Kufuatia Kazi Nzuri Iliyotuka Inayofanywa na ITV, Mnaonaje Mzee Mengi Akabidhiwe Kuiendesha TBC?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kufuatia Kazi Nzuri na Iliyotuka Inayofanywa na vyombo vya habari vya IPP, in particular, kituo cha televisheni cha ITV, katika uchaguzi huu, Jee Mnaonaje Kama tukiishauri serikali ijayo, imkabidhi Mzee Reginald Mengi, Jukumu zito la Kuiendesha TBC?!.

Najua wazo langu hili litapata upinzani, toka kwa watu wanaojiita wazalendo, kwa kuleta hoja, huwezi kuibinafsisha TBC kwa sababu ni taasisi nyeti!. Hili sio jambo la ajabu, Tanzania tumeisha binafsisha taasisi mbalimbali na nyingine ni nyeti zaidi ya TBC mfano, City Water, TTCL, Tanesco, TRL, ATC etc.

Swali hili ni kufutia ITV kuwa ndio tegemeo pekee la taarifa za matokeo ya Uchaguzi Mkuu, as if ITV ndio TV ya Taifa, jukumu ambalo lingepaswa kubebwa na TBC!. Kama hoja ni uzalendo, ni nani mzalendo halisi wa taifa hili kati ya ITV na TBC?!.

Hongera sana ITV, Hongera Mzee wetu, Reginald Abraham Mengi, hongera menejiment ya ITV ikiongozwa na Iron Lady, Joyce Mhavile, na Hongera kwa News team yote ya ITV ambayo ni hakuna kulala, mnafanya kazi 24/7, hivyo na sisi huku majumbani mwetu, tunakesha na nyinyi!.

Mungu awabariki sana!.

Maoni Huru Kutoka Kwa Pasco /Jamii Forums
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad