AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Mkutano huo ni sehemu ya ziara ya viongozi waandamizi wa Chama na UKAWA kwa ujumla ambao watakwenda maeneo mbalimbali nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa namna walivyounga mkono upinzani na agenda nzima ya MABADILIKO katika uchaguzi mkuu uliopita na wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani kuwa ndiyo nguzo imara wanayoweza kuitegemea kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo yao na ustawi wa taifa kwa ujumla.
Itakumbukwa kuwa mbali ya Watanzania kupiga kura za ushindi katika nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu uliopita, wananchi waliwachagua wabunge wengi wa upinzani wanaotokana na UKAWA na kuongeza nguvu kubwa ndani ya bunge hususan kupitia Kambi ya Upinzani Bungeni ambayo itakuwa serikali yao mbadala huku wakiviamini vyama hivyo kusimamia na kuongoza halmashauri zipatazo 34 nchi nzima, ikiwa moja ya misingi imara katika kupigania mabadiliko ambayo Watanzania wanayataka.
Wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo kubwa ambayo ni ishara ya wazi kuwa matumaini yao kwa miaka mingine mitano yatasimamiwa na kuongozwa na upinzani imara kupitia UKAWA.
Katika ziara hiyo ya Tanga, Ndugu Lowassa ataambatana na viongozi wengine waandamizi wa UKAWA ukiwa ni mwanzo tu wa ziara kubwa itakayokwenda nchi maeneo mbalimbali nchi nzima.
Imetolewa leo Jumanne, Desemba 15, 2015 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
agenda nzima ya mabadilikoo... lowasaaaa
ReplyDeletesawa sawaa
Kila la kheri katika ziara hiyo ndug.Lowassa
ReplyDeleteAcha kiloba kunywa bia utapata mabadiliko
ReplyDeleteUlipo Tupo, HAIJALISHI.....!
ReplyDeleteNice move! Wananchi tunashukuru sana kambi ya upinzani maana changamoto wanazoipa serikali kwa kiasi kikubwa zinasaidia sana maendeleo ya nchi hii! Tunaamini mtaendelea kuipa changamoto serikali na kuibua hoja za msingi kwa maendeleo ya taifa! Haipingiki kuwa nyinyi ndiyo vinara wa mabadiliko
ReplyDeleteHahahaha kampeni zinaendelea
ReplyDeleteAmeshafunga choo lakini, hatutaki ya chato yajirudie tena
ReplyDeleteCCM Acheni ushamba mbona kinana anazunguka Kila kona
ReplyDeleteWaacheni UKAWA msaidieni magufuli kufichuwa mafisadi ndani ya CCM