EDWARD LOWASSA Kumzika Marehemu Mchungaji Mtikila Licha ya Maneno yote Kabla ya Kifo Chake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema kupitia mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa, anatarajia kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrati (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, imefahamika.

Duru za siasa kutoka ndani ya Ukawa, zimebainisha kwamba, licha ya kusambazwa kwenye mitandao kwa taarifa za Mchungaji Mtikila kumshambulia Lowassa kwa maneno kabla ya kifo chake, lakini mgombea huyo wa Ukawa amepanga kwenda kuhudhuria mazishi hayo kutokana na sababu kadhaa.

“Kwanza amesema Mtikila ni miongoni mwa waasisi wa siasa za mageuzi nchini na ametoa mchango mkubwa katika mambo mbalimbali yaliyobadilisha demokrasia na kupanua wigo wa siasa za upinzani,” kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya Ukawa.

Lakini pili, kwa mujibu wa chanzo hicho, ni kushindwa kuhudhuria misiba kadhaa ya wanasiasa waliofariki dunia katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.


Hakuhudhuria msiba wa Peter Kisumo kutokana na kususa baada ya msafara wake kuzuiliwa, lakini hakwenda kumzika mgombea wa Chadema katika Jimbo la Lushoto, Mohammed Mtoi na hakuhudhuria msiba wa aliyekuwa Waziri wa Utumishi, Celina Kombani, ambaye alikuwa anatetea kiti chake katika Jimbo la Ulanga Mashariki kupitia CCM,” kilibainisha chanzo hicho.

Mchungaji Mtikila alifariki kwa ajali ya gari Jumapili, Oktoba 4, 2015 katika Kijiji cha Msolwa mkoani Pwani wakati akirejea Dar es Salaam kutoka Njombe alikokwenda kufanya mkutano wa hadhara. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya mwanasiasa huyo, David Mwaijojele, mwili wa marehemu utasafirishwa leo kwenda Ludewa, Njombe na endapo kila kitu kitakwenda sawa, Mchungaji Mtikila atapumzishwa kaburini kesho.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Msema ukweli ni mpenzi wa mungu,mtikila alikuwa mkweli na muwazi,Lowasa kapewa ukweli, hana hata moja la kupinga kutokana na maneno ya Mtikila kabla ya kifo chake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mungu kamjibu. RIP Mtikila
      Na wengine atawajibu karibuni

      Delete
    2. Makongoro , na wote waliosema Lowassa mgonjwa
      Mtikila anawaita aandaaeni makaburi yenu

      Delete
  2. CCM WALIKUA WANAPEWA UKWELI NA MTIKILA KWA MIAKA 35 TANGU MWALIMU AKAJA MWINYI,AKAJA MKAPA NA HUYU WA SASA KIKWETE.KUHUSU KIKWETE MTIKILA ALIWAHI KUSEMA "JAKAYA NI MWIZI NA MPORAJI,IKULU AMEIGEUZA KICHAKA CHA MAFISADI PAPA JAKAYA AMELIMBIKIZA MABILLION KWENYE MABENKI YA NJE,JAKAYA ANAITUMIA VIBAYA,KWA MABAVU NAFASI YAKE KUUA UPINZANI TANZANIA" NA MENGINEYO MAKALI ZAIDI. KWA KUA ALIKUA MUWAZI NA MSEMA UKWELI KWA KIPINDI CHOTE HICHO SI CCM WALA JAKAYA MRISHO KIKWETE RAIS ANAYEMALIZIA MUDA WAKE 25 OCTOBA 2015 WALIWAHI AIDHA KUMKANUSHA MTIKILA AU KUMSAHIHISHA KWA HIYO.ALIYOKUA AKIYASEMA YALIKUA NI YA UKWELI,NA YATAENDELEA KUBAKI HIVYO.

    ReplyDelete
  3. Nenda ukazike mzidi kumalizia kafara mlilotoa kwa mtikila kumbukeni kila nafsi itaonja umauti hata uwe Bilionea, raisi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kafara lipi wewe acha usenge

      Delete
  4. HAKUNA SUALI AU OVU LA CCM LITAKALOKOSA MAJIBU.NI HERI KUANZIA SASA MFUNGE MABAKULI YENU ILI KUPUMUA,KUJINUSURU,KUPUNGUZA MSONGO WA MAWAZO CCM MBAKI KIMYA,KAENI KIMYA KABISA KAMA MI-ROBBOT.TUNA HASIRA KUBWA,KALI NA NYIYI NA KUMBUKENI,NDIO MNAELEKEA KUZIMU HIVYO,NA BADO SASA HIVI TUNAWAANDALIA BAKORA ZA MIIBA TUWACHUBUE KICHAPO HADI MATAKONI.

    ReplyDelete

Top Post Ad