Young Dee aeleza kilichosababisha akaachana na label yake ya zamani MDB

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Young Dee ameelezea kwa uchungu kitu kilichosababisha akaachana na label yake ya zamani, Millian Dollar Boys (MDB) baada ya bosi wa kampuni hiyo, Max Rioba kudai amezingua.

Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM jana, Young Dee alisema hakutaka kuzungumzia suala la Max kwakuwa anaheshimu mchango wake katika muziki wake.

Kama uliona nimekukosea, call me, I will apologize sio kwenda kuzungumzia Instagram,” alisema Young Dee.

Kwahiyo kilichotokea mimi sitaki kumjudge labda alikuwa na hasira. Lakini mimi najua mtu wa karibu ni rahisi kukuathiri kuliko mtu wa mbali. Hayo yote mimi namshukuru kwa mabaya aliyoona kwangu. Wewe unavyotaka mabadiliko sio kila mtu anataka mabadiliko kila kitu ni wewe kama wewe. Mimi namshukuru kama alikuwa kondakta ndio amefanya mabadiliko ya kwenda kumiliki daladala,” alisema Young Dee huku akilia.

Aliongeza, “Mimi sikutaka kusema nimeondoka, sikutaka iwe hivi kwa sababu miaka mingi mimi nimeshatoka kwenye label. Mimi hadi ngoma saa nyingine nalipia mwenyewe, video nyingine tofauti, kuanzia Sio Mchoyo, Fununu. Nagonga beat tu pale halafu najilipia kila kitu. Nyimbo nyingi nataja jina la MDB lakini sio wamelipia wao. Hata ngoma yangu mpya natarajia kuiachia inaitwa ‘Ujanja Ujanja’ nimewataja lakini hawajalipia.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad