Balozi zatakiwa Kujipanga Kuiwakilisha Tanzania Nchi za Nje

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kufuatia agizo la Rais John Magufuli alilotoa hivi karibuni la kusitisha safari za nje kwa wizara, idara na taasisi za serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeanza kutekeleza kwa kutoa maelekezo kwa Balozi zake za nje.

Wizara hiyo imezielekeza Balozi zote zilizopo maeneo mbalimbali duniani kujipanga ili kushiriki kikamilifu katika kuiwakilisha serikali kwenye mikutano yote ya kimataifa na kikanda inayofanyika katika maeneo yao ya uwakilishi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam na wizara hiyo, imeeleza
Tanzania ina Balozi 35 zikiwamo bazozi ndogo tatu, vituo viwili vya biashara na konseli za heshima 17 katika nchi mbalimbali.

“Hizi zote zitahusika katika kuendeleza utekelezaji wa diplomasia yetu ya uchumi na uwakilishi wa maslahi ya nchi yetu,” ilieleza taarifa hiyo.
Hadi sasa mikutano ambayo tayari imefanyika na Balozi zetu kuwakilisha ni pamoja na Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea nchini Malta na Mkutano wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Habari wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika nchini Lesotho.

Aidha, imetoa wito kwa wizara, idara na taasisi za serikali kuwasilisha mapema taarifa za mikutano inayohusu sekta zao ili kutoa fursa ya kuzianyia kazi kwa wakati na kuhakikisha ushiriki wa Tanzania unakuwa wenye tija kwa taifa.

 Ilieleza kuwa wizara inaungana na wadau wengine kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua za kuleta ufanisi mkubwa wakazi na kubana matumizi ili kuiwezesha serikali kuwahudumia wananchi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Fukuza wote Kwani wamejaa watoto wa vigogo kila balozi
    Tupo Watanzania wengi ughaibuni tunajuwa lugha , tumesoma ughaibuni katika Nyanja mbali mbali tunafanya kazi za uhakika ni bora kazi hizo mtupe sisi
    Tuna uchungu Na nchi yetu Na tunawajuwa wazungu haswa

    ReplyDelete

Top Post Ad