SAKATA la Bomoa Bomoa Nyumba ya Mchungaji Getrude Rwakatare Mapya yaibuka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mvutano kati ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutaka kubomoa nyumba anayoishi Mchungaji Getrude Rwakatare umezidi kushika kasi mahakamani.

Hali hiyo ilitokea jana, baada ya wakili wa familia ya Mchungaji Rwakatare, Emmanuel Agustino kupinga maombi ya NEMC ya kutaka kuongezewa muda wa kuwasilisha maombi ya mapitio ya hukumu ya maridhiano inayozuia baraza hilo kuchukua hatua yoyote dhidi ya nyumba hiyo.

Hukumu hiyo ya maridhiano ilitokana na kesi iliyofunguliwa 2012 katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi na Robert Brighton, ambaye ni mtoto wa Mchungaji Rwakatare aliyepinga kubomolewa kwa nyumba hiyo kwa madai kuwa imejengwa mahali pasiporuhusiwa.
Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Hamisa Kalombola Mei 11, 2015, pamoja na mambo mengine, alisema pande zote zilikubaliana kuwa, NEMC na wadau wake wasimbughudhi Brighton katika makazi hayo.

Hata hivyo, Desemba 29, 2015, NEMC ilifungua tena maombi ya kutaka kupatiwa kibali cha kuongezewa muda wa kuwasilisha maombi ya kufanya mapitio ya hukumu hiyo.

Katika maombi hayo namba 825 ya mwaka 2015, NEMC inadai kutoitambua hukumu hiyo na kwamba, uamuzi huo ulifikiwa na mwanasheria wake ambaye hakupatiwa idhini na NEMC.

Hata hivyo, wakati maombi hayo yalipotajwa mahakamani hapo Jumatatu wiki hii, Wakili Agustino kwa niaba ya mjibu maombi (Brighton), aliwasilisha hati ya kiapo kinzani dhidi ya hati ya kiapo cha NEMC kilichoapwa na Mkurugenzi wake Mtendaji, Bonaventure Baya akipinga maombi hayo ya NEMC.

Jaji John Mugeta anayesikiliza shauri hilo, aliamuru watoa maombi wawasilishe mahakamani hapo majibu ya kiapo kinzani cha mjibu maombi kabla ya Januari 20 na akapanga kusikiliza maombi hayo Januari 21, 2016.

Udaku Special Blog
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jamani mi naona ibomolewe tu kuleta usawa bona wengine wamebomolewa

    ReplyDelete
  2. Na ibomolewe tu maana hakuna namna

    ReplyDelete
  3. BOMOABOMOA ISIWE
    KWA WANYONGE TU,HII NYUMBA INATAKIWA IBOMOLEWE,MAMA KUWA NA HOFU YA MUNGU,NYUMBA HAIKO KISHERIA BALI PESA ILITUMIKA.

    ReplyDelete
  4. Ngoja tusikilizie,na lisipobomolewa hili jengo nitaamini kuna kulindana ndani ya CCM.

    ReplyDelete
  5. HATA IWE NYUMBA YA NANI KAMA HAIKO KISHERIA BOMOA TU KAMA KWELI MNATENDA HAKI KWENYE HILI ZOEZI.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  6. wataelewana tu na muafaka upatikane, lakini wasipoivunja italeta kozaazaa,kwani wengine wamevunjiwa tayari
    mimi napita tu

    ReplyDelete
  7. HAKI ITENDEKE !!!!

    ReplyDelete
  8. Kwani ikiachwa mnapungukiwa na nini? Hao waliobomolewa Mungu hawezi kuwapa tena? Mbona mnaenenda kwa mwili? Hakuna mwenye haki hata mmoja. Sasa haki itendeke haki gani? Wewe kama umebomolewa nyumba yako mwombe Mungu atakupa nyingine

    ReplyDelete

Top Post Ad