Tamko: CUF yaipa ZEC siku tatu kukamilisha mchakato wa uchaguzi ........Isipofanya Hivyo Wananchi Wataamua Wenyewwe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema hakuna malalamiko yoyote yaliyowasilishwa katika siku ya upigaji kura.

Maalim Seif ambaye ni Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kuwa mawakala wa CCM wameitwa pamoja na maofisa wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) katika kiwanda cha Makonyo Wilaya ya Chake Chake, kwa ajili ya kujazishwa fomu za malalamiko ili ziweze kutumika kudai kuwa yalikuwepo malalamiko katika zoezi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Chama hicho zilizoko Mtendeni Mjini Zanzibar, Maalim Seif amesema njama hizo za CCM wameshazigundua na kawatozikubali.

Amesema njia pekee ya kuondosha utatanishi wa uchaguzi huo ni kukamilisha uhakiki wa majumuisho na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.

Amesema kwa upande wake pamoja na Chama chake, wataendeleza jitihada za kulipatia ufumbuzi suala hilo kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa, ili kukamilisha uhakiki wa majumuisho ya kura kwa majimbo 14 yaliyobaki na hatimaye kutangazwa mshindi wa Urais si zaidi ya tarehe 02/11/2015.

Hata hivyo amesema iwapo hakutokuwa na hatua zozote zilizochukuliwa kukamilisha uchaguzi huo na kuheshimu maamuzi ya wananchi walio wengi hadi ifikapo tarehe 01/11/2015, viongozi wa CUF wataondoa mkono wao na kuwaachia wananchi waweze kutafuta haki yao kwa njia za amani.

Katika hatua nyengine Maalim Seif ameelezea kusikitishwa na vitendo vinavyofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama kwa kuwatesa na kuwapiga raia wasiokuwa na hatia katika makaazi yao.

Amesema matukio hayo yamekuwa yakiripotiwa zaidi katika Wilaya za Magharibi “A na B”, na katika tukio la hivi karibuni amesema nyumba za raia wasiokuwa na hatia zimechomwa moto katika kisiwa cha Tumbatu na kuwafanya wananchi kuanza kupoteza uvumilivu.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Umeanza uchochezi kama kawaida yako, haandamani mtu hapa, labda wewe utangulie mbele na mkeo na watoto wako, sisi tutafuata......usitusababishie machafuko kwa umero wako wa madaraka.......kwani wewe ukishinda sisi tutapata nini?? Hebu usituchafulie hali ya hewa .......

    ReplyDelete
  2. Heeh! Kila wakati kuongea na waandishi wa habari.......huchoki babu?

    ReplyDelete
  3. Hujalazimishwa kumsikiliza akiwa anaongea,km hujisikii katafute mavi ya kuku ubanje,cc wazanzibar ndio tuna uchungu na zanzibar yetu,fala ww

    ReplyDelete

Top Post Ad