Membe Amtaka Lowassa Aache Kujifananisha na Yesu.......Asema Hana Ubavu wa Kumfufua Balali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia anaungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, hana uwezo wa kumfufua aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT),  marehemu Daud Balali.

Membe ambaye jana alionekana kwa mara ya kwanza katika kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, alisema Balali alikufa kifo cha kawaida na hataonekana tena.

Akizungumza na wakazi wa Lindi Mjini kwenye kampeni za mgombea huyo wa urais wa CCM, Membe alisema anajua vizuri namna Balali alivyougua hadi kufariki dunia, hivyo mgombea kuahidi kumleta mtu aliyekufa ni jambo la kushangaza.

Membe alisema Balali aliugua maradhi ya utumbo na kwenda kutibiwa nchini Marekani mwaka 2008 na baadaye alifariki dunia na kuzikwa kwenye makaburi ya huko huko.

“Lowassa aache kujifanya Yesu kwamba atafufua wafu,” alisema...."nimesikia hata hapa Lindi ameshafika, sasa kamwambieni yeye si Yesu na wala hana uwezo wa kumfufua Balali,” alisema Membe.

Membe alisema kama kweli  Lowassa anaamini kwamba Balali amefichwa na serikali, basi aende akamtafute alikofichwa na amlete na kumwonyesha hadharani.

Aidha, alisema Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, wamekuwa wakidai kwamba serikali haijafanya lolote tangu uhuru wakati nao walikuwa na nafasi kubwa serikalini.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Salma Kikwete, naye aliibuka jana kwenye kampeni za Dk. Magufuli kwa mara ya kwanza na kusisitiza kuwa Dk. Magufuli ndiye chaguo bora.

Alisema rais mwenye uwezo wa kuwaletea maendeleo ya kweli na ya haraka, ni Dk. Magufuli.

Kwa upande wake, mgombea ubunge Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, alisema ingawa kuna wanaomwandama, lakini tayari yeye ndiye atakuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka mitano ijayo.

Alisema wananchi wa Lindi na Mtama wameshaamua kumpa kura zote Dk. Magufuli kwa sababu wanaami kuwa rasilimali gesi  na mafuta iliyogundulika mkoani humo itakuwa salama.

Kwa upande wake, Dk. Magufuli alisema anataka gesi iliyogunduliwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi iwanufaishe Watanzania wote wakiwamo wa mikoa hiyo.

Alisema atahakikisha makampuni ya nje yanayokuja kuwekeza kwenye mikoa hiyo yanaajiri wakazi wa mikoa hiyo kwa nafasi mbalimbali badala ya kwenda na watu wao.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwenda na wewe ndo maana ukazurumiwa Dubai

    ReplyDelete
  2. Salma nawe shule yenyewe ya kuunga unga
    JKT Ruvu
    Hata kijidploma London ukaferi
    Nashangaa kiengereza unaongea Na nani
    Usichonge tunajuwa yako Mengi
    Waachie wana Lindi wachaguwe
    Wenyewe
    Tumechoka Na wewe , mmeo. Na bi hawa bin ghasia
    Shungi hapimwishi mtoto mdogo

    Uislam si shungi
    Anaficha nini mtoto mdogo
    Tumemsomesha wenyewe mzumbe

    ReplyDelete
  3. Tutasema ya wewe Membe mkeo mwizi mwizi
    Mahotelini

    ReplyDelete
  4. Membe mkemee mkeo kabla ya Lowassa
    Ayelikuwa akiiba mataulo Na glass mahoteli yote duniani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kazi unayo,mtu mmoja comments 4 unazitofautisha dakika ili iweje,uwe unaziunganisha tu.

      Delete
  5. Police sahihi mtakuta mataulo, glass bibi keba
    Kwenye party mkeo anatisha komba kuliko komba
    Kwani nyumbani hamna vinywaji?
    Bora ulivyokatwa
    Angekuwa First Lady angeeingia kwenye word record
    Shame CCM
    Miaka yote aliyokaaaaaaa Canada

    ReplyDelete
  6. Ahahaaaaaaaaaaaaaaa eti mtayasema yote dhaaaa eti mkewe ni mwizi kwa hiyo? hamjiwi kwamba wizi nikipaji na shule? iba na wewe uone kama hautashikwa ao uauwawe. Jifunzeni kusema na muwe na heshima, mbona mmepoteza maadili ya kitanzania? hakuna heshima tena? rais Magufuli tunakuomba chukua hao vijana wote uwapeleke shule hata na hao wenye elimu ya chini. kwanio inaonesha elim ni finyu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkwewe mwizi na shule wala hakwenda finyu

      Delete
    2. maadili ya kitanzania kuwaibiya Watanzania Kila kukicha kuzurura ulaya Kwani kwenu ulaya
      Kisa kufuata dozi za HIV Kwani tujui

      Delete
    3. Ahahaaaaa pole sana kwani naona una hasira na wivu basi kama ni kutembea Ulaya au Marekani au kama unaumwa ukimwibasi sema utasaidiwa ila acha hasira na wivu. Nimekupata vizuru.

      Delete
  7. Bili lite nigenge lakuogopwa. No ndugu, nihujuma za halo ya juu kuleta mikataba hiyo nokubwa kusini ambayo ni mali yetu huko mkiwaambia watu wa Lindi n.a. mtwara kula makombo yenu.. mkiona nyusozafichwa hicho ncicho kilichojifiicha.utapeli.

    ReplyDelete
  8. CCM SERA YENU NI LOWASSA ?KILA SIKU LOWASSA
    SASA NDIO MNAJUA KUWA LOWASSA NI ZAIDI YA CCM
    MWAKA WA MABADILIKO

    ReplyDelete
  9. Huu uchaguzi ukiisha wengi watachungulia moto wa jahanamu maana wamemhasi mungu kwa kumfata shetani na watoto wake!

    ReplyDelete

Top Post Ad