Wastara Juma Akwaa Jinamizi la Usagaji..Atumiwa Picha za Utupu na Mwanamke Mwenzake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wastara
Jinamizi la usagaji limetua kwa nyota wa filamu nchini, Wastara Juma baada ya dada aliyefahamika kwa jina moja la Marry, ambaye awali alimsaidia katika matibabu, kumtaka afanye naye mapenzi ya jinsia moja, Ijumaa limenyetishiwa.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Marry ambaye anadaiwa kuishi Dubai, baada ya kuona lengo lake halijatimia, alianza kutoa maneno ya kashfa kwa Wastara kupitia mitandao ya kijamii, akidai ameingia mitini baada ya kuchukua pesa kutoka kwake.
Huyo Marry ambaye alikuwa rafiki wa Wastara anadai alimtumia pesa ili amnunulie dawa za mwanaye, lakini hakufanya hivyo na badala yake, akawa hapokei simu akipigiwa na vilevile ‘akamblock’ kwenye mtandao wa WhatsApp, ndipo huyo dada akakasirika na kuamua kuropoka,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilimtafuta Wastara na kumuuliza kuhusu ishu hiyo, ambapo alikiri kutokea, kwani Marry aliyefahamiana naye kabla hajaondoka nchini, alimtumia fedha shilingi laki tano kwa ajili ya kununua dawa za mwanaye, lakini alipomtaka amuelekeze kwa ndugu zake wanaoishi Kenya ili azipeleke, alikataa.

Wakati nilipokwenda Kenya kwenye matibabu ya mguu wangu, alinitumia tena shilingi laki mbili kunisaidia, lakini siku chache baadaye nikaanza kushangaa ananipigia simu na kunitumia picha akiwa mtupu, akinishawishi tufanye mapenzi ya jinsia moja, kitu ambacho kiliniudhi na kuamua kuacha kupokea simu zake na pia nikamzuia katika akaunti yangu ya WhatsApp,” alisema Wastara.
Kwa upande wake, Marry kupitia mawasiliano kwa njia ya mtandao huo, alionesha kushangazwa kwake na mabadiliko ya tabia ya Wastara, kitu ambacho hata hivyo hakimshtui isipokuwa anahitaji kurejeshewa fedha zake.

Sasa sielewi kwa nini tangu nimtumie zile pesa hataki kuongea na mimi, hayo mambo ya usagaji hata sielewi maana mimi ni mwanamke, nina jinsia moja, sina jinsia ya kiume, nitafanyaje mapenzi na yeye, nachotaka anipe pesa zangu, simuogopi hata kidogo,” alisema.
GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu naye ana nini kika Leo jamani
    Tutoleeni uchafu huu
    Hatupendi kumtukana

    ReplyDelete
  2. Anayataka mwenyewe huyu
    Kila kukicha skandali

    ReplyDelete
  3. Anayataka huyu
    Fyuuuuuuuuu
    Kila kukicha scandalllllllllloy

    ReplyDelete
  4. Ana laana huyu bibi

    ReplyDelete
  5. Hakuna haja ya kumtolea maneno makali. Inaonekana hayuko sawa kisaikolojia baada ya matukio yale mawili. La kukatwa mguu na kuondokewa na mmewe kipenzi.
    Hivyo ushauri wangu apate Ushauri Nasaha. Maana hata mimi binafsi nahisi hayuko sawa, haiwezekani kila siku ni yeye tu kwenye Media.
    Dada Wastara Ushauri Nasaha unahitajika kwako tena wa haraka. Kwa upeo wangu mdogo wa Saikolojia hayo matatizo yako yanaweza kumharibu hata mwanao.

    ReplyDelete

Top Post Ad