Wimbo Mpya wa Christian Bella na Ali Kiba Washindwa Kufanya Vizuri Kwenye Radio Kama Ilivyotarajiwa..Christian Bella Afunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkali wa masauti, Christian Bella amekiri wimbo wake mpya aliomshirikisha Alikiba ''Nagharamia'' haupo kwenye mzunguko mzuri kwenye redio kama ilivyotarajiwa na kwamba ukipewa airtime utakuwa mkubwa.

Akizungumza na Bongo5 leo, Bella alieleza sababu ya kwanini wimbo huo umeshindwa kufanya vizuri kama ilivyotarajiwa ukilinganisha na ukubwa wa wasanii waliomo.

Ngoma bado haina mzunguko kusema kweli, kwa sababu ilitambulishwa redio moja tu na bado haijakaa bado kwenye promotion,amesema.

Ngoma ni nzuri na itafanya vizuri, kwa sababu kuna ngoma nyingine inatambulishwa inafanya vizuri kwa siku za mwanzoni halafu inapotea lakini hii nina uhakika itafanya vizuri kutokana na muziki mzuri tulioimba.

Ngoja video itoke halafu watu wanajua nazungumzia nini kwa sababu mapokezi ni mazuri na watu wanahitaji kinachohitajika ni promotion tu.

Pia mimi wakati wimbo unatambulishwa sikuwepo, kwahiyo mimi naona ni promotion na wiki ijayo tunapokea video, aliongeza.

Chanzo: bongo5
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad