JE Umewahi Kusikia Tetesi Kuwa Mwigizaji Ray na Chuchu Hans Wamemwagana? Basi Chuchu Hans Kasema Haya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chuchu Hans na Ray Mahabani
Msanii wa filamu nchini, Chuchu Hans amesema bado yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Vicent Kigosi aka Ray licha ya hivi karibuni baadhi ya watu kudai wawili hao hawapo tena pamoja.

Akizungumza katika kipindi cha Take One cha Clouds TV Jumanne hii, Chuchu alisema toka aanze kutoka kimapenzi na staa huyo mengi yamezushwa juu yake.

Sasa hivi haya mambo ya mitandao yanapotosha sana jamii na watu wanataka ufanye kile wanachotaka,” alisema. “Sijaachana Ray na wala hatuna mpango huo sema kuna baadhi ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wanataka tuishi maisha yao kitu ambacho hakiwezekani.

Pia Chuchu alisema madai ya kuachana na Ray yamekuja baada ya kufuta baadhi ya taarifa za mpenzi wake katika mtandao wa kijamii.
Chuchu Hans Katika Pozi

Sisi tulikuwa na utaratibu mimi nikipost kitu na Ray anapost kitu lakini baada ya kuacha watu wakajua si tumeachana lakini sisi tupo safi kabisa,” alisisitiza Chuchu.

Hata hivyo mwanadada huyo amewataka watu wa kwenye mitandao ya kijamii kuacha tabia za kumtukania wazazi wake pamoja na ndugu zake kwani wao hawahusiani na mambo yake binafsi.

Udaku Special Blog
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Fashion police boot la winter ndani ya summer time Bongo rahaaaa,,,sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau tueleweshe vizuri unalisifia au unaliponda hilo police fashion winter boot

      Delete

Top Post Ad