Tekno Anajua Kitu Gani Kilichomuuma Ndio Maana Anajishtukia na Kusema Ajatembea Nami Kimapenzi – Agnes Masogange Ajibu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Video vixen wa Bongo, Agnes Masogange ameonesha kupingana na kauli ya msanii wa Nigeria, Tekno Miles ambaye amekanusha kuwahi kuwa na uhusiano naye.
masogange
Drama ya Agnes mshepu na hit maker wa ‘Duro’ imeibuka baada ya Tekno kufanyiwa mahojiano na mtangazaji wa Clouds Fm, Diva kupitia kipindi cha ‘Ala Za Roho’, ambapo alikanusha kabisa kuwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na video vixen huyo.
Baada ya Tekno kukanusha, Masogange amesema kuwa Tekno anajua sababu zilizomfanya afiche ukweli kwa Diva, akimaanisha kuwa amedanganya.
Masogange ameyasema hayo kupitia post ya Instagram ambayo baadae aliifuta, aliyokuwa akimjibu shabiki mmoja mwenye jina la Instagram @diva wolfgang aliyekuwa kama akimshushua kuwa Tekno amekanusha kuwa hajawahi kudate naye.
maso
Masogange aliandika;
“Niko busy Na maisha yangu cna muda wa drama so plz hizo drama zenu hukohuko na why asiongee yote hayo b4 anajua kitu gani kilichomuuma that’s way anajishtukia ryt now niko next level “
Pia mrembo huyo alipost picha za Tbt ambazo aliwahi kuzipost kipindi alipoenda Nigeria, moja akiwa kwenye studio ya Tekno.
tekno maso-2
na nyingine akiwa kwenye kitanda kinachofanana na kile kilichoko kwenye moja ya picha za Tekno mwenyewe alizoziweka Instagram.
tekno maso
tekno room-2
Tekno pia alipost picha ya chumba chake na kuandika, “#homealone”

Inawezekana Masogange hapa anajaribu kuthibitisha kuwa wamewahi kukutana faragha, ila yaliyofanyika kwenye kitanda hicho hayatuhusu…! 
Source:Bongo5
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad