Hii Ndio Sababu ya Rais Magufuli Kumuongezea Mwaka Mmoja Mkuu wa Majeshi Jenerali David Mwamunyange..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

RAIS John Magufuli amemwongeza muda wa mwaka mmoja Mkuu wa  majeshi ya ulinzi nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya kutimiza umri  kwa mujibu wa katiba na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyopo  Upanga jijini Dar es salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi la ulinzi nchini  pamoja na Meneja Jenerali  wawili  ambapo wote kwa  pamoja wamestaafu ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo.

“Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016,lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 30 januari,2016 hadi tarehe  31 Januari 2017,” amesema Jenerali Mwamunyange

Jeneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo .

Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange amesema Rais Magufuli amemteua  Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Safi sana,hata angemuongeza miaka 5 mbona poa tuu.

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa David Mwamunyange anayo kila sababu ya kuongezewa muda kwasababu utendaji kazi wake ni mzuri sana. Hongea sana kaka yetu Mwamunyange kwa kuinda Taifa letu.

    ReplyDelete

Top Post Ad