Zaidi ya Watu 1500 Wajitangaza Kuwa MASHOGA Mkoani Iringa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kukithiri  kwa biashara haramu ya ngono pamoja na tabia ya ushoga mkoani Iringa kunadaiwa kusababishwa na baadhi ya vijana wa vyuo vikuu waonafika mkoani humo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu, huku miongoni mwao wakitaka starehe zilizo nje ya uwezo wao.

Tamaa ya kumiliki vitu vya thamani – ni miongoni mwa mambo yanayotajwa  kuwahadaa baadhi ya wasomi hao wa vyuo vikuu, jambo linalosababisha wengi wao kuangukia katika wimbi la biashara ya ngono na ushoga na kuufanya  ongezeko la maambukzi ya vvu.

Kwa mkoa wa iringa inadaiwa kuwa zaidi ya mashoga 1500 wamejitangaza wenyewe kuendesha  biashara haramu ya ngono, jambo ambalo kiafya linadaiwa kuwa ni hatari  kwa maambukizi ya virus vya ukimwi.

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu  mkoani iringa ndiyo wanaonyooshewa kidole kuhusika na biashara hiyo ya ngono na tabia ya ushoga- ambapo shirika la restless development linalojihusisha na masuala ya afya ya uzazi na makuzi kwa vijana- kupitia mradi wa dance for life- limewakutanisha viongozi hawa wa serikali ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa- ili  kujadili namna ya kujinasua katika wimbi hilo la ushoga na biashara haramu ya ngono.

Serikali inaona  tatizo hilo la ushoga na biashara ya ngono litamalizwa na jamii yenyewe, endapo tu wazazi na  walezi watakemea mapema mienendo hatarishi ya vijana wao.

Ushoga ni tabia inayofanywa na baadhi ya wanaume, kwa  kujihusisha kimapenzi na wanaume wenzao, suala  ambalo kwa kiwango kikubwa linatajwa kuchochewa na mambo ya utandawazi, ambao unaibua mitindo mbalimbali na tabia mpya kila uchwao.

Chanzo :Star tv
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ushoga Upo hasa CCM
    Tangu awamu ya pili
    Awamu ya nne
    Nasikia hata awamu ya tano
    Watu weshanunuliwa nyumba Dubai bibi kufunga mdomo
    London ndo kwenyewe shoga
    Ushoga Upo tena Upo sana
    Tanzania ushoga si ugonjwa Upo toka ikulu hadi Mtaani

    ReplyDelete
    Replies
    1. tehetehetehetehetehetehe uwiiiiiii ikulu tena kuwe na ushoga we una balaa

      Delete
  2. Nyinyi semeni ushoga Upo tangu gomora Na sodoma
    Na ushoga wajuwao wawili kitandani
    Msione Mtu baunza nje kitandani mwanamke kushinda mwanamke

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha taifa likiwa na watu hao.Je wanawake watafanywa nini?wazazi elimisheni vijana wenu.wasiige utamaduni wa Ulaya kwao ni jambo la kawaida.Fateni Muumba wenu alivyowaumba nyinyi ni wanaume.Je munamkosoa Muumba?Basi adhabu itawapata ya maradhi duniani na akhera anajua Muumba atakavyo walipa.

    ReplyDelete
  4. Chaa naona aibu hats kusoma hizo comment hapo juu ushoga ulaaniwe milele ulaya matajiri utibabu bure je bongo be careful

    ReplyDelete

Top Post Ad