Balaa jingine lamkumba mjumbe wa bodi TPA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Siku chache baada ya Rais John Magufuli kuvunja Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) kwa tuhuma za kushindwa kusimamia ipasayo shughuli za taasisi hiyo, mmoja wa wajumbe wake, Donata Mgassa amevuliwa uongozi wa kitengo cha manunuzi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Bodi ya TPA ilivunjwa Desemba 7 baada ya kugundulika kuwa zaidi ya makontena 2,670 yalipita Bandari ya Dar es Salaam bila kulipiwa kodi, hivyo kuikosesha Serikali mapato yake.

Kutokana na uzembe huyo, Rais aliivunja na kutengua uteuzi wa mwenyekiti wake, Profesa Joseph Msambichaka na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dk Shaaban Mwinjaka huku mkurugenzi mkuu wa TPA, Awadh Massawe akisimamishwa kazi.

Licha ya Mgassa kuwa mjumbe wa bodi hiyo, pia alikuwa meneja wa idara ya manunuzi ya UDSM.

Alipotafutwa kuzungunzia sakata hilo, kwa ufupi Mgassa alisema: “Samahani, siwezi kulizungumzia hilo.”

Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala alithibitisha kuenguliwa kwa mjumbe huyo. “Ni mabadiliko ya kawaida ambayo yanalenga kuimarisha utendaji uliotukuka wa chuo kikuu hicho,” alisema na kuongeza kuwa:

Alishamaliza muda wake ndiyo maana tukaona ni vema tubadili damu. Tumeingiza damu mpya ili kuendana na kasi ya miradi tunayotarajia kuwa nayo.”

Bila kuhusisha kilichotokea TPA, Profesa Mukandala alisema mabadiliko hayo yamefanywa kuanzia Desemba 7, siku ambayo bodi ya TPA ilivunjwa na Rais Magufuli.

Taarifa zilizopatikana kutoka vyanzo vingine chuoni hapo vinaeleza kuwa huo ni utaratibu wa siku nyingi miongoni mwa watendaji wake waandamizi na kwamba yeyote ‘anayeharibu’ sehemu moja anakotumika akiwa mjumbe wa bodi chuo pia humwajibisha.

“Ni kanuni za chuo. Asingeweza kubaki. Mara tu baada ya Rais kuvunja bodi ya Bandari chuo nacho kilitangaza kumuondoa kwenye nafasi yake. Mtu mpya ameshapatikana na ameanza kuisimamia ofisi hiyo,” kilisema chanzo hicho. Mbali na Mgassa, wajumbe wengine waliokuwa kwenye bodi hiyo ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson, Dk Francis Michael, Crescentius Magori, Flavian Kinunda, Haruna Masebu, Gema Modu na Musa Nyamsibwa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad