Mapya Kuhusu Chama cha Mapinduzi CCM Kuazimisha Kumbukumbu ya Kuzaliwa ya Miaka 39

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Chama Cha Mapinduzi kila mwaka huadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Februari 05, 1977. Mwaka huu kitakuwa kinatimiza miaka 39.

UZINDUZI
Uzinduzi wa maadhimisho ya kumbukumbu ya hiyo utafanyika tarehe 31 Januari, 2016 Unguja, Zanzibar ambapo Mgeni rasmi atakuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein.

KILELE CHA SHEREHE
Kilele cha maadhimisho hayo Februari 06, 2016 mjini Singida ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete.

Viongozi wa kitaifa na baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu watakaohudhuria watapangiwa shughuli za ujenzi wa Chama na Taifa kwa ujumla katika wilaya zote za mkoa wa Singida siku tatu kabla ya kilele cha maadhimisho hayo.

Mikoa yote iandae shughuli mahsusi kwa wiki nzima ya maadhimisho hayo, mkazo ukiwa ni kufanya shughuli za ujenzi wa Chama na Taifa katika maeneo yao, Mambo ya kuzingatia katika wiki hiyo ni kama ifuatavyo:-

i. Kuingiza wanachama wapya wa CCM na Jumuiya zake na kufanya shughuli nyingine za kuimarisha Chama.

ii. Kufanya mikutano ya kuwashukuru wana CCM na wananchi kwa kuiamini CCM kuendelea kuongoza Nchi yetu kwa kushiriki na kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo CCM ilipata ushindi wa kishindo wa Rais, Wabunge na Madiwani.

iii. Kuhamasisha wananchi kufanya kazi ili kujiletea maendeleo yao binafsi na ya Taifa.

iv. Kushiriki shughuli za maendeleo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa, zahanati, vituo vya afya, upandaji miti, uchimbaji wa mitaro ya maji, kufanya USAFI wa mazingira pamoja na shughuli nyingine za kijamii.

KAULIMBIU
Kaulimbiu ya sherehe hizo ni “Sasa Kazi, Kujenga Nchi na Kukijenga Chama”.

Nape Moses Nnauye (Mb.), 
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
13/01/2016

Udaku Special Blog

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mnalazimisha ili CCM ionekane imeshika hatamu ZNZ

    ReplyDelete
  2. ALUTA CONTINUA COMRADES, hakuna haja ya kurumbana na watu, yale yaliyoazimiwa yafanyike kwa uhakika akusema na discourage waacheni na yao kwani hawawezi fika popote.Kazeni uzi kwa sheria hizi zilizopo kwani zilipuuzwa na zifuatwa na kusimamiwa vizuri, aaaah mwendo mdundo. Wakwepa kodi na wezi wa makontena tutaona sasa jeuri yao.

    ReplyDelete
  3. Nnauye hajaacha nafasi ya Uenezi NIMSAIDIE?

    ReplyDelete

Top Post Ad