Nyumba 100 Zawekwa X Jangwani, Vurugu Zatawala

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zoezi la uwekaji alama nyekundu katika zaidi ya nyumba 100 zinazotakiwa kubomolewa kwenye bonde la Mto Msimbazi, Jangwani limemalizika chini ya ulinzi mkali wa polisi baada ya vurugu za wananchi kuigomea serikali katika zoezi hilo.

Zoezi hilo lililoanza leo majira ya saa nne asubuhi likiongozwa na Mwanasheria wa NEMC, Machare Heche lilisababisha vurugu zilizotokana na wananchi kukataa kuwekewa alama hizo huku wakidai kuwa zoezi hilo alikustahili kufanyika kutokana na kusimamishwa kwa zoezi hilo hadi Januari mosi mwakani.

Alipohitajika kuzungumzia zoezi hilo kwakuwa alikuwepo wakati tukio zima hadi kumalizika kwakwe, Heche aligoma kuzungumzia zoezi hilo kwa kudai kuwa mzungumzaji mkuu ni Waziri anayehusika na Mazingira, January Makamba au Mkurugenzi wa NEMC.

Miongoni mwa malalamiko ya wananchi waishio katika bonde hilo ni kutaka jengo la Stendi ya mabasi yaendayo haraka pia liwekewe alama na hatimaye kubomolewa kwa sababu ya kuwa jengo hilo lipo bondeni sawa na nyumba zao,

Aidha wameiomba serikali kuongeza siku zaidi za maandalizi ili waweze kuhamisha vitu vya majumbani kwani muda uliotolewa hautoshi kufanya maandalizi.

Ikumbukwe kuwa zoezi la kubomoa nyumba zilizopo mabondeni lilianza Desemba 17 mwaka huu na kusitishwa baada ya siku tatu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi hadi Januari 5 kwa kigezo cha kutoa nafasi kwa watu waliojenga katika maeneo hayo kuondoa wenyewe mali zao .
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. poleni sana,inauma sana. lakini hamna jinsi, majipu lazima yakamuliwe.

    ReplyDelete
  2. Majipu ni lazima yakamuliwe bila kujali ukubwa na mahali jipu lilipokaa. Haya mazoeamazoea ya Watanzania kufanya vitu kwa kufuata njia za panya ndio yamelifikisha hili Taifa hapa lilipo. Kila Mafuriko yanapotokea na Watu wanapopoteza maisha unakuta Rais mzima na Mkuu wake wa Mkoa wanaenda kuwajulia hali ya kuwapa pole badala ya kuwaambia ukweli wa adhari za kujenga kwenye mabonde na kuchukua hatua stahiki. Hili liwe fundisho kwa baadhi ya Watanzania ambao wamezoea kuendesha maisha yao kiujanja ujanja.

    ReplyDelete
  3. acheni kuongea pumba hayajawakuta kuna watu kinondoni mkwajuni nyumba zimebomolewa na zipo mahali salama hakuna mafuriko

    ReplyDelete
  4. Kwani hakuna chombo kikubwa kabisa cha kisheria ambacho hawa watu wanaweza kwenda kuishtaki serikali kwa ukatili inao wafanyia wananchi wake! mbona IPTL ilipoona hapa tz haijapewa haki ikaenda ngazi za kimataifa na wakapewa haki ya kulipwa mabilioni ya shilingi hadi wakazigawa kwa mafisadi wa serikalini! na nyinyi jiungeni mwende mahakama ya kimataifa ili mjue kama serikali ipo sawa au la!! mkumbuke hata bhakhresa alisha kwenda na akalipwa iliyokuwa kamata.

    ReplyDelete
  5. JAMANI HAPO KAZI TU, WAMEAMBIWA SIKU NYINGI, LAKINI WOTE VIZIWI AJABU WENGINE BADO WAMEJENGA MWAKA JANA ,BAADA TU YA MAFURIKOM YA MWE<I APRIL MWAKA JANA WATU WAMEFYATUA TOFALI NA KUANZA UJENXI SASA NYINYI MNAFIKIRI SEREKALI IFANYEJE NA HAKUNA HATA MTU MMOJA MWENYE KIBALI CHA KUJENGA (BUILDING PERMIT)

    TUMUOMBE MUNGU LAKINI NI SHERIA WALA MAGUFULI ASILAUMIWE HIO KAULI KAIKUTA IPO KAMAILIVYO YEYE ANATEKELEZA TU. WARUDI KWO VIJIJINI KWANI WENGI WAO NI WAGENI TIKA MIKOANI WAMEFIKA NA KUVAMIA TU

    ReplyDelete
  6. Kwanza kabisa napenda kuanzia na kusema maeneo mengi ya wazi nchini yalivamiwa kwa baraka za CCM
    Wanainchi walianza na kufunguwa matawi ya wakelekwetwa wa CCM viongozi wakuu wa ccm walifunguwa matawi haya kwa vishindo
    Watu wa kaanza kujenga sehemu hizi hasa Jangwani Dar , yakawa ni mazoea mafuriko yakitokea missada inatoka serikali ya ccm ikawa inatumia mabilion ya fedha , Tanzania tuna sehem kubwa sana ya watu kuuishi sasa kwanini wasitengeze maandalizi kwa watu hawa?
    Kabla , Kama ni uvamizi ccm ni namba moja maeneo mangapi nchini yalikuwa wazi CCM imejenga ofisi zao.
    Nafikiriki hata hayo mahekalu ni kulipiza kisasi tu ,
    Yatawagharimu sana haya ccm

    ReplyDelete

Top Post Ad