Magufuli Apiga Mashambulizi Jimboni Kwa Mbowe......Asema Mbowe ni Mbunge mtalii Anayeshinda Akizurura Ulaya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, ametikisa katika Jimbo la Hai na kumshambulia Mbunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema aliyemaliza muda wake,  Freeman Mbowe  kwamba ni Mbunge mtalii anayeshinda akizurura Ulaya, huku akishindwa kutatua kero za wapiga kura wake.

Akihutubia jimboni humo katika siku yake ya kwanza ya kampeni mkoani Kilimanjaro jana, Dk. Magufuli aliwaambia wananchi wa jimbo hilo kwamba, walifanya biashara ya hasara kumchagua Mbowe kuwa Mbunge wao kwani hajali maslahi ya wananchi wake.

Awali mgombea huyo wa CCM alipokelewa na umati wa jimbo hilo kwa mabango yenye ujumbe mbalimbali yanayoelezea kero za maji, barabara, elimu na afya, ambayo aliagiza yachukuliwe na msafara wake ili atakapoingia Ikulu azifanyie kazi kero hizo.

Dk. Magufuli alisema wananchi wa Jimbo la Hai wameteseka kwa muda mrefu kwa kuwa na Mbunge ambaye kazi yake imekuwa kuzunguka jijini Dar es Salaam na mataifa ya Ulaya na Marekani, huku jimbo likikabiliwa na matatizo ya kijamii kama maji, elimu na ukosefu wa huduma za afya.

“Ingawa nampenda Mbowe, lakini wananchi wa jimbo hili wanapaswa kufanya mabadiliko kwa kumtosa Mbunge huyo  abaki na nafasi yake ya uenyekiti wa Chadema ili akaimarishe chama hicho na wamchague mbunge wa CCM ambaye atawasaidia,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Magufuli, Mbowe hawezi kushughulikia masuala ya maendeleo kwa kuwa anakabiliwa na majukumu mengi ya biashara na uenyekiti wa Taifa wa Chadema.

“Mbowe ana nipenda na huwa ana nisifia hadharani kwamba mimi ni mchapakazi na mimi pia nampenda sana lakini kwenye masuala ya maendeleo ya Watanzania sitaweka urafiki achaneni naye na mumchague Dunstan Mallya wa CCM awafanyie kazi watu wa Hai.” alisema mgombea huyo wa CCM.

Alisema hata Halmashauri ya Wilaya ya Hai ambayo inaongozwa na Chadema imeshindwa kuondoa kero za wananchi na kuongeza kuwa ingawa wilaya hiyo ni ya zamani imebaki nyuma kwa miaka mingi kulinganisha na wilaya mpya.

Akiwahutubia wananchi wa Siha, mkoani hapa jana, Dk. Magufuli alisema ameshajihakikishia ushindi wa kishindo na kudai wapinzani wanamsindikiza na kuwataka wananchi wa jimbo hilo wamchague Agrey Mwanri kwa mara nyingine awe Mbunge wao kutokana na kazi nzuri aliyowafanyia.

Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Dk. Emmanuel Nchimbi, aliibukia kwenye kampeni za Dk. Magufuli wilayani Siha na baadaye Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro jana na kumrushia makombora mgombea urais  wa Ukawa, Edward Lowassa.

Dk. Nchimbi ambaye alikuwa swahiba mkubwa wa Lowassa kwenye harakati za kuwania kuteuliwa na CCM kuwania urais, alidai Lowassa ni dhaifu na hawezi kuiongoza Tanzania.

Nchimbi alisema Watanzania wanahitaji  Rais aina ya Magufuli ambaye atawaendesha mchakamchaka wa maendeleo na si wagombea wengine ambao historia zao zinaonyesha walishindwa kwenye nafasi za juu walizowahi kushika.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Usipoteze muda kaskazini
    Bora uwende Chato

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa hiyo unakubali kuwa ukabila ndio hasa ngao ya UKAWA(CHADEMA?)

      Delete
    2. Si ukabila Bali kukubalika
      Mimi msukuma vile vile
      Lakini CCM sipendi

      Delete
  2. Weraaaaaaaaaaaaaa!
    CHAGUA MAGUFULI,MUONE KAZI.

    ReplyDelete
  3. MZEEE SIMUELWI KABISA

    ReplyDelete
  4. HA HA ETI RAISI WETU,GADAFI RAISI WA IRAQ HAPANA KUWEIT WATU EEEEEEEH KWELI
    UKISTAAJABU YA CCM UTAYAONA YA MAGUFURI

    ReplyDelete
  5. CHATO MPK LEO MAJI NI SHIDA UMASIKINI FULL MUSIC ,KWANZA HAWAMTAKI CHATO NDIO MAANA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA ALIANGUKIA PUA

    ReplyDelete
  6. Annze. Kusema boss wake kuhusu kuzurura
    Jk
    Vasco dagama
    Mwenye PHD feki Kila chuo duniani

    ReplyDelete
  7. MTAELEWA TU,MNAKATAA UFISADI CCM WAKATI MNAKARIBISHA MAFISADI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousAugust 28, 2015 at 11:41 AM
    Kuna watu respectable wenye CV zao za maana duniani…lakini walivyojihusisha na CCM wamechafua CV zao;
    Mfano;
    Getruda Mongela mwanamama aiyeongoza mkutano wa Beijing unajua kashfa za rushwa zilizokuja kumkumba
    Sospeter Muhongo-A respectable Journalist unajua Amefanya nini kwenye ESCROW
    Omar Nundu mtaalamu wa dunia wa usafiri wa anga unajua ni nini kimemtokea
    Prof Anna Tibaijuka mama aliyeongoza shirika la Umoja wa mataifa unajua nini kimemtokea
    Daudi Balali a respectable IMF and World Bank Economist unajua nini kimemtokea baada ya kujihusisha na CCM.
    Ukiachana na hao…Jakaya Kikwete wakati anaingia madarakani alikuwa mtu mchapa kazi…Katika wizara alizopita kabla ya hapo alikuwa mwadilifu na Mchapa kazi…alichaguliwa kwa 80% kumbuka….Nini kimetokea baada ya kuwa Ikulu?
    Benjamin Mkapa..Jembe la Nyerere aliingia kama mzee wa kazi ameondoka na kujimilikisha mgodi wa Kiwira.
    Magufuli anayegombea urais wa CCM Alishiriki kikamilifu katika kuuza nyumba za serikali….Ameshiriki kuiingiza hasara serikali majuzi kwenye kivuko ca kigamboni shs Bilioni 8…Kivuko hakina muda wa miezi mitano lakini hakifanyi kazi ….ameiingiza hasara serikali kwa maamuzi mabovu mengi aliyofanya.
    Ndio maana kwa tunaotazama mambo kwa umbali ni bora CCM ikakaa pembeni tuanze upya (Sio kwamba wapinzani ni wazuri sana)…Kutakuwa na maumivu ya miaka 5 lakini baada ya hapo tuta endelea kama taifa.
    Kama taifa inabidi tuweze kufanya maamuzi magumu kwa mustakabali wa vizazi vyetu vijavyo.
    Mfano kulikua na haja gani ya kumilikisha kampuni za wazungu gesi yetu kwa miaka 99…tena kwa mikataba ya siri…….
    Utakuwa kichaa kudahani magufuli ataipitia hio mikataba na kuifumua…You must be mad

    ReplyDelete

Top Post Ad