YAMETIMIA:Dr John Pombe Magufuli Atangazwa Rasmi Kuwa Mshindi Wa Kiti cha Urais wa Tanzania kwa Asilimia 58.45

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tume ya uchaguzi ya Tanzania Bara (NEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva   imemtangaza  Rasmi  mgombea  Urais  wa  CCM, Dr John Pombe  Magufuli  kuwa  mshindi  halali  wa  kiti  cha  Urais  katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya jumapili wiki iliyopita.

Kwa  Mujibu  wa  jaji  Lubuva, Dr  magufuli  amepata  ushindi  wa  kura Milioni 8 ( 8,882,935  ) sawa  na  asilimia  58.45%  huku  akimwacha  kwa  mbali  mpinzani  wake  wa  karibu , Edward  Lowassa (Chadema )  ambaye  amepata  jumla  ya  kura  Milioni 6 (  6,077,848  )  sawa  na  asilimia  39.97%

Dr  Magufuli  na  mgombea  mwenza, Samia Suluhu  watakabidhiwa  rasmi  vyetu  vya  ushindi  kesho  saa  nne  asubuhi  katika  ukumbi  wa  hoteli  ya  Diamond  Jubilee
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wapi ukawa na moto wa mabua, chezea ccm weye

    ReplyDelete
  2. ASANTE WALIOMPIGIA KURA MUHESHIMIWA MAGUFULI.MUNGU AWABARIKI MNO HASA PALE MLIPOTUMIA BUSARA BILA KUJALI UCHOCHEZI WA WAUME/WAZAZI.BINAFSI SIKUPIGA KURA KWA SABABU NILIKUWA NALAZIMISHWA NA MUME NIMPIGIE KURA LOWASA KWA KIAPO,SIKUWEZA NA NIKASEMA BORA NIACHE KUPIGA KURA,NILIOMBA MUNGU MAGUFURI ASHINDE NA KAJIBU MAOMBI.

    ReplyDelete
  3. HAPPY BIRTH DAY MR. PRESIDENT!!!

    ReplyDelete
  4. Hongera sana wana CCM kwa chama kuongoza kwa mara nyingine tena.Ile HAPA KAZI TU na iwe kazi kweli tukimtanguliza Muumba wetu mbele.Tumeshinda ila cha moto tumekiona na tukilegea na kuchemka itakula kwetu.Hii ni TZ mpya.R.I.P UKAWA KARIBU ACT KWA MAPAMBANO.

    ReplyDelete
  5. Shukrani za kipekee zimuendee Mzee wa Kubadilisha gia angani aka Mbowe, bila yeye kutuondolea lile 'zigo', CCM ingeonja joto ya jiwe. Kwa kweli kuna mchango wake mkubwa tu katika ushindi huu, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni......THANK YOU MR. DJ!!!!

    ReplyDelete
  6. Ni Rais wa Watanzania wote,ukubali ukatae ndio imekuwa.
    Watanzania wengi tumemkubali,hata baadhi ya wapinzani pia,NI MCHAPAKAZI,na matunda tumeyaona,afya tele na push-up kwa sana tu tofauti na upande wa pili,lakini kumbe eti tatizo chama chake anachotoka,lakini kwani si chaguzi bado zinaendelea?akichemka tunampiga chini vilevile.Mungu ibariki TANZANIA.

    ReplyDelete
  7. Hongera DR.Magufuli, hongera watanzania kwa maamuzi sahihi. Tusibweteke tuchape kazi.Maendeleo hayaji kwa ahadi za jukwaani bali kwa kazi. "TANZANIA HAPA KAZI TU"

    ReplyDelete
  8. Na hiyo kauli mbiu ya hapa kazi itekelezwe watanzania WA Leo sio WAle wa tanu yajenga nchi, usipoleta tunalotarajia kweli tutakupiga chini muheshimiwa wetu, hongera Sana rais mpya tupe Tanzania mpya na ccm mpya sio ya kurithishana vizazi vya vigogo Tu, ccm iwe ya wote PIA futa ule msemo WA ccm Ina wenyewe, tumekupa nchi mtangulize Mungu

    ReplyDelete

Top Post Ad