Kafulila Alitetemesha Serikali Kwa Kuibua Ufisadi wa ESCROW, Lembeli na TOKOMEZA. Sasa Yamewakuta! Hawa Ndio Watanzania!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

UKAWA wanasema ufisadi ni maisha ya mfumo wa serikali ya CCM. Hivyo wakasisitiza kuwa dawa ya ufisadi ni kuiondoa serikali ya CCM madarakani. Lakini kuendelea kukomaa na ufisadi bado sio kete muhimu ya kuwang'oa CCM. Na hili ndio chimbuko la kukubali kumpa Lowassa ridhaa ya kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA!

Na kweli hili limedhihirika mchana kweupe kabisa. Hakuna kashfa kubwa iliyowahi kuitetemesha serikali kama ya ESCROW iliyoibuliwa na David Kafulila na OPERESHENI TOKOMEZA iliyokuwa chini ya James Lembeli.

Lakini cha ajabu leo hii hawa wawili hawapo bungeni. Wameangushwa. Kwa namna ambavyo wamejitoa mhanga kwa ajili ya kuwatetea wananchi nilitegemea huu pia ni muda muafaka wa wananchi hususan wa majimbo yao kuwapigania na kuwatetea kama wana ubungo wana kibamba wana kawe walivyowatetea makamanda wao!

Kama watawala wakiona kuwa una back up kubwa kutoka kwa wananchi wanakuogopa na kukuacha ushinde lakini wakiona kuwa back up yako ni ndogo sana basi wanakomaa na kuhakikisha kuwa unang'oka.

Tukumbuke akina Sign wana mpango wa kumfungulia Kafulila kesi kisa mambo ya Escrow. Kafulila shujaa wa Taifa kakosa watetezi!

Itoshe kusema kuwa hawa ndio watanzania wetu. Na hii ndio nchi yetu, Tanzania. Pengine kuna watanzania wengi hatujui nini tunachokitaka!

CCM waliwahi kusema hawapo tayari kukabidhi nchi kwa karatasi! Na wanaishi kauli yao hii!
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. TUKUBALI MATOKEO,MTAJUTAAAAAAAAAAA KUMNYANYASA ZITO KABWE!LOL!

    ReplyDelete
  2. Kata rufaaa tutakulipia gharama zote
    Mimi ntatoa 100000000

    ReplyDelete
  3. Masikini Mr.two mbili anarudi kichakani kula majani!

    ReplyDelete

Top Post Ad