FLORA MBASHA Akiri..Mwanangu si wa Emmanuel Mbasha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

OHOOO! Kimenuka tena. Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amesema mwanaye mdogo (jina linahifadhiwa) hahusiani hata kidogo na aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha huku akidai kuwa anamtambua mwanaume huyo kama mzazi mwenzake kwa mtoto mmoja tu (Liz), Risasi Jumatano linakupa zaidi.

Akizungumza na waandishi wetu kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki, Flora alisema amechoshwa na manenomaneno yanayosemwa juu yake na Emmanuel na kwamba kama mumewe huyo ameamua kumwaga ugali, yeye yupo tayari kumwaga mboga.

Mwimbaji huyo alisema kwamba kauli aliyoitoa hivi karibuni kuwa anampenda mumewe na kwamba yupo tayari kuishi naye haikutoka moyoni, isipokuwa alifanya hivyo kwa huruma tu, kwa sababu mwanaume huyo ni mtu katili, mwenye roho mbaya na asiyemuogopa Mungu.
“Mtu mwenyewe alimtelekeza mtoto (Liz) kwa zaidi ya mwaka mmoja, ni mtu mbaya sana, sina mapenzi na Mbasha hata kidogo, ni afadhali niolewe na chizi anayeokota makopo kuliko kurudiana na mtu katili na mnyama kama huyo, namheshimu kama mzazi mwenzangu kwa Liz,” alisema.
Mtoto anayedaiwa kuibua mazito.

“Huyo mwanaume hafai kabisa, ni katili, namfananisha na shetani, anajifanya mwema kwa watu wakati hajawahi kuiomba msamaha familia, sikubaliani kabisa na hukumu ya mahakama, ukweli anaujua kwamba alibaka na hata mkimtaka huyo binti mumhoji nitamleta, isitoshe sasa hivi hata mtoto wake hamjali, hajui anasoma vipi, hajawahi kulipa hata shilingi ya ada, mimi mwenyewe ndo nahangaika kumlea mwanangu Liz ambaye anasoma kidato cha kwanza.


“Hastahili kabisa kuitwa baba sababu mzazi mwenye akili hawezi kutelekeza familia hata kama tumegombana, nimemwachia nyumba niliyojenga kwa pesa yangu na pesa zote aliweka kwenye akaunti yake na zote nilimwachia lakini kashindwa kuihudumia familia.”


Flora anajulikana kuwa na watoto wawili, mdogo akiwa ni yule aliyezaliwa wakati wanandoa hao wakiwa katika mzozo uliosababisha watengane hadi hivi sasa. Alipoulizwa kwa nini anadai aliyekuwa mumewe kumtelekeza mtoto mmoja tu, badala ya wawili, alifunguka.
“Huyu mwanangu mdogo hausiki naye kabisa, tena asiwe anamtaja kabisa kwa sababu hamhusu, hajui hata matumizi yake yakoje, mengine kaka achana nayo tu,” alisema Flora.
Mwimbaji huyo mwenye kipaji alipoulizwa sababu za kufuta kesi ya kudai talaka, aliyoifungua hivi karibuni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati anadai hamtaki na hawezi kurudiana naye, alisema alifanya hivyo baada ya kushinikizwa na mtu ambaye hata hivyo, alikataa kumtaja.
Mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha.\

Flora alisema familia yake haijaridhishwa kabisa na suala la kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili mumewe kumalizika kwa kuachiwa huru na kwamba wanajipanga kwa ajili ya kukata rufaa.“Hiyo kesi imeisha kisiasa, Mbasha aliwahi kukiri kuwa ni kweli alifanya kitendo hicho, iweje leo aonekane hana hatia? Tutakwenda kukata rufaa ili haki itendeke.”

Baada ya kuzungumza na Flora, mwandishi wetu alimtafuta Mbasha kwa lengo la kumuuliza kuhusu madai ya mtoto yule mdogo kutohusika naye kama alivyosema mkewe, naye bila ‘kutafuna maneno’, alisema hata yeye hamtambui huyo mtoto mdogo, ila anaomba arudishiwe mtoto wake mkubwa, Liz na maisha mengine yaendelee.
“Hata mimi simtambui huyo mwingine, ninachoomba anirudishie tu mtoto wangu mkubwa Liz, huyo mwingine sihusiki naye kabisa kama alivyosema, yeye (Flora) ndiye anajua mhusika wa huyo mtoto, lakini si mimi na wala hajakosea kusema hivyo, nililitambua hilo tangu zamani, anipe tu mwanangu wa kwanza,” alisema Mbasha.

Source:GPL-meandikwa na Brighton Masalu, Mayasa Mariwata na Gladness Mallya
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wote wa sanii wa injilibnankomedian hao

    ReplyDelete
  2. wako wengi waaobambikiwa watoto, lakii emma alistuka mapema!

    ReplyDelete
  3. Flora si alisema kamsamehe sasa ilikuwaje tena mtoto si wambsha? ulifikiri utamuingia mkenge sio Domo huyoooooo

    ReplyDelete
  4. Nonsense both of them.

    ReplyDelete
  5. mbasha hajui kutunza ndio shida aliyonayo.flora we lea watoto wako kama vile hawana baba ,mbasha ni uzuri watosha hana jipya

    ReplyDelete
  6. Frola muongo umesaliti ndoa kuzaa na mtu jeba mwingine, halafu unasena Emmanuel kabaka ndugu jayo wewe ni muongo mkubwa, Emmanuel yupo ulaiani sasa sasa wewe frola unasema oo mtoto wa pili si wa Emmanuel hamna mtu anataka kujua huyo mtoto, utajiju mwenyewe na Emmanuel hataki kujua, hahahaha shem on you Flora. Emmanuel ni mrembo kila mwanamke anamtamani. Flora hauna mvuto hupendezi hata kidogo pamoja na mkorogo. Wadau kutoka Sweden

    ReplyDelete
  7. Biblia inasema, mwanamke mpumbamvu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake. Vilevile Yesu alituagiza kusamehe 7 mara70. Kwhyo alicho fanya huyu mama, japo Ni mwinjilisti, anaonekana hasomi biblia, alichofanya hakuna tofauti na watu wa mataifa wasio mjua Mungu.
    Kumshtaki mumewe, yaweza kuwa mbinu ya kupumbaza watu juu ya dhambi aliyofanya, baada ya kupata ujauzito nje ya mumewe. Tabia ya shetani hubadilika Kama kinyonga. Hivi unaweza kumwambia mtu nimekusamehe, kisha ukasema tena nilishinikizwa nisingekusamehe....huoni ndani kuwa shetani ndo anafanya kazi (kukuendesha) badala ya kumwendesha! Imma Ana Roho wa Mungu ndo maana kablock.
    Mungu hadhihakiwi.

    ReplyDelete
  8. We Edna akili yako Kama Flora. Ndo walewale, hamuwezi kutulia Na waume zenu uhuni Tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad