Rais Kikwete Awaonya Wanaopanga Kulinda Kura Vituoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Jakaya Kikwete amesema watu wanaopanga kubaki katika vituo vya kupigia kura baada ya kumaliza zoezi hilo kwa lengo la kulinda kura kunaashiria uvunjaji amani, hivyo serikali imejipanga kupambana na hali hiyo siku ya uchaguzi.

Rais amesisitiza kwamba wanaopaswa kulinda kura ni mawakala pekee na si wafuasi wa mgombea ama vyama.

Akizungumza jana katika sherehe za Kilele cha Mwenge wa Uhuru zilizofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kiongozi huyo anayemalizia muda wake madarakani alisema viongozi wanaowaagiza wafuasi wao kulinda kura wana nia mbaya dhidi ya amani ya nchi.

“Mnatakiwa muondoke kwenye vituo baada ya kupiga kura….kura utazilindaje? Mawakala ndio pekee wanaoweza kulinda. Mkikaidi hilo, hatutawavulimia. Serikali imejipanga kupambana na wale wote watakaokaidi agizo la Tume ya Uchaguzi (NEC),” alisisitiza Rais Jakaya Kikwete.

Katika shehere hizo za mwenge zilizoendana sambamba na maadhimisho ya siku ya kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kikwete aliwataka Watanzania kuchagua watu waadilifu ambao wana dhamira ya kupambana na rushwa kwa vitendo.

“Tumchague mtu ambaye hana ukabila, udini na ubaguzi wa rangi…tumchague kiongozi atakayetetea maslahi ya makabila yote 126,” alisema rais huku akimnukuu Mwalimu Nyerere aliyefariki miaka 16 iliyopita.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa pia na Spika wa Bunge anayemaliza muda wake, Anne Makinda, wakuu wa mikoa na viongozi wengine wa ngazi tofauti serikalini na kupambwa na nyimbo za makabila na wanafunzi wa shule mbalimbali mjini Dodoma.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata hao wanaokupa medali ni wapumbavu
    Hufai hufai
    Shame on you
    Tatizo lipi mtu kulinda kura yake
    Mitambo ya uchaguzi ni fekikikiji
    Mtaiba kuraaaaaAaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukikaidi utapigwa tuu

      Delete
    2. Kwahiyo mkilinda ndio hamtaibiwa??!! Kura zinapigwa ndani, nyinyi kwa 'upumbavu' wenu mnalinda nje tena mita 100............are you serious?? Au mtatumia skype....lakini poa tu, hao 'wajeda' wote ni wageni, wamepewa mafunzo ambayo hawaja ya'practice' mtakuwa mmewasaidia sana kujipima kama 'wamekwiva'.......ASIYESIKIA LA MKUU, HUMPATA MAKUU

      Delete
    3. Kumbe medali za JK winawauma roho...SAGA CHUPA UBWIE.
      Kama mnajua mitambo ni feki na mtaibiwa kura, kuna haja gani ya nyinyi malofa kufanya kampeni? Chunga mdomo wako, kwani mdomo uliponza kichwa

      Delete
  2. Wacha wavae sare Kila kukicha wanabadili sare
    Bora pesa mngeleka hospitalini
    Shame you CCM
    Tuchague CCM tunaumwa
    Ni Lowassa Lowassa
    Badilini sare Kila kukicha ndo sera zenu

    ReplyDelete
  3. Kwa akili ya mtu mwenye akili timamu hawezi kukaa analinda kura,lazima tujiulize hivi wote tulinde kura zetu hicho kituo kitakuwaje?Je tutawekewa camera za kuona kinachoendelea huko ndani?Alichokipanga Mungu binadamu hatuwezi kukitengua,KAMWE.

    ReplyDelete
  4. Jakaya ushauri wa bure uliingia madarakani kwa nguvu ya mtaandao. Wapiga kura wanahaki ya kukaa mita 200 ongeza Na Mia watakaa.ulisilete ubabe usiobebeka. Tulikubeba 2005 ,
    2015 si ya mbebo tena its people's power (ni nguvu ya isiyo Na mtaandao wala nini)
    Watu waliochoka na ukilu timbal wa CCM. Unamaliza urais wako maliza kwa amani kama ulivyoingia usitishe watu kwakuwa una nguvu za dola.nguvu za dola zinamilikiwa Na umma
    Acha uchaguzi uwe Huru Na amani kisiwe kisingizio uvunjifu wa amani kama wimbo wenu CCM kila kukicha
    Tuachie tumchaguwe Na nani kwa mapenzi yetu
    Kwa kauri zako hizi unambeba yule uliingia Na jina kamati kuu ya CCM ,nashukuru hata huko walikuzomeo, lakini hiii it's over over jakaya
    Kama unataka kupoteza heshima yako itakuwa Mwaka huu
    Tuachie Watanzania tuchague tunayemtaka
    Na tuna mj uwa ni Nani

    ReplyDelete
  5. Huyu kiongozi ni mchochezi wa amani

    ReplyDelete
  6. MTANZANIA UNAPASWA UWE NA HESHIMA HATA KIDOGO UNAPOONGEA KWANINI TUFANANE NA MATAIFA MENGINE RAIS KIKWETE AMEFANYA MAMBO MENGI NA MAZURI, HEBU WEWE UNAYETUKANA HAPO JUU UWE NA HOFU YA MUNGU UKIINGIA WEWE MADARAKANI LEO UTAFANYA NINI. KWELI WATU WAZIMA HAO NI WAZAZI WAKO UNAWAAMBIA WAPUMBAVU? UKAWA VIPI JAMANI HATUWEZI KUEBDESHA NCHI KWA MTINDO HUU WA MATUSI. MUNGU WETU ATUSAMEHE. NAUMIA SANA SANA.

    ReplyDelete

Top Post Ad