Header Ads Widget


Kwanini Couples Nyingi Za Vyuoni Huwa Hazidumu Hadi Ndoa Na Huishia Tu Siku Ya Graduation?


Nakumbuka Na Wengi Wenu Mtakubaliana Nami Kwa Kiasi Fulani Kuwa Humu Vyuoni Huwa Kuna Kuwa Na Couples Nyingi Ambazo Mara Nyingine Hutuaminisha Kuwa Huko Mbeleni Baada Ya Kumaliza Masomo Basi Pia Watakuja Kufunga Ndoa Na Kuishi Pamoja Kama Mume Na Mke Lakini 98.9% Ya Hizi Couples Tunazoziona au Kukutana Nazo Humu Vyuoni Huwa Zinafikia Tu Kikomo Siku Ile ya Mahafali ( Graduation ) Na Baada Ya Pale Tu Kila Mtu Ana Chapa zake lapa Na Ni Chache Sana Ambazo Huja Kuwa Real. Naomba Kujua Nini Hupelekea Hali Hii?

Kuna NJEMBA Moja Nakumbuka Ilikuwa Inatusumbua Sana Skonga Pamoja Na Demu Wake Yaani Kila Kitu Lazima Wafanye Pamoja Na Hata Wakati Mmoja Wapo Anaenda Chooni Basi Mwenzake Ataweka Gadi Nje Kumsubiri Hadi Ikawa Inatukera Sisi Masela Japo Kiasi Fulani KAWIVU Nako Kalikuwepo Kwani Hii Couple Iliishi Kama Tayari Wameshaooana. 

Kichekesho Tumemaliza Tu Kuhitimu Jumamosi Jumatano Ijayo MASELA Tunaletewa Kadi Za Mchango Wa Harusi Wa Yule Demu Na Bwana Mwingine Na Mwezi Mmoja Baadae Tena Tukaletewa Kadi Za Michango Ya Harusi Ya Yule Mwanaume Na Demu Mwingine. Tulihudhuria Hizo Harusi Zao Zote Mbili Ila Kwa Masikitiko Makubwa, Butwaa Na Mikono Ikiwa Shavuni.

Tatizo Huwa Ni Nini?

Post a Comment

4 Comments

  1. baada ya graduation tu boom linakata ndo maana mambo yanaishia hapohapo

    ReplyDelete
  2. booom likikata na mapenzi yanakata

    ReplyDelete
  3. Booom ndio kitu gani???

    ReplyDelete
  4. Mdau hujui boom

    ReplyDelete