Video: Kura FEKI Zakamatwa Shuleni Bukoba Zikiwa Zimepigwa kwa Ajili ya Wagombea wa CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wilayani Bukoba, karatasi za kupigia kura ambazo ziliwekewa alama ya vema kwenye sehemu za wagombea wa udiwani, ubunge na urais, jana  ziligundulika nyuma ya bweni la Shule ya Sekondari ya Kahororo.

Karatasi hizo zilikuwa zimesambaa nyuma ya bweni la wanafunzi wa kidato cha sita, hali iliyowafanya wanafunzi wahisi kuwapo kwa karatasi zaidi ndani ya mabweni.

 Mmoja wa wanafunzi alisema karatasi hizo zilisambaa nyuma ya bweni hilo baada ya mwanafunzi mmoja kuzirusha kupitia dirishani kutokana na kutuhumiwa kutumiwa na mmoja wa wagombea kwenye jimbo hilo lenye ushindani mkali kati ya Chadema na CCM.

Mmoja wa walimu, Charles Rushinge alisema aligundua karatasi hizo wakati akikagua mazingira ya shule na baadaye kutoa taarifa kwa vyombo husika kwa ajili ya kuchukua hatua.

Hata hivyo, pamoja na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi kufika shuleni hapo kushuhudia tukio akiwa na baadhi ya maofisa usalama, bado hakuwa tayari kutoa ufafanuzi wa idadi ya karatasi za kura na chanzo cha tukio hilo.

Tukio hilo liliibuka huku yakiwepo malalamiko mengi katika vituo vya Kata ya Kashai kuwa kuna karatasi zimenyofolewa kutoka kwenye baadhi ya vitabu vya kupigia kura, ikiwa ni pamoja na kituo cha Zahanati ya Kashai na Shule ya Msingi na Mafumbo.

Mkurugenzi wa uchaguzi wa Jimbo la Bukoba Mjini, Aron Kagurumjuri aliwataka wananchi wapige kura na kudai alipokea vitabu kutoka NEC vikiwa vimefungwa kwenye maboksi, hivyo tatizo la karatasi hizo za kura si lake....Tazama  Video  hiii
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad