Mabomu ya Machozi Yarindima Mwanza Kuwatawanya Wafuasi wa Chadema Walioingia Barabarani Kushangilia Ushindi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polisi mkoani Mwanza jana walitumia mabomu ya machozi  kuwatawanya watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema  walioingia mitaani kushangilia wakiamini wagombea wao wanaongoza katika matokeo ya awali.

Tukio hilo lilitokea kwenye kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Mlimani, eneo la Butimba, Ghana na Shule ya Msingi Buzuluga kwenye majimbo ya Nyamagana na Ilemela.

Taarifa toka jijini Mwanza zinasema kundi la watu waliokuwa vituoni wakisubiri kubandikwa kwa matokeo hayo, lililipuka kwa shangwe, nderemo na shamrashamra baada ya matokeo hayo kubandikwa na wasimamizi wa uchaguzi wakiamini wagombea wao wanaongoza.

Baafa  ya  hali  hiyo, polisi waliingilia kati na kufyatua mabomu ya machozi kutawanya wafuasi hao.

Katika uchaguzi wa mwaka huu, mgombea ubunge wa Chadema na mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo la Nyamagana, Ezekiel Wenje anachuana vikali na aliyekuwa Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula wa CCM.

Katika jimbo la Ilemela, mbunge anayemaliza muda wake, Highness Kiwia wa Chadema anatetea nafasi yake kwa kupambana na mgombea wa CCM, Anjela Mabula.

Uchaguzi wa urais, ubunge na udiwani umefanyika jana Oktoba 25, mwaka huu ambapo takribani Watanzania milioni 22.7 wamejiandikisha kwenye daftari la kudumu kwa upande wa Tanzania Bara huku kwa upande wa Zanzibar zaidi ya wapigakura laki tano wamejiandikisha.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad