOWE
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. 1.Kama kuna ukweli ama ni uongo sijui kwa kuwa hakuna kitu kinathibitisha kama usemayo ni kweli.
    2. Inawezekana kuwa ni maneno ya kampeni tu,ila mimi binafsi ni bora
    kura yangu niipigie CCM,kuliko CHADEMA maana kwa masikio yangu nilimsikia
    Lowasa anasema eti haijawahi kutokea kiongozi mluteli mwaka huu tumchague yeye.
    je huo sio ubaguzi wa dini?wakristo wenyewe wanabaguana uluteri na roma,JE?
    Tuombee Amani .

    ReplyDelete
  2. Mkubwa unaposema uongo unadharaulika bro.
    Tanesco imefilisika?mbona wafanyakazi wa TANESCO hatujui hilo,wewe umelipata wapi?
    Siasa za uongo ni kujiharibia na hapo hujui umeshapoteza kura nyingi kwa uongo wako,hivi ni mangapi umeongopa?kubwa kumbe ovyoooo.

    ReplyDelete
  3. Wanasiasa wengi wao ni waongo.
    Wakati wanataka kura wanakuwa fisi alievaa ngozi ya kondoo na bahati mbaya sana watanzania walio wengi (majority) ni wavivu wakufanya kazi na pia wavivu wakufikiri, wengi wao ni watu wakufwata mkumbo tu na hii ni hatari sana kwa maendeleo na usalama wa nchi yetu. Nahofia sana future ya nchi yetu.

    ReplyDelete
  4. DJ Mbowe anaongea mpaka povu,yaani ingepeza kama huyu ndio angekuwa Lowasa.
    Mmmh kumbe kuna maisha baada ya uchaguzi,uwiiiiiiiiiiiiiiii,ngachoka!

    ReplyDelete
  5. Wanasiasa wengi ni waongo. Wakati Wa uchaguzi wanakuwa fisi waliovaa ngozi za kondoo. Na kitu cha kusikitisha ni kuwa watanzania wengi ni wavivu wakufanya kazi lakini pia ni wavivu wakufikiri, wengi ni wafwata mkumbo. Ninahofia sana future ya nchi hii. Mungu Tujaalie kiongozi muadilifu, Mungu Tujaalie amani.

    ReplyDelete
  6. Kuliko kuongozwa na Lowasa ne heri jeshi lichukue madaraka.....Lowasa HAFAI, HAFAI tena HAFAI kuwa Rais wa Tanzania........FISADI PAPA, mara kajinyea, mara kajikojolea......kwakweli HAPANA

    ReplyDelete
  7. Na huyo macho-kumchuzi asitake kutubadilishia gea angani kama kawaida yake.......HAPA KAZI TU!!

    ReplyDelete
  8. Sasa hilo lilikuwa baraza la Idd au mkutano wa kampeni?? Lowasa kapiga kampeni kanisani, Mbowe kwenye mabaraza ya Idd.........na bado, mtaweweseka sana tu.....

    ReplyDelete
  9. wote msiotaka mabadiliko mna walakini , hii ni dunia kila siku inamambo mapya. kaeni na ujinga wenu wa kuona mabadiliko ni hasara.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mabadiliko gani?kudanganywa kama watoto?Usiamini kama kila m-TZ atakuwa tajiri hata atawale miaka 10.Enzi za safari ya matumaini(enzi hizo nikiwa CHADEMA )ndio nilijua huyu jamaa ana lake jambo,na bora alikatwa,CCM waliona mbali.
      Mabadiliko yanakuja chini ya DK.J.P.Magufuli.

      Delete
  10. Mtapiga kampeni mpaka katika vyoo vya site, mtajutraaa kulibeba lile 'zigo' lililotupwa na CCM.......mnahaha kulisafisha lakini wapii, mnalo limewaganda

    ReplyDelete
  11. Mzee wa kubadili gia angani, utajuta kuuza cdm kwa fisadi, we jipange na uendelee kutafuta visingizio, ili upate cha kuwadanganyia wanachama wako, mara jeshi, mara usalama wa taifa...MTAISOMA NAMBA

    ReplyDelete

Top Post Ad